< Mithali 9 >
1 Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo saba kutoka katika miamba.
2 Ameandaa wanyama wake kwa chakula cha usiku; ameichanganya divai yake; na kuandaa meza yake.
3 Amewatuma watumishi wake kupeleka mialiko na kutoka mahali pa juu sana kwenye mji anaita:
4 “Wale wasiofunzwa waje hapa!” anawaambia wale wasionaufahamu.
5 Njoo, ule chakula, na unywe divai nimeshaichanganya.
6 Acheni njia zenu za kijinga, na mkaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
7 Yeyote amrekebishaye mwenye dhihaka hukaribisha matusi na yeyote anayemshutumu mtu mbaya atapata madhara.
8 Usimshutumu mwenye dhihaka, ama atakuchukia; mshutumu mtu mwenye busara, naye atakupenda.
9 Mpe mafundisho mtu mwenye busara, naye atakuwa na busara zaidi; mfundishe mtu mwenye haki, naye ataongeza elimu.
10 Hofu ya Mungu ni chanzo cha hekima na maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu.
11 Maana kwa njia yangu siku zako zitazidishwa na uzima wako utaongezewa miaka.
12 Kama unahekima, unahekima kwako mwenyewe, lakini ukidharau, utaibeba peke yako.
13 Mwanamke mpumbavu anakelele nyingi- hajafunzwa wala haelewi chochote.
14 Anakaa kwenye mlango wa nyumba yake, kwenye kiti cha sehemu ya juu sana ya mji.
15 Anawaita kwa sauti wanaopita karibu, watu wale wanaotembea wima katika njia zao.
16 Wale ambao hamjafunzwa njoni hapa ndani!” anawaambia wale wasio na akili. “
17 Maji ya kuiba ni matamu na mkate unaoliwa kwa siri unapendeza.”
18 Lakini hajui kwamba wafu wapo pale, wageni wake wapo kwenye vina vya kuzimu. (Sheol )