< Hesabu 34 >

1 BWANA akanena na Musa akasema,
Bwana akamwambia Mose,
2 “Waamuru watu wa Israeli na uwaambie, 'Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani, nchi ambayo itakuwa mali yenu, nchi ya Kanaani na mipaka yake, mpaka wenu wa kusini utaendelea kutoka nyika ya Sini hadi mpaka wa Edomu.
“Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:
3 Mwisho wa mpaka wa kusini utakuwa mwisho wa bahari ya chumvi kuelekea mashariki.
“‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi,
4 Mpaka wenu utageukia kusini kutoka mlima kuelekea Akrabimu na kupitia nyika ya Sini. na kutokea huko utaelelkea kusini mwa Kadeshi Barinea na kuelekea Hazari Adari mpaka Azimoni.
katiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni,
5 Kutoka huko, mpaka utageuka kutoka Azimoni kuelekea kijito cha Misri na kukifuata mpaka baharini.
mahali ambapo utapinda, na kuunganika na Kijito cha Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati.
6 Mpaka wa Magharibi utakuwa pwani ya bahari kuu. Huu ndio utakuwa mpaka wenuwa Magharibi.
“‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.
7 Mpaka wenu wa kaskazini utaanzia kwenye bahari kuu hadi Mlima Hori,
“‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori,
8 kisha kutoka Mlima Hori hadi Lebo Hamathi, kisha Zedadi.
na kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi,
9 Mpaka utaendelea hadi Zifroni na kuishia Hazari Enani. Huu ndio utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.
kuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hasar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.
10 Kisha mtaweka alama za mpaka wenu wa mashariki ambao utaanzia Hazari Enani kuelekea kusini Shefamu.
“‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hasar-Enani hadi Shefamu.
11 Kisha mpaka wa kusini utaendelea kutoka Shefamu hadi Ribla, upande wa masharikia mwa Aini. Mpaka utaedelea upande huo wa mashariki hadi upande wa mashariki wa bahari ya Kinerethi.
Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.
12 Kisha mpaka utaendelea kuelekea kusini hadi mto Yorodani na hadi bahari ya chumvi. Hii ndiyo itakuwa nchi yenu, kwa kuifuata mipaka yake yote inayozunguka.'”
Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi. “‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’”
13 Kisha Musa akawaamuru watu wa Israeli akasema, “Hii ndiyo nchi ambayo mtaipokes kwa kura, ambayo BWANA ameamuru kuwapa wale makabila tisa na nusu.
Mose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi. Bwana ameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu,
14 Kabila ya uzao wa Reubeni, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na uzao wa kabila la Gadi, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na nusu ya Manase wamepata ardhi yao.
kwa sababu jamaa ya kabila la Reubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase wamekwishapokea urithi wao.
15 Wale makabila mawili na nusu wameshapata mgawo wao ng'ambo ya mto Yorodani upande wa mashariki, kuelekea kule linakotokea jua.”
Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ngʼambo ya Yeriko, kuelekea mawio ya jua.”
16 BWANA akanena na Musa akasema,
Bwana akamwambia Mose,
17 “Haya ndiyo majinaya watu watakaoigawa ardhi kwa ajili ya urithi wao: Eliazari kuhani na Joshua mwana wa Nuni.
“Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni.
18 Mtachagua kiongozi mmoja toka kila kabila ili kuigawa ardhi kwa koo zao.
Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi.
19 Haya ndiyo majina ya wanaume: Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
Haya ndiyo majina yao: “Kalebu mwana wa Yefune, kutoka kabila la Yuda;
20 Kutoka kwenye kabila la uzao wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
Shemueli mwana wa Amihudi, kutoka kabila la Simeoni;
21 Kutoka kabila la Benjamini, Elidadi mwana wa Kisloni.
Elidadi mwana wa Kisloni, kutoka kabila la Benyamini;
22 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Dani, Buki mwana wa Jogili.
Buki mwana wa Yogli, kiongozi kutoka kabila la Dani;
23 Kiongozi kutoka uzao wa Yusufu, kwenye kabila la Manase, Hannieli mwana wa Efodi.
Hanieli mwana wa Efodi, kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;
24 Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Efraimu, Kemueli mwana wa Shiftani.
Kemueli mwana wa Shiftani, kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;
25 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Zabuloni, Elizafani mwana wa Parinaki.
Elisafani mwana wa Parnaki, kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;
26 Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Isakari, Palitieli mwana wa Azzani.
Paltieli mwana wa Azani, kiongozi kutoka kabila la Isakari;
27 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Asheri, Ahihudi mwana wa Shelomi.
Ahihudi mwana wa Shelomi, kiongozi kutoka kabila la Asheri;
28 Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Naftali, Pedaheli mwana wa Amihudi.”
Pedaheli mwana wa Amihudi, kiongozi kutoka kabila la Naftali.”
29 BWANA aliwaamuru wanaume hawa kuigawa nchi ya Kanaani na kuwapa kila kabla sehemu yao.
Hawa ndio watu ambao Bwana aliamuru wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

< Hesabu 34 >