< Hesabu 28 >
1 BWANA akanena na Musa akamwambia,
2 “Waamuru wana wa Isrseli uwaambie, 'Mtanitolea sadaka kwa wakati uliopangwa, chakula cha sadaka yangu kilichotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa ajili yangu.
3 Pia uwaambie, 'Hii ni sadaka iliyotengenezwa kwa moto ambayo mtaitoa kwa BWANA- mwanakondoo dume wa mwaka mmoja asiyekuwa na waa, wawili kila siku kuwa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.
4 Mwanakodoo mmoja atatolewa sadaka asubuhi, na mwingine atatolewa sadaka jioni.
5 Mtatoa sadaka ya sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta yaliyokamuliwa.
6 Hii ni sadaka ya ya kuteketezwa ya kila siku iliyoamriwa mlima Sinai ili kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajili ya BWANA.
7 Pamoja na robo ya hini ya sadaka ya kinywaji kwa mmoja wa hao wanakondoo. Utaimimina mahali patakatifu hiyo sadaka ya kinywaji kwa BWANA.
8 Yule mwanakondoo mwingine utamtoa sadaka jioni pamoja na sadaka ya unga kama kama yule wa asubuhi alivyotolewa. Pia utatoa tena sadaka ya kinywaji pamoja naye, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA.
9 Katika siku ya Sabato utatoa wanakondoo dume wawili, wa umri wa mwaka mmoja kila mmoja wasiokuwa na dosari, na sehemu ya kumi mbili ya efa ya unga mwembamba kwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka ya kinywaji.
10 Hii itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa kila siku ya Sabato, kama nyongeza ya ile sadaka ya kila siku pamoja na ile sadaka ya kinywaji.
11 Kila mwanzo wa mwezi, mtatoa sadaka za kuteketezwa kwa BWANA. Utatoa sadaka ya fahari wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na wanakondoo dume saba wa umri wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari.
12 Pia mtatoa sehemu ya kumi tatu ya efa unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa kila fahari, na sehemu za kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa yule kondoo mume mmoja.
13 Pia mtatoa sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwanakondoo. Hii itakuwa sadaka ya kuteketezwa, ya kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajilI ya BWANA.
14 Sadaka ya kinywaji ya watu itakuwa nusu ya hini ya divai ya yule fahari, sehemu ya tatu ya hini ya kondoo dume, na robo ya hini ya mwanakondoo. Hii ndiyo itakuwa sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi kwa miezi yote ya mwaka.
15 Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA. Hii itakuwa nyongeza kwa ile sadaka ya kila siku pamoja na ile sadaka ya viinywaji.
16 Katika siku kumi na nne, ya mwezi wa kwanza itakuwa Pasaka ya BWANA.
17 Katika sku ya kumi na tano ya mwezi huu kutakuwa na sikukuu. Mtakuka mikate isiyo na chachu kwa siku saba.
18 Katika siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu la kumheshimu BWANA. Katika siku hiyo msifanye kazi zenu za kila siku
19 Hata hivyo, mtatoa sadaka iliyotengenezwa kwa moto, sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. Mtatoa sadaka ya fahari wawili, kondoo dume mmoja, na kondoo dume saba wa umri wa mwaka mmoja wakamilifu.
20 Pamoja na yule fahari, mtatoa sadaka sehemu za tatu efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, pamoja na yule kondoo mume sehemu za pili za kumi.
21 Kwa kila wale wanakondoo saba, mtatoa sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta,
22 na beberu mmoja kuwa sdaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
23 Mtotoa hivi vitu kama sadaka ya nyongeza katika ile sadaka ya kila siku inayotakiwa kila asubuhi.
24 Kama ilivyofafanuliwa hapa, mtatoa sadaka hizi kila siku, kwa zile siku saba za Pasaka, kile chakula cha sadaka kilichotengenezwa kwa moto kuwa harufu nzuri kwa BWANA. Hiki kitatolewa kuwa sadaka ya nyongeza ya ile sadaka ya kuteketezwa na pamoja na ile sadaka ya vinywaji.
25 Siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu ili kumheshimu BWANA, na katika siku hiyo msifanye zile kazi zenu zakila siku.
26 Pia katika siku ya malimbuko, mtakapokuwa mnatoa sadaka ya unga mpya katika sikukuu zenu za Majuma, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumheshimu BWANA, na katika siku hiyo msifanye kazi zenu za kila siku.
27 Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari wawili wachanga, kondoo mume mmoja, na wanakondoo saba waume wa mwaka mmoja.
28 Pamoja na hiyo mtatoa sadaka ya unga: unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa kila fahari na sehemu kumi mbili za yule kondoo mume.
29 Toeni sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa kila wale wanakondoo saba,
30 na beberu mmoja ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
31 Mtakapotoa hao wanyama wasio na dosari, pamoja na sadaka zake za vinywaji, hii itakuwa sadaka ya nyongeza katika zile sadaka za kila siku na pamoja na zile sadaka za unga.'”