< Zaburi 134 >
1 Njoni, mtukuzeni Yahwe, enyi nyote watumishi wa Yahwe, ninyi mnaotumika hekaluni mwa Yahwe wakati wa usiku.
Wimbo wa kwenda juu. Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.
2 Inueni mikono yenu patakatifu pake na mtukuzeni Yahwe.
Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu Bwana.
3 Mungu na awabariki toka Sayuni, yeye aliye ziumba mbingu na nchi.
Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni.