< Mithali 7 >

1 Mwanangu, yatunze maneno yangu na ndani yako udhihifadhi amri zangu.
Mwanangu, shika maneno yangu na kuzihifadhi amri zangu ndani yako.
2 Uzilinde amri zangu ili uishi na uyatunzetu mafundisho yangu kama mboni ya jicho.
Shika amri zangu nawe utaishi; linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.
3 Uyafunge katika vidole vyako; uyaandike katika kibao cha moyo wako.
Yafunge katika vidole vyako; yaandike katika kibao cha moyo wako.
4 Mwambie hekima, “wewe ni dada yangu,” na ufahamu mwite jamaa yako,
Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,” uite ufahamu jamaa yako;
5 ili ujitunze mwenyewe dhidi ya mwanake haramu, dhidi ya mwanamke mgeni mwenye maneno laini.
watakuepusha na mwanamke mzinzi, kutokana na mwanamke mpotovu na maneno yake ya kubembeleza.
6 Nilikuwa naangalia kwenye wavu wa dirisha la nyumba yangu.
Kwenye dirisha la nyumba yangu nilitazama nje kupitia upenyo kwenye mwimo wa dirisha.
7 Nikawatazama watu mwenye ukosefu wa uzoefu, na miongoni mwa watu vijana nikamwona kijana asiye na akili.
Niliona miongoni mwa wajinga, nikagundua miongoni mwa wanaume vijana, kijana asiye na akili.
8 Kijana huyo alishuka mtaani kwenye kona karibu na yule mwanamke, akaenda kwenye nyumba yake.
Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake, akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke
9 Ilikuwa katika utusiutusi wa siku muda wa jioni, wakati wa usiku na giza.
wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake, giza la usiku lilipokuwa likiingia.
10 Akakutana na yule mwanake, amevaa kama kahaba, katika moyo wa udanyanyifu.
Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki, hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
11 Alikuwa na kelele na upotovu; miguu yake haikutulia kwenye masikani.
(Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi, miguu yake haitulii nyumbani;
12 Alielekea mitaani, kisha sehemu ya sokoni, na katika kila upande alisubiri kwa kuviza.
mara kwenye barabara za mji, mara kwenye viwanja vikubwa, kwenye kila pembe huvizia.)
13 Basi akamshika na kumbusu, kwa uso wa nguvu akamwambia,
Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu, na kwa uso usio na haya akamwambia:
14 leo nimetoa sadaka yangu ya amani, nimelipa nadhili yangu,
“Nina sadaka za amani nyumbani; leo nimetimiza nadhiri zangu.
15 hivyo nilikuja kukutana nawe, kuutafuta uso wako kwa hamu, na sasa nimekupata.
Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki; nimekutafuta na nimekupata!
16 Nimeweka matandiko juu ya kitanda changu, kitani za rangi kutoka Misri.
Nimetandika kitanda changu kwa kitani za rangi kutoka Misri.
17 Kitanda changu nimenyunyizia manemane, udi na mdalasini.
Nimetia manukato kitanda changu kwa manemane, udi na mdalasini.
18 Njoo, tunywe tujishibishe kwa upendo wetu hata asubuhi; tupate furaha kuu kwa matendo ya mahaba.
Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi; tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!
19 Maana mume wangu hayupo nyumbani kwake; amekwenda safari ya mbali.
Mume wangu hayupo nyumbani; amekwenda safari ya mbali.
20 Alichukua mkoba wa fedha; atarudi siku ya mwezi mpevu.
Amechukua mkoba uliojazwa fedha na hatakuwepo nyumbani karibuni.”
21 katika maneno yake mengi akamshinda; na kwa midomo yake laini anampotosha.
Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha; alimshawishi kwa maneno yake laini.
22 Ghafula alimfuata kama maksai anayekwenda kwa mchinjaji, kama ayala aliyekamatwa kwa nguvu,
Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke kama fahali aendaye machinjoni, kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
23 mpaka mshale upasue ini lake. Alikuwa kama ndege anayekimbili kwenye mtego. Hakujua kuwa itamgharimu maisha yake.
mpaka mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake.
24 Na sasa, wanangu, nisikilizeni; zingatieni maneno ya kinywa changu.
Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo.
25 Moyo wako usiyageukie mapito yake; usipotoshwe katika mapito yake.
Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake.
26 Amesababisha watu wengi kuanguka kwa kuwajeruhi; ameua watu wengi.
Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa.
27 Nyumba yake ipo juu ya barabara ya kwenda kuzimu; huelekea chini kwenye vyumba vya mauti. (Sheol h7585)
Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti. (Sheol h7585)

< Mithali 7 >