< Zaburi 149 >
1 Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu.
Msifuni Bwana. Mwimbieni Bwana wimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.
2 Israeli ishangilie katika yeye aliye iumba; watu wa Sayuni na washangilie katika mfalme wao.
Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.
3 Nao walisifu jina lake kwa kucheza; na wamuimbie sifa yeye kwa ngoma na kinubi.
Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi.
4 Kwa kuwa Yahwe hupata furaha katika watu wake; huwapa utukufu wanyeyekevu kwa wokovu.
Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.
5 Wacha Mungu wauchangilie ushindi; nao waimbe kwa furaha vitandani mwao.
Watakatifu washangilie katika heshima hii, na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.
6 Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na panga mbili zenye makali mkononi mwao
Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,
7 kutekeleza kisasi juu ya mataifa na matendo ya adhabu juu ya watu.
ili walipize mataifa kisasi na adhabu juu ya mataifa,
8 Nao watawafunga wafalme wao kwa minyororo na wakuu wao kwa pingu za chuma. Watatekeleza hukumu ambayo imeandikwa.
wawafunge wafalme wao kwa minyororo, wakuu wao kwa pingu za chuma,
9 Hii itakuwa ni heshima kwa ajili ya watakatifu wake wote. Msifuni Yahwe.
ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao. Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote. Msifuni Bwana.