< Zaburi 141 >

1 Ee Yahwe, ninakulilia wewe; uje upesi kwangu. Unisikilize nikuitapo.
上主,我呼求您,請求速來救助我;上主,我呼求您,請您聽我的呼號。
2 Maombi yangu na yawe kama uvumba mbele zako; mikono yangu iliyoinuliwa na iwe kama dhabihu ya jioni.
願我向您的祈禱,像馨香上升;願我的手高舉,如同晚祭的高騰。
3 Ee Yahwe, uweke mlinzi kinywani mwangu; mngojezi malangoni pa midomo yangu.
上主,求您在我的口邊派守衛,求您在我的唇前派警備。
4 Usiruhusu tamaa ya moyo wangu kutamani uovu wowote wala kushiriki katika matendo ya dhambi na watu waishio maovuni. Nisile vyakula vyao vya anasa.
莫讓我的心傾向邪道,免得我再去犯罪作惡;莫讓我與惡人同作壞事,免得我嚐食他們的美味。
5 Mwenye haki na anipige; nao utakuwa ni wema kwangu. Anirudi; itakuwa kama mafuta kichwani pangu; kichwa changu na kisikatae kupokea. Lakini maombi yangu siku zote yatakuwa dhidi ya matendo yao mauvu.
義人責打我,算是我的恩遇,他責斥我,是給我頭的傅油。我的頭也決不會加以抗拒,我仍然為迫害我的人祈求。
6 Viongozi wao watatupwa chini toka juu mlimani; watayasikia maneno yangu kuwa ni matamu.
當他們的首領被拋於巖石時,纔感覺到我的話是如何甘飴。
7 Watalazimika kusema, “Kama vile jembe moja livunjapo ardhi, hivyo mifupa yetu imesambaratishwa kinywani pa kuzimu.” (Sheol h7585)
他們的骨頭被棄置在陰府門旁,像人耕地掘田,將土塊任意拋放。 (Sheol h7585)
8 Hakika macho yangu yanakutazama wewe, Yahwe, Bwana; katika wewe napata kimbilio; usiiache nafsi yangu.
上主天主,我的雙目一直仰望你,我信賴你,不要將我的靈魂拋棄。
9 Unilinde dhidi ya mitego waliyoiweka kwa ajili yangu, na matanzi yao watendao maovu.
求你保護我免陷於他們為我設的網羅,求你使我能夠脫離為非作歹者的圈套。
10 Waovu na waangukie kwenye nyavu zao wenywe pindi mimi nitorokapo.
願惡人一起墮入自設的網羅,而我卻得以安然無恙地脫逃。

< Zaburi 141 >