< Zaburi 148 >

1 Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe, ninyi mlio katika mbingu; msifuni yeye, ninyi mlio juu.
הללו-יה הללו את-יהוה מן-השמים הללוהו במרומים
2 Msifuni yeye, enyi malaika wake wote; msifuni yeye, majeshi ya malaika wake wote.
הללוהו כל-מלאכיו הללוהו כל-צבאו
3 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi; msifuni yeye, nyota zote zing'aazo.
הללוהו שמש וירח הללוהו כל-כוכבי אור
4 Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu zaidi na maji yaliyo juu ya anga.
הללוהו שמי השמים והמים אשר מעל השמים
5 Na vilisifu jina la Yahwe, maana aliamuru, navyo vikaumbwa.
יהללו את-שם יהוה כי הוא צוה ונבראו
6 Pia ameviimrisha milele na milele; naye alitoa amri ambayo haitabadilika.
ויעמידם לעד לעולם חק-נתן ולא יעבור
7 Msifuni yeye kutoka nchi, ninyi viumbe wa baharini na viumbe vyote katika kina cha bahari,
הללו את-יהוה מן-הארץ-- תנינים וכל-תהמות
8 moto na mvua ya mawe, theluji na mawingu, upepo wa dhoruba ukitimiza neno lake.
אש וברד שלג וקיטור רוח סערה עשה דברו
9 Msifuni yeye, enyi milima na vilima, miti ya matunda na mierezi yote,
ההרים וכל-גבעות עץ פרי וכל-ארזים
10 wanyama pori na wanyama wafugwao, viumbe vitambaavyo na ndege.
החיה וכל-בהמה רמש וצפור כנף
11 Msifuni Yahwe, wafalme wa nchi na mataifa yote, wakuu na watawala wote wa nchi,
מלכי-ארץ וכל-לאמים שרים וכל-שפטי ארץ
12 wote vijana wa kiume na vijana wa kike, wazee na watoto.
בחורים וגם-בתולות זקנים עם-נערים
13 Na walisifu jina la Yahwe, kwa kuwa jina lake pekee limetukuka na utukufu wake umeongezwa juu ya nchi na mbingu.
יהללו את-שם יהוה-- כי-נשגב שמו לבדו הודו על-ארץ ושמים
14 Naye ameyainua mapembe ya watu wake kwa ajili ya sifa kutoka kwa waaminifu wake wote, Waisraeli, watu wa karibu naye. Msifuni Yahwe.
וירם קרן לעמו תהלה לכל-חסידיו-- לבני ישראל עם קרבו הללו-יה

< Zaburi 148 >