< Zaburi 135 >

1 Msifuni Yahwe. Lisifuni jina la Yahwe. Msifuni yeye, enyi watumishi wa Yahwe,
你们要赞美耶和华! 你们要赞美耶和华的名! 耶和华的仆人站在耶和华殿中; 站在我们 神殿院中的,你们要赞美他!
2 ninyi msimamao katika nyumba ya Yahwe, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.
3 Msifuni Yahwe, kwa kuwa ni mwema; liimbieni sifa jina lake, maana ni vizuri kufanya hivyo.
你们要赞美耶和华! 耶和华本为善; 要歌颂他的名, 因为这是美好的。
4 Kwa kuwa Yahwe amemchagua Yakobo kwa ajili yake mwenyewe, Israeli kama urithi wake.
耶和华拣选雅各归自己, 拣选以色列特作自己的子民。
5 Najua ya kuwa Yahwe ni mkuu, na kwamba Bwana wetu yuko juu ya miungu yote.
原来我知道耶和华为大, 也知道我们的主超乎万神之上。
6 Chochote Yahwe apendacho, hufanya mbinguni, duniani, katika bahari na katika vilindi vyote.
耶和华在天上,在地下, 在海中,在一切的深处, 都随自己的意旨而行。
7 Hushusha mawingu kutoka mbali, akifanya mianga ya radi kuongozana na mvua na kuleta upepo toka katika ghala yake.
他使云雾从地极上腾, 造电随雨而闪, 从府库中带出风来。
8 Aliua mzaliwa wa kwanza wa Misri, wote wanadamu na wanyama.
他将埃及头生的, 连人带牲畜都击杀了。
9 Alituma ishara na maajabu kati yako Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
埃及啊,他施行神迹奇事, 在你当中,在法老和他一切臣仆身上。
10 Aliwashambulia mataifa mengi na aliua wafalme wenye nguvu,
他击杀许多的民, 又杀戮大能的王,
11 Sihoni mfalme wa Waamori na Ogu mfalme wa Bashani na falme zote za Kanaani.
就是亚摩利王西宏和巴珊王噩, 并迦南一切的国王,
12 Alitupatia sisi nchi yao kama urithi, urithi wa Israeli watu wake.
将他们的地赏赐他的百姓以色列为业。
13 Jina lako, Yahwe, inadumu milele; Yahwe, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.
耶和华啊,你的名存到永远! 耶和华啊,你可记念的名存到万代!
14 Kwa kuwa Bwana huwatetea watu wake na anahuruma juu ya watumishi wake.
耶和华要为他的百姓伸冤, 为他的仆人后悔。
15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
外邦的偶像是金的,银的, 是人手所造的;
16 Sanamu hizo zina vinywa, lakini haziongei; zina macho, lakini hazioni;
有口却不能言, 有眼却不能看,
17 zina masikio, lakini hazisikii, wala vinywani mwao hamna pumzi.
有耳却不能听, 口中也没有气息。
18 Wale wazitengenezao wanafanana nazo, vilevile kila anaye zitumainia.
造他的要和他一样, 凡靠他的也要如此。
19 Enyi kizazi cha Israeli, mtukuzeni Yahwe; kizazi cha Haruni, mtukuzeni Yahwe.
以色列家啊,你们要称颂耶和华! 亚伦家啊,你们要称颂耶和华!
20 Kizazi cha Lawi, mtukuzeni Yahwe.
利未家啊,你们要称颂耶和华! 你们敬畏耶和华的,要称颂耶和华!
21 Atukuzwe Yahwe katika Sayuni, yeye aishiye Yerusalemu. Msifuni Yahwe.
住在耶路撒冷的耶和华 该从锡安受称颂。 你们要赞美耶和华!

< Zaburi 135 >