< Hesabu 36 >

1 Kisha wale viongozi wa nyumba za mababa wa ukoo wa Gileadi mwana wa Machiri (ambaye alikuwa mwana wa Manase), ambao walikuwa wa ukoo wa uzao wa Yusufu, walikuja wakasema mbele za Musa na mbele za vionigozi wa familia za mababa wa watu wa Israeli.
那時若瑟後裔的家族中,有默納協的子孫,瑪基爾的兒子基肋阿得子孫的家族首領,來到梅瑟和叵子民各家族的首領前說:
2 Wakasema, “BWANA alikuamuru, wewe bwana wetu, kutupa mgawo wa ardhi kwa kura kwa wana wa Israeli. Uliamuriwa na BWANA kutoa mgawo wa Zerofehadi kaka yetu kwa binti zake.
「上主吩咐我主,以抽籤來分給以色列子民土地為產業,我主又領了木的保,將我們兄弟責羅斐哈得的產業,分給他的女兒們。
3 Lakini hawa binti wameolewa na wanaume toka kabila zingine za wana wa Israeli, basi mgawo wao wa ardhi utaondolewa kutoka kwenye mgawo wa mababa zao. Utaongezwa kwenye mgawo wa makabila ambayo wao wanaungana nao. Kwa sababu hiyo, Utaondolewa kwenye mgawo uliopangwa kwenye urithi wetu.
現在,如果她們嫁給了以色列子民另一支派的人,她們的產業就脫離了我們祖先的產業,而加在所嫁給的那一支派的產業上:這樣,我們抽籤分得的產業就減少了。
4 Kwa sababu hiyo, wakati wa mwaka wa yubilee ya wana wa Israeli utakapofika, mgawo wao utaunganishwa na kabila ile waliyoungana nao. Kwa sababu hii mgawo wao utaondolewa kwenye mgawo wa mababa zetu.”
甚至一到以色列子民的喜年,她們的產業仍舊加在所嫁的那一支派的產業內,我們祖先支派的產業就減少了她們那一份」。
5 Basi Musa akawapa amri wana wa Israeli, kwa neno la BWANA. Akasema, “Kile wanachosema watu wa kabila la Yusufu kiko sahihi.
梅瑟依上主的指示訓令以色列子民說:「若瑟子孫支派說的有理。
6 Hiki ndicho BWANA anaagiza kuhusu mabinti wa Zelofehadi. Anasema, 'Acha waolewa na wale ambao wao wanaofikri ni vizuri zaidi, lakini lazima waolewe ndani ya kabila ya baba yao.'
上主對於責羅斐哈得的女兒們這樣這樣吩咐說:她們可任意嫁給自己所喜愛的人,但只應嫁給屬於自己祖先支派的人。
7 Hakuna mgawo wa watu utakaobadilika kutoka kabila moja kwenda jingine. Kila mtu wa Israeli ataendelea na mgawo wa kabila ya baba y ake.
以色列子民的產業不可由一支派轉移至另一支派,因為以色列子民每人應固守自己祖先支派的產業。
8 Kila mwanamke wa watu wa Israeli aliye na mgao kwenye kabila lake lazima aolewe na mtu wa ukoo unaotoka kwenye kabila la baba yake. Hii itafanyika hivyo ili kila mtu wa wana wa Israeli aweze kuwa na urithi kutoka kwa mababa zake.
以色列子民支派中,凡繼承產業的子女,應嫁給她祖先支派的人為妻,好使每個以色列子民能固守祖先的產業。
9 Hakuna mgawo utakaobadilika kutoka kabila nyingine kwenda kabila nyingine. Kila mtu wa kabila za watu wa Israeli atalinda urithi wake.”
這樣產業就不會由一支派轉移至另一支派,因為以色列子民各支派應固守自己的產業」。
10 Kwa hiyo wale binti wa Zelofehadi walifanya kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Mahila, Tiriza, Hogila, Milika, na Noha, binti za
上主怎樣吩咐了梅瑟,責羅斐哈得的女兒們就怎樣做了。
11 Zelofehadi, waliolewa na wana wa uzao wa Manase.
責羅斐哈得的女兒:瑪赫拉、提爾匝、曷米革拉、米耳加和諾阿,嫁給了自己叔伯的兒子們,
12 Waliolewa katika koo za uzao wa Manase mwana wa Yusufu. Kwa sababu hii, urithi wao ulibaki kwenye kabila la ukoo ambalo baba yao alikuwa anatoka.
即嫁給了若瑟的兒子默納協子孫家族的人:如此她們的產業仍留在她們祖先家族的支派內。
13 Hizi ndizo amri na maagizo ambayo BWANAaliyatoa kupitia Musa kwa wana wa Israeli katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.
這是上主在耶利哥對面,約旦河邊,摩阿布曠野內,藉梅瑟向以色列子民所頒佈的誡命和規則。

< Hesabu 36 >