< Zaburi 115 >

1 Sio kwetu, Yahwe, sio kwetu, bali kwa jina lako ulete heshima, kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na uaminifu wako.
Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi, bali utukufu ni kwa jina lako, kwa sababu ya upendo na uaminifu wako.
2 Kwa nini mataifa yalazimike kusema, “Yuko wapi Mungu wako?”
Kwa nini mataifa waseme, “Yuko wapi Mungu wao?”
3 Mungu wetu aliye mbinguni; hufanya chochote apendacho.
Mungu wetu yuko mbinguni, naye hufanya lolote limpendezalo.
4 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5 Sanamu hizo zina vinywa, lakini haziongei; zina macho, lakini hazioni;
Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona;
6 zina masikio, lakini hazisikii; zina pua lakini hazinusi.
zina masikio, lakini haziwezi kusikia, zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7 Sanamu hizo zina mikono, lakini hazishiki; zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala haziongei kutoka viywani mwao.
zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8 Wale wanao zitengeneza wanafanana nazo, vile vile yeyote anaye amini katika hizo.
Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
9 Israeli, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.
10 Nyumba ya Haruni, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.
11 Ninyi mnao mheshumu Yahwe, mwamini yeye; yeye ni msaada wenu na ngao yenu.
Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana, yeye ni msaada na ngao yao.
12 Yahwe hutukumbuka sisi na atatubariki; ataibariki familia ya Israeli; atabariki familia ya Haruni.
Bwana anatukumbuka na atatubariki: ataibariki nyumba ya Israeli, ataibariki nyumba ya Aroni,
13 Atawabariki wale wanao muheshimu yeye, wote vijana na wazee.
atawabariki wale wanaomcha Bwana, wadogo kwa wakubwa.
14 Yahwe na awaongeze ninyi zaidi na zaidi, ninyi pamoja na watoto wenu.
Bwana na awawezeshe kuongezeka, ninyi na watoto wenu.
15 Yahwe na awabariki, aliyeziumba mbingu na nchi.
Mbarikiwe na Bwana Muumba wa mbingu na dunia.
16 Mbingu ni za Yahwe; lakini nchi amewapa wanadamu.
Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana, lakini dunia amempa mwanadamu.
17 Wafu hawamsifu Yahwe, wala wote washukao chini kwenye ukimya;
Sio wafu wanaomsifu Bwana, wale washukao mahali pa kimya,
18 bali tutamtukuza Yahwe sasa na hata milele. Msifuni Yahwe.
bali ni sisi tunaomtukuza Bwana, sasa na hata milele. Msifuni Bwana.

< Zaburi 115 >