< Mithali 29 >
1 Mtu aliyepokea makaripio mengi lakini anashupaza shingo yake atavunjika ndani ya muda mfupi na hata pona.
2 Watenda mema wanapoongezeka, watu wanafurahi, bali wakati mtu mwovu anapotawala, watu huugua.
3 Mwenye kupenda hekima baba yake anafurahi, bali anayeshikamana na makahaba huuharibu utajiri wake.
4 Mfalme huimarisha nchi kwa haki, bali mwenye kudai rushwa huirarua.
5 Mtu anayejipendekeza kwa jirani yake anatandaza wavu kwenye miguu yake.
6 Mtu mbaya hunaswa kwenye mtego wa dhambi yake mwenyewe, bali yeye atendaye haki huimba na kufurahi.
7 Atendaye haki hutetea madai ya masikini; mtu mwovu hafahamu maarifa kama hayo.
8 Mwenye dhihaka huutia moto mji, bali wale wenye busara huigeuza ghadhabu.
9 Mtu mwenye busara anapojadiliana na mpumbavu, hughadhabika na kucheka, hakutakuwa na utulivu.
10 Mkatili humchukia mwenye ukamilifu na hutafuta maisha ya mwenye haki.
11 Mpumabavu huonyesha hasira yake, bali mtu mwenye busara huishikilia na kujituliza mwenyewe.
12 Kama matawala atazinagatia uongo, maafisa wake wote watakuwa waovu.
13 Mtu masikini na mkandamizaji wanafanana, maana Yehova huyapa nuru macho yao wote.
14 Kama mfalme atamhukumu masikini kwa uaminifu, kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele.
15 Fimbo na maonyo huleta hekima, bali mtoto huru mbali na makaripio humwaibisha mama yake.
16 Watu waovu wanapotawala, uovu huongezeka, bali wenye kutenda haki wataona anguko la watu waovu.
17 Mwadibishe mwanao naye atakupa pumziko; ataleta furaha katika maisha yako.
18 Pasipo na maono ya kinabii watu huenda bila utaratibu, bali mwenye kuitunza sheria amebarikiwa.
19 Mtumwa hawezi kurekebishwa kwa maneno, maana ingawa anaelewa, hakuna mwitikio.
20 Je unamwona mtu mwenye haraka katika maneno yake? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
21 Mwenye kumdekeza mtumwa wake tangu ujana, mwisho wake itakuwa taabu.
22 Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi na bwana mwenye hasira sana hutenda dhambi nyingi.
23 Kiburi cha mtu humshusha chini, bali mwenye roho ya unyenyekevu atapewa heshima.
24 Anayeshirikiana na mwizi huyachukia maisha yake mwenyewe; husikia laana na wala hasemi chochote.
25 Kumwogopa binadamu ni mtego, bali mwenye kumtumaini Yehova atalindwa.
26 Wengi huutafuta uso wa mtawala, bali kutoka kwa Yehova huja haki kwa ajili yake.
27 Mtu dhalimu ni chukizo kwa wenye kutenda haki, bali mwenye njia ya haki ni chukizo kwa watu waovu.