< Zaburi 125 >
1 Wale wamwaminio Yahwe ni kama mlima Sayuni, hautikisiki, wadumu milele.
上行之诗。 倚靠耶和华的人 好像锡安山,永不动摇。
2 Kama milima inavyo izunguka Yerusalemu, hivyo ndivyo Yahwe anavyo wazunguka watu wake sasa na hata milele.
众山怎样围绕耶路撒冷, 耶和华也照样围绕他的百姓, 从今时直到永远。
3 Fimbo ya uovu haitatawala katika nchi ya wenye haki. Vinginevyo wenye haki wanaweza kukosea.
恶人的杖不常落在义人的分上, 免得义人伸手作恶。
4 Ee Yahwe, utende wema kwa wale walio wema na wale walio wanyoofu mioyoni mwao.
耶和华啊,求你善待那些为善 和心里正直的人。
5 Lakini kwa wale wanaogeukia njia zao za upotovu, Yahwe atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli.
至于那偏行弯曲道路的人, 耶和华必使他和作恶的人一同出去受刑。 愿平安归于以色列!