< Mithali 18 >
1 Yule ambaye hujitenga hutafuta matakwa yake mwenyewe na hupingana na hukumu zote za kweli.
2 Mpumbavu hapati raha katika ufahamu, lakini hufunua kile kilichopo katika moyo wake.
3 Mtu mwovu anapokuja, dharau huja pamoja naye- sambamba na aibu na shutuma.
4 Maneno ya kinywa cha mtu ni maji yenye kina kirefu; chemchemi ya hekima ni mkondo unaotiririka.
5 Si vema kuwa na upendeleo kwa mwovu, wala haifai kukana haki kwa wale watendao mema.
6 Midomo ya mpumbavu huletea mafarakano na kinywa chake hukaribisha mapigo.
7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na hujinasa mwenye kwa midomo yake.
8 Maneno ya mmbea ni kama chembe tamu na hushuka katika sehema za ndani sana kwenye mwili.
9 Basi, ambaye ni mzembe katika kazi yake ni ndugu yake anayeharibu wengi.
10 Jina la Yehova ni mnara imara; atendaye haki hukimbilia na kuwa salama.
11 Mali ya tajiri ni mji wake imara na katika fikira zake ni kama ukuta mrefu.
12 Moyo wa mtu huwa na kiburi kabla ya anguko lake, bali unyenyekevu hutangulia kabla ya heshima.
13 Anayejibu kabla ya kusikiliza- ni upuuzi na aibu yake.
14 Roho ya mtu itajinusuru na madhara, bali roho iliyopondeka nani anaweza kuivumilia?
15 Moyo wa mwenye akili hujipatia maarifa na usikivu wa mwenye busara huitafuta.
16 Zawadi ya mtu inaweza kufungua njia na kumleta mbele ya mtu muhimu.
17 Wa kwanza kujitetea katika shitaka lake huonekana kuwa na haki hadi mpinzani wake aje na kumuuliza maswali.
18 Kupiga kura kunamaliza mabishano na kuwatawanya wapinzani imara.
19 Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kushawishiwa kuliko mji wenye nguvu, na kugombana ni kama makomeo ya ngome.
20 Tumbo la mtu litashiba kutoka kwenye tunda la kinywa chake; atatoshelezwa kwa mavuno ya midomo yake.
21 Uzima na kifo hutawaliwa kwa ulimi, na wale wenye kuupenda ulimi watakula tunda lake.
22 Yeye apataye mke anapata kitu chema na kupokea fadhila kutoka kwa Yehova.
23 Mtu masikini huomba rehema, lakini mtu tajiri hujibu kwa ukali.
24 Anayejidai kwa marafiki wengi watamleta katika uharibifu, bali yupo rafiki ambaye huwa karibu kuliko ndugu.