< Mithali 5 >

1 Mwanangu, zingatia hekima yangu; sikiliza kwa makini ufahamu wangu,
Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,
2 ili ujifunze busara na midomo yako iweze kuhifadhi maarifa.
ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa.
3 Maana midomo ya malaya hutiririsha asali na kinywa chake ni laini kuliko mafuta,
Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4 lakini mwishoni anakuwa mchungu kama mnyoo, hukata kama upunga mkali.
lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili.
5 Miguu yake huelekea mauti; hatua zake huelekea njia yote ya kuzimu. (Sheol h7585)
Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. (Sheol h7585)
6 Hafikirii njia ya uzima. Hatua za miguu yake hupotea, maana hajui anakwenda wapi.
Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.
7 Sasa, wanangu, nisikilizeni; wala msiache kusikiliza maneno ya kinywa changu.
Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia.
8 Lindeni njia yenu mbali naye wala msiende karibu na mlango wa nyumba yake.
Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake,
9 Kwa njia hiyo hamtawapa wengine heshima yenu au miaka ya uzima wenu kwa mtu mkatiri;
usije ukatoa nguvu zako nzuri kwa wengine na miaka yako kwa aliye mkatili,
10 wageni usije kufanya karamu kwa utajiri wenu; kazi mliyoifanya haitaenda katika nyumba ya wageni.
wageni wasije wakasherehekea utajiri wako na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine.
11 Mwishoni mwa maisha yenu mtajuta ambapo nyama na mwili wenu vitaangamia.
Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
12 Nanyi mtasema, “Namna gani nilichukia fundisho na moyo wangu ulidharau sahihisho!
Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!
13 Sikuweza kuwatii walimu wangu au kuwasikiliza walionielekeza.
Sikuwatii walimu wangu wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
14 Nilikuwa nimeharibika kabisa katikati ya kusanyiko, miongoni mwa makutano ya watu.”
Nimefika ukingoni mwa maangamizi kabisa katikati ya kusanyiko lote.”
15 Munywe maji kutoka kwenye birika lenu mwenyewe na munywe maji yanatiririka kutoka kwenye kisima chenu.
Kunywa maji kutoka kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kwenye kisima chako mwenyewe.
16 Je inapaswa chemichemi yenu ifurike popote na mifereji yenu ya maji itiririke katika njia kuu?
Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani?
17 Yawe yenu wenyewe peke yenu wala si kwa wageni.
Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni.
18 Chemichemi yako ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.
Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.
19 Maana ni ayala apendezaye na kulungu mwenye uzuri. Matiti yake na yakujaze furaha muda wote; daima na utekwe na upendo wake.
Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.
20 Mwanangu, kwa nini uwe mateka wa malaya, kwa nini uyakumbatie matiti ya mwanamke mgeni?
Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?
21 Yehova huona kila kitu afanyacho mtu na huangalia mapito yake yote.
Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Bwana, naye huyapima mapito yake yote.
22 Mtu mwovu atatekwa na makosa yake mwenyewe; kamba za dhambi yake zitamnasa kwa nguvu.
Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.
23 Atakufa kwa kukosa maonyo; atapotelea mbali kwa upumbavu wake wingi.
Atakufa kwa kukosa nidhamu, akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.

< Mithali 5 >