< Zaburi 122 >
1 Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.”
大衛上行之詩。 人對我說:我們往耶和華的殿去, 我就歡喜。
2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako!
耶路撒冷啊, 我們的腳站在你的門內。
3 Ee Yerusalemu, uliojengwa kama mji uliopangiliwa kwa umakini!
耶路撒冷被建造, 如同連絡整齊的一座城。
4 Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe.
眾支派,就是耶和華的支派,上那裏去, 按以色列的常例稱讚耶和華的名。
5 Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
因為在那裏設立審判的寶座, 就是大衛家的寶座。
6 Ombeni kwa ajili ya amani ya Yerusalemu! “Wote wakupendao wawe na amani.
你們要為耶路撒冷求平安! 耶路撒冷啊,愛你的人必然興旺!
7 Amani iwepo ndani ya kuta zako ili ikutetee, na wawe na amani ndani ya ngome zako.”
願你城中平安! 願你宮內興旺!
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu nitasema, “Amani iwe ndani yenu.”
因我弟兄和同伴的緣故,我要說: 願平安在你中間!
9 Kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu, nitatafuta mema kwa ajili yako.
因耶和華-我們上帝殿的緣故, 我要為你求福!