< Mithali 15 >
1 Jawabu la upole huondoa ghadhabu, bali neno la ukatili huchochea hasira.
回答柔和,使怒消退; 言語暴戾,觸動怒氣。
2 Ulimi wa watu mwenye hekima husifu maarifa, bali kinywa cha wapumbavu humwaga upuuzi.
智慧人的舌善發知識; 愚昧人的口吐出愚昧。
3 Macho ya Yehova yapo kila mahali, yakiwatazama juu ya waovu na wema.
耶和華的眼目無處不在; 惡人善人,他都鑒察。
4 Ulimi unaoponya ni mti wa uzima, bali ulimi wa udanganyifu huvunja moyo.
溫良的舌是生命樹; 乖謬的嘴使人心碎。
5 Mpumbavu hudharau marudi ya baba yake, bali yeye anayejifunza kutokana na masahihisho ni mwenye hekima.
愚妄人藐視父親的管教; 領受責備的,得着見識。
6 Katika nyumba ya wale watendao haki kuna hazina kubwa, bali mapato ya watu waovu huwapa taabu.
義人家中多有財寶; 惡人得利反受擾害。
7 Midomo ya wenye hekima husambaza maarifa, bali mioyo ya wapumbavu haifanyi hivyo.
智慧人的嘴播揚知識; 愚昧人的心並不如此。
8 Yehova anachukia sadaka za watu waovu, bali maombi ya watu waadilifu ndiyo furaha yake.
惡人獻祭,為耶和華所憎惡; 正直人祈禱,為他所喜悅。
9 Yehova anachukia njia ya watu waovu, bali anampenda yule ambaye huandama haki.
惡人的道路,為耶和華所憎惡; 追求公義的,為他所喜愛。
10 Marudi ya ukatili hungojea kwa yeyote ambaye huiacha njia na yule ambaye huchukia masahihisho atakufa.
捨棄正路的,必受嚴刑; 恨惡責備的,必致死亡。
11 Kuzimu na uharibifu vipo wazi mbele za Yehova; je si zaidi sana mioyo ya wana wa wanadamu? (Sheol )
陰間和滅亡尚在耶和華眼前, 何況世人的心呢? (Sheol )
12 Mwenye mzaha huchukia masahihisho; hatakwenda kwa wenye hekima.
褻慢人不愛受責備; 他也不就近智慧人。
13 Moyo wenye furaha husababisha uchangamfu wa uso, bali huzuni huvunja moyo.
心中喜樂,面帶笑容; 心裏憂愁,靈被損傷。
14 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa, bali kinywa cha wapumbavu hujilisha kwenye upuuzi.
聰明人心求知識; 愚昧人口吃愚昧。
15 Siku zote za watu waliokandamizwa ni taabu, bali moyo wenye furaha unakaramu daima.
困苦人的日子都是愁苦; 心中歡暢的,常享豐筵。
16 Bora kitu kidogo pamoja na kumcha Mungu kuliko hazina kubwa pamoja na ghasia.
少有財寶,敬畏耶和華, 強如多有財寶,煩亂不安。
17 Bora mlo wenye mboga kukiwa na upendo kuliko kuandaliwa ndama aliyenona kwa chuki.
吃素菜,彼此相愛, 強如吃肥牛,彼此相恨。
18 Mtu mwenye hasira huchochea mabishano, bali mtu ambaye hukawia kukasirika hutuliza ugomvi.
暴怒的人挑啟爭端; 忍怒的人止息紛爭。
19 Mapito ya mtu goigoi ni kama sehemu yenye uwa wa miiba, bali mapito ya mtu mwadilifu ni njia kuu iliyojengwa imara.
懶惰人的道像荊棘的籬笆; 正直人的路是平坦的大道。
20 Mwana mwenye busara huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.
智慧子使父親喜樂; 愚昧人藐視母親。
21 Upuuzi humfurahia mtu ambaye amepungukiwa akili, bali mwenye ufahamu hutembea katika njia nyofu.
無知的人以愚妄為樂; 聰明的人按正直而行。
22 Mipango huharibika ambapo hakuna ushauri, bali washauri wengi wanafanikiwa.
不先商議,所謀無效; 謀士眾多,所謀乃成。
23 Mtu anapata furaha wakati anapotoa jibu la kufaa; je ni zuri kiasi gani neno kwa wakati muafaka!
口善應對,自覺喜樂; 話合其時,何等美好。
24 Njia ya uzima huwapeleka juu watu wenye hekima, ili waondoke kutoka chini kuzimu. (Sheol )
智慧人從生命的道上升, 使他遠離在下的陰間。 (Sheol )
25 Yehova hurarua urithi wa mwenye kiburi, bali huzilinda mali za mjane.
耶和華必拆毀驕傲人的家, 卻要立定寡婦的地界。
26 Yehova huyachukia mawazo ya watu waovu, bali maneno ya upole ni safi.
惡謀為耶和華所憎惡; 良言乃為純淨。
27 Mporaji huleta shida kwenye familia yake, bali yeye ambaye huchukia rushwa ataishi.
貪戀財利的,擾害己家; 恨惡賄賂的,必得存活。
28 Moyo wa yule atendaye haki hutafakari kabla ya kujibu, bali kinywa cha watu waovu humwanga ubaya wake wote.
義人的心,思量如何回答; 惡人的口吐出惡言。
29 Yehova yupo mbali na watu waovu, bali husikia maombi ya wale watendao haki.
耶和華遠離惡人, 卻聽義人的禱告。
30 Nuru ya macho huleta furaha moyoni na habari njema ni afya kwenye mwili.
眼有光,使心喜樂; 好信息,使骨滋潤。
31 Kama utazingatia wakati mtu anapokurekebisha jinsi ya kuishi, utabaki miongoni mwa watu wenye busara.
聽從生命責備的, 必常在智慧人中。
32 Yeye anayekataa karipio hujidharau mwenyewe, bali yule asikilizaye masahihisho hujipatia ufahamu.
棄絕管教的,輕看自己的生命; 聽從責備的,卻得智慧。
33 Kumcha Yehova hufundisha hekima na unyenyekevu huja kabla ya heshima.
敬畏耶和華是智慧的訓誨; 尊榮以前,必有謙卑。