< Mithali 30 >

1 Maneno ya Aguri mwana wa Yake - mausia: Mtu huyu alimwambia Ithieli, kwa Ithiel na Ukali:
Misemo ya Aguri mwana wa Yake, usia: Huyu mtu alimwambia Ithieli, naam, kwa Ithieli na kwa Ukali:
2 Hakika nipo kama mnyama kuliko mwanadamu na sina ufahamu wa wanadamu.
“Mimi ni mjinga kuliko wanadamu wote; sina ufahamu wa kibinadamu.
3 Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya Mtakatifu.
Sijajifunza hekima, wala sina maarifa ya kumjua yeye Aliye Mtakatifu.
4 Je ni nani amekwenda juu mbinguni na kurudi chini? Je ni nani aliyekusanya upepo kwenye mikono yake? Je ni nani aliyekusanya maji kwenye kanzu? Je ni nani aliyeziimarisha ncha za dunia yote? Jina lake ni nani, na jina la mtoto wake ni nani? Hakika unajua!
Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? Ni nani ameshakusanya upepo kwenye vitanga vya mikono yake? Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? Niambie kama unajua!
5 Kila neno la Mungu limejaribiwa, yeye ni ngao kwa wale wanaokimbilia kwake.
“Kila neno la Mungu ni kamilifu; yeye ni ngao kwa wale wanaomkimbilia.
6 Usiyaongezee maneno haya, au atakukemea, na utathibitishwa kuwa mwongo.
Usiongeze kwenye maneno yake, ama atakukemea na kukuthibitisha kuwa mwongo.
7 Vitu viwili ninakuomba, usivikatalie kwangu kabla sijafa:
“Ninakuomba vitu viwili, Ee Bwana; usininyime kabla sijafa:
8 Majivuno na uongo viweke mbali nami. Usinipe umasikini wala utajiri, nipe tu chakula ninachohitaji.
Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku.
9 Maana nikipata vingi zaidi, nitakukana wewe na kusema, “Yehova ni nani?” Au kama nitakuwa masikini, nitaiba na kukufuru jina la Mungu wangu.
Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘Bwana ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.
10 Usimkashifu mtumwa mbele ya bwana wake, au atakulaani na utapata hatia.
“Usimchongee mtumishi kwa bwana wake, asije akakulaani, ukapatilizwa kwalo.
11 Kizazi ambacho kinachomlaa baba yao na hakimbariki mama yao,
“Wako watu wale ambao huwalaani baba zao na wala hawawabariki mama zao;
12 kizazi hicho ni safi katika macho yao wenyewe, lakini hawajaoshwa uchafu wao.
wale ambao ni safi machoni pao wenyewe kumbe hawakuoshwa uchafu wao;
13 Hicho ni kizazi- jinsi gani macho yao yanakiburi na kope zao zimeinuka juu! -
wale ambao daima macho yao ni ya kiburi, ambao kutazama kwao ni kwa dharau;
14 kuna kizazi ambacho meno yao ni upanga, na mifupa ya taya zao ni visu, ili waweze kumrarua masikini wamtoe duniani na mhitaji atoke miongoni mwa wanadamu.
wale ambao meno yao ni panga na ambao mataya yao yamewekwa visu kuwaangamiza maskini katika nchi, na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu.
15 Ruba anamabinti wawili, “Toa na Toa” wanalia. Kuna vitu vitatu ambavyo havitosheki, vinne ambavyo havisememi, “Inatosha”:
“Mruba anao binti wawili waliao, ‘Nipe! Nipe!’ “Kuna vitu vitatu visivyotosheka kamwe, naam, viko vinne visivyosema, ‘Yatosha!’:
16 Kuzimu, tumbo tasa, nchi yenye kiu kwa maji, na moto usiosema, “Inatosha.” (Sheol h7585)
Ni kaburi, tumbo lisilozaa, nchi isiyoshiba maji kamwe, na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ (Sheol h7585)
17 Jicho ambalo linamdhihaki baba na kudharau utii kwa mama, macho yake yatadonolewa na kunguru wa bondeni, na ataliwa na tai.
“Jicho lile limdhihakilo baba, lile linalodharau kumtii mama, litangʼolewa na kunguru wa bondeni, litaliwa na tai.
18 Kuna vitu vitatu ambavyo vinanishangaza, vinne ambavyo sivifahamu:
“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana, naam, vinne nisivyovielewa:
19 njia ya tai angani; njia ya nyoka juu ya mwamba; njia ya meli kwenye moyo wa bahari; na njia ya mtu pamoja mwanake kijana.
Ni mwendo wa tai katika anga, mwendo wa nyoka juu ya mwamba, mwendo wa meli katika maji makuu ya bahari, nao mwendo wa mtu pamoja na msichana.
20 Hii ni njia ya mzinzi- anakula na kufuta kinywa chake na kusema, “sijafanya ubaya wowote.”
“Huu ndio mwendo wa mwanamke mzinzi, hula akapangusa kinywa chake na kusema, ‘Sikufanya chochote kibaya.’
21 Chini ya vitu vitatu dunia hutetemeka na vinne haiwezi kuvivumilia:
“Kwa mambo matatu nchi hutetemeka, naam, kwa mambo manne haiwezi kuvumilia:
22 mtumwa anapokuwa mfalme; mpumbavu anaposhiba vyakula;
Mtumwa awapo mfalme, mpumbavu ashibapo chakula,
23 mwanamke anayechukiwa anapoolewa; kijakazi anapochukua nafasi ya mkuu wake.
mwanamke asiyependwa aolewapo, naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake.
24 Vitu vinne duniani ni vidogo na bado vinabusara:
“Vitu vinne duniani vilivyo vidogo, lakini vina akili nyingi sana:
25 mchwa ni viumbe ambao sio imara, lakini huandaa chakula chao wakati wa hari,
Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.
26 Wibari siyo viumbe wenye nguvu, lakini hutengeneza makazi yake kwenye miamba.
Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba.
27 Nzige hawana mfalme, lakini wote wanamwendo wa mpangilio.
Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi.
28 Kama mjusi, unaweza kumkunja kwa mikono yako miwili, lakini wanapatikana katika majumba ya wafalme.
Mjusi anaweza kushikwa kwa mkono, hata hivyo huonekana katika majumba ya kifalme.
29 Kuna vitu vitatu ambavyo ni fahari katika mwendo na vinne ambavyo ni fahari katika namna ya kutembea:
“Viko vitu vitatu ambavyo vinapendeza katika mwendo wao, naam, vinne ambavyo hutembea kwa mwendo wa madaha:
30 simba, aliyeimara miongoni mwa wanyama- wala hajiepushi na kitu chochote;
simba, mwenye nguvu miongoni mwa wanyama, asiyerudi nyuma kwa chochote;
31 jogoo anayetembea kwa mikogo; mbuzi; na mfalme ambaye askari wapo kando yake.
jogoo atembeaye kwa maringo, pia beberu, naye mfalme pamoja na jeshi lake lililomzunguka.
32 Kama umekuwa mpumbavu, jitukuze mwenyewe, au kama umekuwa ukisimamia vibaya- weka mkono wako juu ya kinywa chako.
“Ikiwa umefanya upumbavu na ukajitukuza mwenyewe, au kama umepanga mabaya, basi funika mdomo wako na mkono wako.
33 Kama kusuka maziwa hufanya siagi na pua ya mtu hutoa damu kama imepigwa, basi matendo yanayofanywa kwa hasira huzalisha mafarakano.
Kwa maana kama vile kusukasuka maziwa hutoa siagi, na pia kule kufinya pua hutoa damu, kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.”

< Mithali 30 >