< Zaburi 124 >

1 “Kama Yahwe asingekuwa upande wetu,” Israeli na aseme sasa,
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa:
2 “Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu,
kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia,
3 basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu.
wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai,
4 Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia.
mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika,
5 Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha.”
maji yaendayo kasi yangalituchukua.
6 Atukuzwe Yahwe, ambaye hajaruhusu tuwe mawindo kwa meno yao.
Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.
7 Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka.
Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka.
8 Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.
Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.

< Zaburi 124 >