< Zaburi 21 >

1 Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mfalme anashangilia katika uweza wako, Yahwe! Ni kwa namna kuu anashangilia katika wokovu uliouleta!
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa!
2 Wewe umempa yeye matamanio ya moyo wake na hauja mkatalia maombi midomo yake.
Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake.
3 Kwa kuwa wewe unamletea baraka nyingi; wewe uliweka katika kichwa chake taji ya dhahabu iliyo safi kabisa.
Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
4 Yeye alikuomba wewe maisha; ukampatia maisha; wewe ulimpatia maisha malefu milele na milele.
Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele.
5 Yeye utukufu wake ni mkuu kwa sababu ya ushindi wako; wewe umemuwekea mapambo na enzi.
Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu.
6 Kwa kuwa unampatia yeye baraka za kudumu; unamfurahisha kwa furaha ya uwepo wako.
Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako.
7 Kwa kuwa Mfalme humwamini Yahwe; kwa kupitia uaminifu wa agano la aliye juu zaidi yeye hataondolewa.
Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.
8 Mkono wako utawakamata adui zangu wote wote; mkono wako wa kuume utawakamata wale wote wanao kuchukia.
Mkono wako utawashika adui zako wote, mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.
9 Wakati wa hasira yako, wewe utawachoma kama katika tanuru la moto. Yahwe atawamaliza wao katika hasira yake, na moto utawateketeza upesi wao.
Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza.
10 Wewe utawaangamiza watoto wao duniani na ukoo wao kutoka katika mrorongo wa wanadamu.
Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, uzao wao kutoka wanadamu.
11 Kwa kuwa walikusudia kukufanyia mambo maovu wewe; wao walitunga njama ambayo kwayo hawawezi kufanikiwa!
Ingawa watapanga mabaya dhidi yako na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,
12 Kwa kuwa wewe utawarudisha nyuma; wewe utafyatua upinde wako mbele yao.
kwa kuwa utawafanya wakimbie utakapowalenga usoni pao kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.
13 Uninuliwe, Yahwe, katika uweza wako; tutaimba na kusifu nguvu zako.
Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako.

< Zaburi 21 >