< Hesabu 29 >
1 Katika siku ya kwanza, ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumwabudu BWANA. Katika siku hiyo hamtafanya kazi zenu za kila siku. Itakuwa siku ya kupiga matarumbeta.
2 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ya kufanya harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja na wanakondoo dume saba wa mwaka mmoja, kila mmoja mkamilifu.
3 Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa ajili ya huyo fahari, sehemu mbili za kumi kwa ajili ya huyo kondoo mume,
4 na sehemu ya kumi ya kila hao wanakondoo waume saba.
5 Na mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
6 Toeni hizo sadaka katika mwezi wa saba kama nyongeza ya sadaka mtakazotoa kila mwanzo wa kila mwezi: pamoja na sadaka maalumu za kuteketezwa na sadaka za unga. Hizi zitakuwa nyongeza za sadaka za kuteketezwa za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji. Utakapokuwa ukiendelea na sadaka hizi, utakuwa ukitii kile kilichoamriwa kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa BWANA.
7 Siku ya kumi ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumwabudu BWANA. Mtajinyeneyekeza na hamtafanya kazi.
8 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari mmoja mchanga ili kutoa harufu nzuri, kondoo mmoja mume, na wanakondoo saba waume wa mwaka mmoja. Wote wakamilifu.
9 Pamoja na sadaka hizo utatoa sadaka ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa ajili ya fahari, sehemu mbili za kumi za kondoo dume mmoja,
10 na sehemu ya kumi ya efa moja kwa kila mwanakondoo wale saba.
11 Mtatatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya upatanisho. Hii itakuwa sadaka ya nyongeza ya upatanisho, ya sadaka ya kila siku ya kuteketezwa, pamoja na sadaka za unga, na sadaka zake za vinywaji.
12 Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu lakumwabudu BWANA. Siku hiyo hamtafanya kazi za kila siku, na mtazitunza hizo sikukuu kwa muda wa siku saba kwa ajili ya BWANA.
13 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ilikutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa mafahari wachanga kumi na tatu, kondoo waume wawili, na wanakondoo waume kumi na nne wa mwaka mmoja. Wote wakamilifu.
14 Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembaba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa kila fahari katika hao kumi na tatu, sehemu mbili za kumi kwa kila hao kondoo dume wawili,
15 na sehemu ya kumi ya efa ya hao wanakondoo kumi na nne.
16 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa, sadaka yake ya unga, pamoja na sadaka za vinywaji.
17 Siku ya pili ya kusanyiko, mtatoa mafahari kumi na mbili, kondoo dume wawili na wanakondoo dume kumi na mbili wa umri wa mwaka mmoja, wote wakamilifu.
18 Pamoja nao mtatoa sadaka ya unga, na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, kondoo dume, na kwa ajili ya wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilvyoamriwa.
19 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kuwa nyongeza ya sadaka za kila siku, sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
20 Siku ya tatu ya kusanyiko, mtatoa sadaka mafahari kumi na moja, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa umri wa mwaka mmoja, wakamilifu.
21 Pamoja na hizo sadaka mtatoa sadaka ya unga na sdaka ya vinywaji kwa wale mafahari, kwa wale kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, utoe sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
22 Mtatoa sadaka beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya zile sadaka za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
23 Siku ya nne ya kusanyiko, mtatoa mafahari kumi, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
24 Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga na sdaka za vinywaji kwa wale mafahari, na kwa wale kondoo dume na kwa wale wanakodoo, mtatoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
25 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kuwa nyongeza ya sadaka za kuteketezwa za kila siku, sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji
26 Siku ya tano ya kusanyiko, mtatoa mafahari tisa, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
27 Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, kondoo dume, na wale wanakondoo, mkitoa sdaka nyingi kama ilivyoamriwa.
28 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kuteketezwa za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka za vinywaji.
29 Siku ya sita ya kusanyiko, mtatoa mafahari wanane, kondoo dume wawili, na wanakondoo kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
30 Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga nasadaka za vinywaji kwa wale mafahari, kondoo wa dume na wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
31 Mtatoa beberu kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kila siku za kuteketezwa, sadaka zadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
32 Siku ya saba ya kusanyiko, mtatoa mafahari saba, kondoo dume saba, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
33 Pamoja nao mtataengeneza sadaka ya unga na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, na kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
34 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya vinywaji.
35 Siku ya nane mtakuwa na kusanyiko lingine makini. Hamtafanya kazi zenu za kila siku.
36 Mtafanya sadaka za kuteketezwa, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari mmoja, kondoo mmoja dume, na wanakondoo saba dume wa umri wa mwaka mmoja, wakamilifu.
37 Mtatoa sadaka zake za unga na sadaka zake za vinywaji kwa ajili ya yule fahari, kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, mkifanya sadaka nyingi kadri ilivyoamriwa.
38 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
39 Hivi ndivyo utakavyotoa sadaka kwa BWANA katika sikukuu zenu za kila mwaka. Hivi vitakuwa nyongeza ya viapo vyenu na sadaka zenu za hiari. Mtavitoa hivi kama sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za unga, sadaka za vinywaji, na sadaka za amani.”
40 Musa aliwaambia wana wa Israeli kila kitu ambacho BWANA alikuwa amemwamuru kusema.