< Hesabu 30 >

1 Musa aliwambia viongizi wote wa makabila ya watu wa Israeli. “Hiki ndicho ambacho BWANA ameamuru.
וַיְדַבֵּר מֹשֶׁה אֶל־רָאשֵׁי הַמַּטּוֹת לִבְנֵי יִשְׂרָאֵל לֵאמֹר זֶה הַדָּבָר אֲשֶׁר צִוָּה יְהֹוָֽה׃
2 Mtu yeyote atakayefanya nadhiri kwa BWANA, au kuapa kwa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asivunje neno lake. Atafanya sawa na ahadi yake imtokayo kinywani mwake.
אִישׁ כִּֽי־יִדֹּר נֶדֶר לַֽיהֹוָה אֽוֹ־הִשָּׁבַע שְׁבֻעָה לֶאְסֹר אִסָּר עַל־נַפְשׁוֹ לֹא יַחֵל דְּבָרוֹ כְּכׇל־הַיֹּצֵא מִפִּיו יַעֲשֶֽׂה׃
3 Na kama binti anaishi katika nyumba ya baba yake kwa atafanya nadhiri kwa BWANA na kuifunga nafsi yake kwa kiapo,
וְאִשָּׁה כִּֽי־תִדֹּר נֶדֶר לַיהֹוָה וְאָסְרָה אִסָּר בְּבֵית אָבִיהָ בִּנְעֻרֶֽיהָ׃
4 na kama baba yake atasikia hiyo nadhirina ahadi ambayo ametumia kuifunga nafsi yake, naye asiseme kitu kumzuia, ndipo nadhiri zake zitakuwa na nguvu. Kila ahadi ambayo ameitumia kuifunga nafsi yake itabaki kuwa na nguvu.
וְשָׁמַע אָבִיהָ אֶת־נִדְרָהּ וֶֽאֱסָרָהּ אֲשֶׁר אָֽסְרָה עַל־נַפְשָׁהּ וְהֶחֱרִישׁ לָהּ אָבִיהָ וְקָמוּ כׇּל־נְדָרֶיהָ וְכׇל־אִסָּר אֲשֶׁר־אָסְרָה עַל־נַפְשָׁהּ יָקֽוּם׃
5 Lakini kama baba yake atasikia nadhairi yake na ahadi zake, na kama hatasema chochote kwake, ndipo nadhiri zake zote na ahadi alizofanya zitakapokuwa na nguvu.
וְאִם־הֵנִיא אָבִיהָ אֹתָהּ בְּיוֹם שׇׁמְעוֹ כׇּל־נְדָרֶיהָ וֶֽאֱסָרֶיהָ אֲשֶׁר־אָסְרָה עַל־נַפְשָׁהּ לֹא יָקוּם וַֽיהֹוָה יִֽסְלַח־לָהּ כִּי־הֵנִיא אָבִיהָ אֹתָֽהּ׃
6 Hata hivyo, kama baba yake atasikia nadhri zake zote alizofanya na ahadi zake makini ambazo ametumia kufunga nafsi yake, na kama atazitengua ndani ya siku hiyo, ndipo hizo nadhiri hazitakuwa na nguvu. BWANA atamsamehe kwa kuwa baba yake amemzuia.
וְאִם־הָיוֹ תִֽהְיֶה לְאִישׁ וּנְדָרֶיהָ עָלֶיהָ אוֹ מִבְטָא שְׂפָתֶיהָ אֲשֶׁר אָסְרָה עַל־נַפְשָֽׁהּ׃
7 Kama ataolewa angali katika hivyo viapo, au kama atafanya ahadi za bila kufikiri ambazo atajifunga nazo, hivyo vifungo vitakuwa na nguvu.
וְשָׁמַע אִישָׁהּ בְּיוֹם שׇׁמְעוֹ וְהֶחֱרִישׁ לָהּ וְקָמוּ נְדָרֶיהָ וֶֽאֱסָרֶהָ אֲשֶׁר־אָסְרָה עַל־נַפְשָׁהּ יָקֻֽמוּ׃
8 Lakini kama mume wake atamzuia siku hiyo hiyo ambayo atamskia akiapa, basi atabatailisha hicho kiapo alichokifanya, maneno yake ya midomo yaka ya bila kufikiri ambayo kwayo amefunga nafsi yake. BWANA atamfungua.
וְאִם בְּיוֹם שְׁמֹעַ אִישָׁהּ יָנִיא אוֹתָהּ וְהֵפֵר אֶת־נִדְרָהּ אֲשֶׁר עָלֶיהָ וְאֵת מִבְטָא שְׂפָתֶיהָ אֲשֶׁר אָסְרָה עַל־נַפְשָׁהּ וַיהֹוָה יִֽסְלַֽח־לָֽהּ׃
9 Lakini kwa mjane au kwa mwanamke aliyetalikiwa, kila kitu amabacho atakisema kufunga nafsi yake lazima kitabaki na nguvu kinyume na yeye.
וְנֵדֶר אַלְמָנָה וּגְרוּשָׁה כֹּל אֲשֶׁר־אָסְרָה עַל־נַפְשָׁהּ יָקוּם עָלֶֽיהָ׃
10 Na kama mwanamke atafanya kiapo katika nyumba ya mume wake au akijifunga mwenyewe kwa kufanaya kiapo,
וְאִם־בֵּית אִישָׁהּ נָדָרָה אֽוֹ־אָסְרָה אִסָּר עַל־נַפְשָׁהּ בִּשְׁבֻעָֽה׃
11 na mume wake akakisikia hicho kiapo na hakusema chochote kwake na hakumpinga, basi viapo vyake vitasimama na vifungo alivyovifanaya vitabaki na nguvu.
וְשָׁמַע אִישָׁהּ וְהֶחֱרִשׁ לָהּ לֹא הֵנִיא אֹתָהּ וְקָמוּ כׇּל־נְדָרֶיהָ וְכׇל־אִסָּר אֲשֶׁר־אָסְרָה עַל־נַפְשָׁהּ יָקֽוּם׃
12 Lakini kama mume wake atamzuilia katika siku hiyo ambayo atavisikia, basi chochote ambacho kitatoka katika kinywa chake kuhusu viapo vyake au ahadi zake havitabaki kuwa na nguvu. Mume wake atkuwa amevibatilisha. BWANA atamfungua.
וְאִם־הָפֵר יָפֵר אֹתָם ׀ אִישָׁהּ בְּיוֹם שׇׁמְעוֹ כׇּל־מוֹצָא שְׂפָתֶיהָ לִנְדָרֶיהָ וּלְאִסַּר נַפְשָׁהּ לֹא יָקוּם אִישָׁהּ הֲפֵרָם וַיהֹוָה יִֽסְלַֽח־לָֽהּ׃
13 Kila kiapo ambacho mwanamke anakifanya ambacho kinamfunga ili kujikana kianaweza kuthibitika au kubatilishwa na mume wake.
כׇּל־נֵדֶר וְכׇל־שְׁבֻעַת אִסָּר לְעַנֹּת נָפֶשׁ אִישָׁהּ יְקִימֶנּוּ וְאִישָׁהּ יְפֵרֶֽנּוּ׃
14 Lakini kama hatasema chochote kwake siku baada ya siku, basi atathibitisha nadhiri zake na ahadi zake zinazomfunga ambazo amefanya. Atakuwa amezithibitisha kwa sababu hakusema chochote wakati alipozisikia.
וְאִם־הַחֲרֵשׁ יַחֲרִישׁ לָהּ אִישָׁהּ מִיּוֹם אֶל־יוֹם וְהֵקִים אֶת־כׇּל־נְדָרֶיהָ אוֹ אֶת־כׇּל־אֱסָרֶיהָ אֲשֶׁר עָלֶיהָ הֵקִים אֹתָם כִּי־הֶחֱרִשׁ לָהּ בְּיוֹם שׇׁמְעֽוֹ׃
15 Na kama mume wake atajariibu kubatilisha kiapo cha mke wake baada ya kuzisikia kwa muda mrefu, basi ataajibika kwa dhambi zake.”
וְאִם־הָפֵר יָפֵר אֹתָם אַחֲרֵי שׇׁמְעוֹ וְנָשָׂא אֶת־עֲוֺנָֽהּ׃
16 Hizi ndizo amri ambazo Mungu alimwamuru Musa kuzitangaza - amri ambazo ziko kati ya mume na mke wake na kati ya baba na binti yake wakati akiwa katika ujana wake katika familia ya baba yake.
אֵלֶּה הַֽחֻקִּים אֲשֶׁר צִוָּה יְהֹוָה אֶת־מֹשֶׁה בֵּין אִישׁ לְאִשְׁתּוֹ בֵּֽין־אָב לְבִתּוֹ בִּנְעֻרֶיהָ בֵּית אָבִֽיהָ׃

< Hesabu 30 >