< Hesabu 31 >

1 BWANA alinena na Musa na kumwambia,
Bwana akamwambia Mose,
2 “Uwalipizie kisasi Wamidiani kwa kile walichowafanya Waisraeli. Baada ya kufanya hivyo utakufa na kukusanyika na watu wako.”
“Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.”
3 Kwa hiyo Musa akawaambia watu. Akasema, “andaeni baadhi ya majeshi yenu kwa ajili ya vita ili kwamba wakawapige Wamidiani na kubeba kiapo cha BWANA.
Kwa hiyo Mose akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi cha Bwana.
4 Kwa kila kabila la Israeli watatuma askari elfu moja kwa ajili ya vita.”
Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.”
5 Kwa hiyo kati ya wanaume maelfu elfu wa Israeli, wanaume elfu moja walitolewa kwa ajili ya vita, jumla ya wanaume elfu kumi na mbili.
Kwa hiyo waliandaliwa wanaume 12,000 kwa vita, wanaume 1,000 kutoka kila kabila, walitolewa kutoka koo za Israeli.
6 Kisha Musa akawatuma kwenda vitani, elfu moja toka kila kabila pamoja na Finehasi mwana wa Eliazari kuhanai, wakiwa na vitu kutoka mahali patakatifu wakiwa na matarumbeta kwa ajili ya ishara za sauti.
Mose aliwatuma vitani, watu 1,000 kutoka kila kabila, pamoja na Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, ambaye alichukua vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kuashiria.
7 Wakapigana na Midiani, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Wakamwua kila mwanaume.
Walipigana dhidi ya Wamidiani, kama Bwana alivyomwagiza Mose, nao waliua kila mwanaume.
8 Wakawaua wafalme wa Midiani pamoja na wengine waliowaua ni: Evi, Rekimu, Zuri, Huri, na Reba, hawa walaikuwa ndio waflme watano wa Midiani. pia walimwua Balaamu mwana wa Beori, kwa upanga.
Miongoni mwa watu waliouawa walikuwepo wafalme watano wa Midiani, nao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vilevile walimuua Balaamu mwana wa Beori kwa upanga.
9 Jeshi la Israeli likawachukua mateka wanawake wa Midiani, watoto wao, mifugo yao yote, kondoo wao na bidhaa zao zote. walivichukua hivi kama mateka.
Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ngʼombe, kondoo na mali zao kama nyara.
10 Waliichoma moto miji yao yote walimoishi na kambi zao zote.
Walichoma moto miji yote ambayo Wamidiani walikuwa wanaishi, pamoja na kambi zao zote.
11 Walichukua vitu vyote na wafungwa, watu na wanyama.
Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama,
12 Wakawaleta mateka, nyara, na wakakamata vitu wakavileta kwa Musa, na Eliazari kuhani, na kwa jamii ya watu wa Israeli. Wakavileta hivi vitu kambini katika uwanda wa Moabu, kule Yorodani karibu na Yeriko.
nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Mose na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.
13 Musa, Eliazari kuhani, pamoja na viongozi wa watu wakaenda kukutana nao nje ya kambi.
Mose, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi.
14 Lakini Musa alikuwa na hasira dhidi ya viongozi wa jeshi, Wale majemedari wa maelfu na maakida wa mamia, waliotoka kupigana.
Mose aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.
15 Musa akawaambia, “Je, mmeawaacha wanawake wote kuishi?
Mose akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?”
16 Tazama, wanawake hawa ndio waliosababisha watu wa Israeli, kwa kupitia ushauri wa Balaamu, kufanya dhambi dhidi ya BWANA huko Peori, wakati ile tauni iliposambaa kwa watu wa Mungu.
“Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasi Bwana kwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu wa Bwana.
17 Sasa basi, ueni kila mwanaume kuanzia wadogo, na ueni kila mwanamke aliyelala na mwanamume.
Sasa waue wavulana wote. Pia muue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa,
18 Lakini chukueni wale mabinti wadogo ambao hawajalala na mwanamume.
lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.
19 Mtaweka kambi nje na kambi za Israeli kwa muda wa siku saba. Ninyi wote ambao mmeua watu au ambao mmegusa maiti yeyote mtajitakasa wenyewe katika siku ya tatu na katika siku ya saba - ninyi na mateka wenu.
“Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.
20 Na mtayatakasa mavazi yenu yote, na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi za wanyama, na manyoya ya mbuzi, na kila kitu kilichotengenezwa kwa mbao.”
Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”
21 Eliazarai kuahani akawaambia wale wanajeshi waliokuwa wameenda vitani, “Hii ni amri ya sheria ambayo BWANA alimpa Musa:
Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari waliokuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayo Bwana alimpa Mose:
22 Zile dhahabu, fedha, vyuma, bati, risasi,
Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi,
23 na kila kitu knaweza kuhhimili moto, mtakiweka katka moto, navyo vitakuwa safi. Nakisha mtavitakasa vitu hivyo na maji ya farakano. Na vitu vyote ambavyo haviwezi kupita katika moto, mtavitakasa kwa maji hayo.
na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.
24 Na mtazifua nguao zenu katika siku ya saba, ndipo mtakapokuwa safi. Baada ya hapo mnaweza kurudi kwenye kambi za Israeli.”
Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”
25 Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
Bwana akamwambia Mose,
26 “Vihesabu vitu vyote vilivyochukuliwa nyara, wote watu na wanyama. Wewe, Eliazari kuhani, na viongozi wa watu kufuata koo
“Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa.
27 watavigawa hivi vitu katika mkundi mawili. Mvigawe kwa wanajeshi walioenda kupigana na kwa watu wote.
Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya.
28 Kisha toza kodi ambayo itatolewa kwangu kutoka kwa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani. Hii kodi itakuwa moja kati ya mia tano, katika watu, ng'ombe, punda, kondoo, au mbuzi.
Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili ya Bwana kitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo au mbuzi.
29 Uichukue hii kodi kutoka katika nusu yao na umpe Eliazari kuhani kwa ajili ya sadaka itakayotolewa kwangu.
Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu ya Bwana.
30 Pia kutoka katika nusu ya watu wa Israeli, utachukua moja kati ya hamsini -kutoka vitu, ng'ombe, punda, na mbuzi. Uvitoe hivi kwa Walawi wanaotumika katika masikani yangu.”
Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani ya Bwana.”
31 Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa.
Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Mose.
32 Sasa zile nyara zilizokuwa zimebaki ambazo wanajeshi walikuwa wameteka zilikuwa kondoo 675, 000,
Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000,
33 maksai elfu sabini na mbili,
ngʼombe 72,000,
34 punda elfu sitini na moja,
punda 61,000,
35 na wanawake elfu thelathini na mbili ambao walikuwa hawajalala na mwanamume yeyote.
na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.
36 Ile hesabu ya nusu iliyokuwa imetunzwa kwa ajili ya wanajeshi ilikuwa kondoo 337, 000. Ile sehemu ya
Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa: Kondoo 337,500
37 BWANA ya kondoo ilikuwa kondoo 675.
ambayo ushuru kwa ajili ya Bwana ilikuwa kondoo 675;
38 Maksai walikuwa elfu thelathini na sita ambayo kodi ya BWANA ilikuwa sabini na mbili.
ngʼombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa ngʼombe 72;
39 Punda walikuwa 30, 500 ambao sehemu ya BWANA ilikuwa sitini na moja.
punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa punda 61;
40 Watu walikuwa wanawake elfu kumi na sita ambao kodi ya BWANA ilikuwa thelathini na mbili.
Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili ya Bwana ulikuwa watu 32.
41 Musa aliichukua ile kodi ambayo ilitakiwa kuwekwa sadaka kwa BWANA. Akampatia Eliazari kuhani, kama BWANA alivyomwamuru Musa.
Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu ya Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
42 Ile nusu ya watu wa Israeli ambayo Musa alikuwa ameichukua toka kwa wanawjeshi waliokuwa wameenda vitani -
Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani,
43 ile nusu y a watu ilikuwa kondoo 337, 500,
nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500,
44 maksai elfu thelathini na sita,
ngʼombe 36,000,
45 punda 30, 500,
punda 30,500,
46 na wanawake elfu kumi na sita.
na wanadamu 16,000.
47 Kutoka kwenye nusu ya watu wa Israeli, Musa alichukua moja katika hamsini, wote watu na wanyama. Aliwapa Walawi ambao huitumikia masikani ya BWANA, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.
Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kama Bwana alivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani ya Bwana.
48 Kisha wale maakida wa jeshi, makamanda wa elfu na makapteni wa mamia, wakaja kwa Musa.
Kisha maafisa waliokuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Mose
49 Wakamwambia, “watumishi wako wamewahesabu wanajeshi ambao wako chini yetu, hakuna hata mmoja wao aliyekosa.
na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana.
50 Tumemletea BWANA sadaka, ambayo kila mmoja amepata, vitu vya dhahabu, metali, timbi, pete za mhuri, vipini na vikuku, ili kujifanyia upatanisho kwa BWANA.”
Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwa Bwana vyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele za Bwana.”
51 Musa na Eliazari kuhani akapokea kutoka kwao dhahabu na vitu vyote vilivyotengenezwa kwa ufundi.
Mose na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakshiwa.
52 Vitu vyote vya sadaka ya dhahabu ambavyo walimpa BWANA- sadaka toka kwa makamanda wa maelfu na kutoka kwa makepteni wa mamia - vilikuwa na uzito wa shekeli 16, 750.
Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimletea Bwana kama zawadi ilikuwa shekeli 16,750
53 Kila mwanajeshi alikuwa ameteka nyara ya kila mtu kwa ajili yake.
Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi.
54 Musa na Eliazari kuhani wakazichukuazile dhahabu toka kwa makamanda wa maelfu na makepteni wa mamia. Wakavipeleka kwenye hema ya kukutania kama ukumbusho wa watu wa Israeli kwa BWANA.
Mose na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana.

< Hesabu 31 >