< Wafilipi 3 >
1 Hatimaye, ndugu zangu furahini katika Bwana. Sioni usumbufu kuwaandikia tena maneno yaleyale. Haya mambo yatawapa usalama.
As to the rest, my brethren, rejoice in the Lord; the same things to write to you to me indeed is not tiresome, and for you [is] sure;
2 Jihadharini na mbwa. Jihadharini na watenda kazi wabaya. Jihadharini na wale wajikatao miili yao.
look to the dogs, look to the evil-workers, look to the concision;
3 Kwa kuwa sisi nndiyo tohara. Sisi ndiyo huwa tumwabudu Mungu kwa msaada wa Roho. Tujivuniao katika Kristo Yesu, na ambao hatuna ujasiri katika mwili.
for we are the circumcision, who by the Spirit are serving God, and glorying in Christ Jesus, and in flesh having no trust,
4 Hata hivyo, kama kungekuwa na mtu wa kuutumainia mwili huu, mimi ningeweza kufanya hivyo zaidi.
though I also have [cause of] trust in flesh. If any other one doth think to have trust in flesh, I more;
5 Kwani nilitahiriwa siku ya nane, nilizaliwa katika kabila la Waisraeli. Ni wa kabila la Benjamini. Ni Mwebrania wa waebrani. Katika kuitimiza haki ya sheria ya Musa, nilikuwa, Farisayo.
circumcision on the eighth day! of the race of Israel! of the tribe of Benjamin! a Hebrew of Hebrews! according to law a Pharisee!
6 Kwa juhudi zangu nililitesa Kanisa. Kwa tuitii haki ya sheria, sikuwa na lawama kisheria.
according to zeal persecuting the assembly! according to righteousness that is in law becoming blameless!
7 Lakini katika mambo yote niliyoyaona kuwa ya faida kwangu mimi, niliyahesabu kama takataka kwa sababu ya kumfahamu Kristo.
But what things were to me gains, these I have counted, because of the Christ, loss;
8 Kwa kweli, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kutokana ubora wa kumjua wa Kristo Yesu Bwana wangu. Kwa ajili yake nimeaacha mambo yote, nayahesabu kama takataka ili nimpate Kristo
yes, indeed, and I count all things to be loss, because of the excellency of the knowledge of Christ Jesus my Lord, because of whom of the all things I suffered loss, and do count them to be refuse, that Christ I may gain, and be found in him,
9 na nionekane ndani yake. Sina haki yangu binafisi kutoka katika sheria, bali ninayo haki ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, itokayo kwa Mungu, yenye msingi katika imani.
not having my righteousness, which [is] of law, but that which [is] through faith of Christ — the righteousness that is of God by the faith,
10 Sasa nataka kumfahamu yeye na nguvu ya ufufuo wake na ushirika wa mateso yake. Nataka kubadilishwa na Kristo katika mfano wa kifo chake,
to know him, and the power of his rising again, and the fellowship of his sufferings, being conformed to his death,
11 angalau niweze kuwa na matumaini katika ufufuo wa wafu.
if anyhow I may attain to the rising again of the dead.
12 Siyo kweli kwamba tayari nimeishayapata mambo hayo, au kwamba nimekuwa mkamilifu katika hayo. Bali najitahidi ili niweze kupata kile kupata kile nilichopatikana na Kristo Yesu.
Not that I did already obtain, or have been already perfected; but I pursue, if also I may lay hold of that for which also I was laid hold of by the Christ Jesus;
13 Ndugu zangu, sidhani kwamba nimekwisha kupata mambo haya. Bali nafanya jambo moja: nasahau ya nyuma nayatazamia ya mbele.
brethren, I do not reckon myself to have laid hold; and one thing — the things behind indeed forgetting, and to the things before stretching forth —
14 Najitahidi kufikia lengo kusudi ili nipate tuzo ya juu ya wito wa Mungu katika Kristo Yesu.
to the mark I pursue for the prize of the high calling of God in Christ Jesus.
15 Sote tulio ukulia wokovu, tunapaswa kuwaza namna hii. Na ikiwa mwingine atafikiri kwa namna iliyotofauti kuhusu jambo lo lote, Mungu pia atalifunuao hiilo kwenu.
As many, therefore, as [are] perfect — let us think this, and if [in] anything ye think otherwise, this also shall God reveal to you,
16 Hata hivyo, hatua ifikia na tuenende katika mtindo huo.
but to what we have come — by the same rule walk, the same thing think;
17 Ndugu zangu, niigeni mimi. Waangalieni kwa makini wale wanaoenenda kwa mfano ulio wa jinsi yetu.
become followers together of me, brethren, and observe those thus walking, according as ye have us — a pattern;
18 Wengi wanaoishi niwale ambao mara nyingi nimewaambieni, na sasa nawaambia kwa machozi -wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.
for many walk of whom many times I told you — and now also weeping tell — the enemies of the cross of the Christ!
19 Mwisho wao ni uharibifu. Kwa kuwa Mungu wao ni tumbo, na kiburi chao kiko katika aibu yao. Wanafikiria mambo ya kidunia.
whose end [is] destruction, whose god [is] the belly, and whose glory [is] in their shame, who the things on earth are minding.
20 Bali uraia wetu uko mbinguni, ambako tunamtarajia mwokozi wetu Yesu Kristo.
For our citizenship is in the heavens, whence also a Saviour we await — the Lord Jesus Christ —
21 Atabadilisha miili yetu dhaifu kuwa kama mwili wake wa utukufu; kwa uweza ule ule unaomwezesha kuvidhibiti vitu vyote.
who shall transform the body of our humiliation to its becoming conformed to the body of his glory, according to the working of his power, even to subject to himself the all things.