< Zaburi 140 >

1 Yahwe, uniokoe dhidi ya waovu; unikinge dhidi ya watu wenye vurugu.
(Til Sangmesteren. En Salme af David.) Red mig, HERRE, fra onde Mennesker, vær mig et Værn mod Voldsmænd,
2 Wao wanapanga uovu mioyoni mwao; wanasababisha mapigano kila siku.
der pønser på ondt i Hjertet og daglig ægger til Strid.
3 Ndimi zao zinajeruhi kama nyoka; sumu ya fira imo midomoni mwao. (Selah)
De hvæsser Tungen som Slanger, har Øglegift under deres Læber. (Sela)
4 Ee Yahwe, unilinde dhidi ya mikono ya waovu; unikinge na vurugu za watu wanaopanga kuniangusha.
Vogt mig, HERRE, for gudløses Hånd, vær mig et Værn mod Voldsmænd, som pønser på at bringe mig til Fald.
5 Wenye majivuno wameweka mtego kwa ajili yangu; wameeneza nyavu; wameweka kitanzi kwa ajili yangu. (Selah)
Hovmodige lægger Snarer og Strikker for mig, breder et Net for min Fod, lægger Fælder for mig ved Vejen. (Sela)
6 Nilimwambia Yahwe, “Wewe ni Mungu wangu; usikie kilio changu unihurumie.”
Jeg siger til HERREN: Du er min Gud, HERRE, lyt til min tryglende Røst!
7 Ee Yahwe, Bwana wangu, wewe ni mwenye nguvu uwezaye kuniokoa; hunifunika ngao kichwa changu siku ya vita.
HERRE, Herre, min Frelses Styrke, du skærmer mit Hoved på Stridens Dag.
8 Ee Yahwe, usiyatimize matakwa ya waovu; usiruhusu njama zao kufanikiwa. (Selah)
Opfyld ej, HERRE, den gudløses Ønsker, lad ikke hans Råd have Fremgang!
9 Wale wanao nizunguka huinua vichwa vyao; madhara ya midomo yao wenyewe na yawafunike.
Lad dem ikke løfte Hovedet mod mig, lad deres Trusler ramme dem selv!
10 Makaa ya moto na yawaangukie; uwatupe motoni, kwenye shimo refu, wasiweze kuinuka tena.
Det regne på dem med gloende Kul, styrt dem i Dybet, ej stå de op!
11 Watu wenye ndimi na wasifanywe salama juu ya nchi; na uovu umuwinde kumpiga mtu mwenye vurugu mpaka afe.
Lad ikke Bagtaleren holde sig i Landet, ondt ramme Voldsmanden Slag i Slag!
12 Ninajua kuwa Yahwe atahukumu kwa haki walioteswa, na kuwa atawapa haki wahitaji.
Jeg ved, at HERREN vil føre de armes Sag og skaffe de fattige Ret.
13 Hakika watu wenye haki watalishukuru jina lako; watu wanyoofu wataishi uweponi mwako.
For vist skal retfærdige prise dit Navn, oprigtige bo for dit Åsyn.

< Zaburi 140 >