< Zaburi 150 >

1 Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu za ukuu wake.
הללו-יה הללו-אל בקדשו הללוהו ברקיע עזו
2 Msifuni yeye kwa matendo yake makuu; msifuni yeye kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.
הללוהו בגבורתיו הללוהו כרב גדלו
3 Msifuni kwa mlipuko wa pembe; msifuni kwa kinanda na kinubi.
הללוהו בתקע שופר הללוהו בנבל וכנור
4 Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa vyombo vya nyuzi na filimbi.
הללוהו בתף ומחול הללוהו במנים ועגב
5 Msifuni kwa matoazi yavumayo; msifuni kwa matoazi avumayo sana.
הללוהו בצלצלי-שמע הללוהו בצלצלי תרועה
6 Kila kilicho na pumzi kimsifu Yahwe. Msifuni Yahwe.
כל הנשמה תהלל יה הללו-יה

< Zaburi 150 >