< Hesabu 3 >

1 Sasa hii ndiyo historia ya uzao wa Haruni na Musa wakati BWANA aliposema na Musa kwenye mlima Sinai.
Hii ni hesabu ya jamaa ya Aroni na Mose kwa wakati ambao Bwana alizungumza na Mose katika Mlima Sinai.
2 Majina ya watoto wa Haruni walikuwa Nadabu ambaye ndiyo mtoto wa kwanza, na Abihu, na Eliezeri, na Ithamari.
Majina ya wana wa Aroni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari.
3 Haya ndiyo majina ya wana wa Haruni, makuhani waliokuwa wamepakwa mafuta na kuwekwa wakfu kutumika kama makuhani.
Hayo yalikuwa majina ya wana wa Aroni, makuhani wapakwa mafuta, waliokuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani.
4 Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya BWANA walipomtolea moto usiokubalika walipokuwa katika nyika ya Sinai. Nadabu na Abihu hawakuwa na watoto, kwa hiyo Eliazari na Ithamari walitumika kama makuhani pamoja na baba yao.
Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Aroni baba yao.
5 BWANA alinena na Musa, akamwambia,
Bwana akamwambia Mose,
6 “Walete kabila ya Lawi na uwaweke kwa Haruni kuhani ili wamsaidie
“Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie.
7 Nao lazima wafanye majukumu badala ya Haruni na jumuiya yote mbele ya hema ya kukutania. Lazima watumike hemani.
Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani.
8 Watayatunza mapambo ya hema ya kukutania, na watawatumikia makabila ya Israel kwa huduma ya hemani.
Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.
9 Uwaweke Walawi kwa Haruni na watoto wake. Nimewatoa kikamilifu ili wamsaidie kuwatumikia watu wa Israel.
Wakabidhi Walawi kwa Aroni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kwake kabisa.
10 Umchague Haruni na watoto wake kuwa makuhani, lakini mgeni yeyote atakayekaribia lazima auawe.”
Waweke Aroni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine yeyote atakayesogea mahali patakatifu ni lazima auawe.”
11 BWANA alinena na Musa. akamwambia,
Bwana akamwambia Mose,
12 “Tazama, nimewachagua Walawi katika watu wa Israel. Nimefanya hivyo badala ya kuchukua mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wana wa Israel. Hawa Walawi ni wangu.
“Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu,
13 Na hata wazaliwa wa kwanza ni mali yangu. Katika siku ambyo niliwavamia wazaliwa wote wa kwanza wa nchi ya Misri, Niliwatenga wazaliwa wa kwanza wa Israeli kwa ajili yangu, watu na wanyama pia. Ni mali yangu. Mimi ndimi BWANA.”
kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana.”
14 BWANA alinena na Musa katika nyika ya Sinai. Akasema,
Bwana akamwambia Mose katika Jangwa la Sinai,
15 “Wahesabu uzao wa Lawi katika kila familia, katika nyumba za koo zao. Hesabu kila mume kuanzia mwezi mmoja au zaidi.”
“Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”
16 Musa aliwahesabu, kufuata maelekezo ya BWANA, kama alivyoamriwa kufanya.
Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Bwana.
17 Majina ya watoto waLawi yalikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.
Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
18 Ukoo uliotokana na watoto wa Gerishoni walikuwa ni Libni na Shimei.
Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni: Libni na Shimei.
19 Ukoo uliotokana na watoto Kohathi walikuwa ni Amramu na, Izihari, Hebroni, na Uzieli.
Koo za Wakohathi zilikuwa ni: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
20 Ukoo uliotokana na watoto wa Merari walikuwa ni Mahili na Mushi. Hizi ndizo koo za Walawi, zilizoorodheshwa ukoo kwa ukoo.
Koo za Wamerari zilikuwa ni: Mahli na Mushi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.
21 Koo za Walibini na Washimei zilitokana na Wagerishoni. Hizi ndizo koo za Wagerishoni.
Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagershoni.
22 Wanaume wote wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi walihesabiwa na kufikia idadi ya 7, 500.
Idadi ya waume wote waliokuwa na mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 7,500.
23 Koo za Wagerishoni watapanga upande wa magharibi wa hema.
Ukoo wa Wagershoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani.
24 Eliasafu mwana wa Laeli ataongoza koo za uzao wa Wagerishoni.
Kiongozi wa jamaa za Wagershoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli.
25 Familia ya Gerishoni watalilinda hema la kukutania pamoja na hiyo masikani. Watalilinda hema, kifuniko chake, na lile pazia la lango la hema ya kukutania.
Katika Hema la Kukutania, Wagershoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania,
26 Wataulinda ua, lile pazia la kwenye lango—ua unaozunguka mahali patakatifu na madhabahu. Watazilinda kamba za hema ya kukutania na vyote vilivyomo.
mapazia ya ua, pazia katika ingilio la ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.
27 Koo zifuatazo zinatokana na Kohathi: ukoo wa Waamrami, ukoo wa Waizihari ukoo wa Wahebroni, na ukoo wa Wauzieli. Koo hizi zinatokana na Wakohathi.
Kwa Kohathi kulikuwepo koo za Waamramu, Waishari, Wahebroni na Wauzieli; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wakohathi.
28 Wanaume 8, 600 wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi walihesabiwa ili kulinda vitu vya BWANA.
Hesabu ya waume wote wenye mwezi mmoja au zaidi ilikuwa watu 8,600. Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu.
29 Familia ya uzao wa Kohathi watapanga upande wa kusini wa Hema.
Koo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani.
30 Elizafani mwana wa Uzieli ndiye atakayeongoza ukoo wa Wakohathi.
Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli.
31 Watalilinda sanduku, meza, vikalishio vya taa, madhabahu, vitu vitakatifu ambvyo hutumika katika huduma yao, pazia, na kazi zote zinazoambatana na hema.
Waliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake.
32 Eliazari mwana wa Haruni kuhani atawaongoza wanaume wanaowaongoza Walawi. Atawasimamia wanaume wanaongoza eneo takatifu.
Kiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Aroni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.
33 Koo mbili zimetoka kwa Merari: Ukoo wa Mahili na ukoo wa Mushi. Koo hizi zimetokana na Merari,
Kwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari.
34 Wanaume 6, 200 wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi walihesabiwa.
Hesabu ya waume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 6,200.
35 Zurieli mwana wa Abihaili ataongoza ukoo wa Merari. Hawa watapanga upande wa kaskazini mwa hema.
Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.
36 Uzao wa Merari utatunza mbao za hema, mataruma, nguzo, makalishio, viifaa vya ujenzi na vitu vyote vinavyohusika,
Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake,
37 na nguzo za ua zinazozunguka hema, makalishio, vigingi na kamba zake.
na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.
38 Musa na Haruni na watoto wake watapanga upande wa mashariki wa masikani, mbele ya hema ya kukutania kuelekea mawio ya jua. Wao wataajibika na majukumu ya mahali patakatifu na majukumu ya wana wa Israeli. Mgeni atakayekaribia mahali patakatifu auawe.
Mose, na Aroni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea mawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.
39 Musa na Haruni wakawahesabu wanaume wote wa ukoo wa Walawi walikuwa na umri wa mwezi mmoja na zaidi, kama vile BWANA alivyokuwa ameagiza. Walihesabu wanaume ishirini na mbili elfu.
Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Mose na Aroni kwa amri ya Bwana, kufuatana na koo, pamoja na kila mume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa 22,000.
40 BWANA alisema na Musa, “Wahesabu wanaume wote ambo ni wazaliwa wa kwanza wa Israeli ambao wana umri wa mwezi mmoja na zaidi. Orodhesha majina yao.
Bwana akamwambia Mose, “Wahesabu wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wa Waisraeli wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi na uorodheshe majina yao.
41 Unitwalie walawi kwa ajili yangu badala ya wazaliwa wa kwanza wa Israeli, Mimi ndimi BWANA. Na utwae wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa uzao wa Israeli,”
Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimi Bwana.”
42 Musa akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli kama BWANA alivyomwagiza kufanya.
Hivyo Mose akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Waisraeli, kama Bwana alivyomwamuru.
43 Aliwahesabu wazaliwa wote wa kwanza kwa mjina, wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi. Alihesabu wanaume 22, 273.
Jumla ya hesabu ya wazaliwa wa kwanza waume wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walioorodheshwa kwa majina, walikuwa 22,273.
44 Tena BWANA alinena na Musa. Akasema,
Bwana akamwambia Mose,
45 “Watwae Walawi badala ya wazaliwa wote wa kwanza wa wana wa Israeli. Na utwae wanyama wa Walawi badala ya wanyama wa Waisreli wengine. Walawi ni mali yangu. Mimi ndimi BWANA.
“Watwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya mifugo yao. Walawi watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana.
46 Unikusanyie shekeli tano za wokovu kwa kila hao 273 za hao wazaliwa wa kwanza wa Israeli za hao wanaozidi idadi ya Walawi.
Ili kukomboa wazao wa kwanza 273 wa Waisraeli ambao wamezidi hesabu ya Walawi,
47 Utazitumia hizo shekeli tano kwa kipimo cha mahali patakatifu. Shekeli moja ni sawa na gera ishirini.
kusanya shekeli tano kwa kila mmoja, kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.
48 Utawalipa hizo shekeli za wokovu kwa Haruni na wanawe.”
Mpe Aroni na wanawe hizo fedha kwa ajili ya ukombozi wa idadi ya Waisraeli waliozidi.”
49 Kwa hiyo Musa akakusanya shakeli za wokovu kutoka kwa wale waliozidi idadi ya wale waliookolewa na Walawi.
Kwa hiyo Mose akakusanya fedha za ukombozi kutoka kwa wale ambao hesabu yao ilizidi wale waliokombolewa na Walawi.
50 Musa akakusanya zile fedha kutoka kwa hao wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli. Alikusanya jumla ya shekeli 1, 365, zenye kipimo sawa na mahali patakatifu. Musa akamlipa Haruni na wanawe hizo shekeli za wokovu.
Kutokana na wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli alikusanya fedha yenye uzito wa shekeli 1,365 kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu.
51 Musa akafanya kila kitu alichoagizwa na neno la BWANA kama BWANA alivyomwagiza.
Mose akampa Aroni na wanawe ile fedha ya ukombozi, kama alivyoamriwa na neno la Bwana.

< Hesabu 3 >