< Hesabu 26 >
1 Ilitokea baada ya tauni ambayo BWANA alimwambia Musa na Eliazari mwana wa Haruni kuhani, Alisema,
2 Wahesabu watu wote wa Israeli, kuanzia miaka ishirini na zaidi, kwa jamaa ya familia zao wote ambao wanaweza kwenda kwenye vita kwa ajili ya Israeli.”
3 Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakawaambia katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko na kusema,
4 Wahesabuni watu, kuanzi umri wa miaka ishirini na zaidi kama BWANA alivyomwamuru Musa na watu wa Israeli walitoka katika nchi ya Misri.”
5 Reubeni ndiye aliyekuwa wa kwanza, Kutoka kwa mwana wake Hanoki ulitokea ukoo wa Wahanoki. Kutoka kwa Palu ulitokea ukoo wa Wapalu.
6 Kutoka Hezroni. ulitokea ukoo wa Wahezroni. Kutoka kwa Kami ulitokea ukoo wa Wakami.
7 Hizi ndizo zilikuwa koo za uzao wa Reubeni, ambzo idadi yao ilikuwa wanaume 43, 730.
8 Eliabu alikuwa mwana wa Palu.
9 Wana wa Eliabu walikuwa ni Nemueli, Dathani. na Abiramu. Hawa ni walewale Dathani na Abiramu waliomfuata Kora waliompinga Musa na Haruni na kumpinga BWANA.
10 Pale ambapo dunia ilifungua kinywa na kuwameza pamoja na Kora wakati ambapo wafuasi wa Kora walikufa. Wakati ule, moto uliteketeza wanaume 250, amboa wlikuwa ishara ya onyo.
11 Lakini uzao wa Kora haukufa.
12 Ukoo wa uzao wa Simeoni walikuwa hawa wafuatao: Kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli, kwa Jamini, ukoo wa Wajamini, kwa Jakini, ukoo wa Wajakini,
13 kwa Zera, ukoo wa Wazera, kwa Shauli, ukoo wa Washauli.
14 Hizi ndizo koo za uzao wa Simeoni, idadi yao ilikuwa wanaume 22, 200.
15 Koo za uzao wa Gadi zilikuwa hizi: Kwa Zefoni, Ukoo wa Wazefoni, kwa Hagi, ukoo wa Wahagi, kwa Shuni, ukoo wa Washuni,
16 kwa Ozini, ukoo wa Waozini, kwa Eri, ukoo wa Waeri,
17 kwa Arodi, ukoo wa Waarodi, kwa Areli, ukoo wa Waareli.
18 Hizi ndizo koo za uzao wa Gadi, idadi yao walikuwa wanaume 40, 500.
19 Wana wa Yuda walikwa Er na Onani, lakini hawa walifia katika nchi ya Kanaani.
20 Koo zingine za uzao wa Yuda zilikuwa hizi: Kwa Shela, ukoo wa Washela, kwa Perezi, ukoo wa Waperezi, na kwa Zera, ukoo wa Wazera.
21 Uzao wa Perezi walikuwa hawa: Kwa Hezroni, ukoo wa Wahezroni, kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.
22 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda, idadi yao ilikuwa wanaume 76, 500.
23 Koo za uzao wa Isakari zilikuwa hizi: Kwa Tola, ukoo wa Watola, kwa Puva, ukoo wa Wapuva,
24 kwa Jashubu, ukoo wa Wajashubu, kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.
25 Hizi ndizo zilikuwa koo za Isakari, Idadi yao ilikuwa wanaume 64, 300.
26 Koo za uzao wa Zabuloni zilikuwa hizi: Kwa Seredi, ukoo wa Waseredi, kwa Eloni, ukoo wa Waeloni, kwa Jahaleeli, ukoo wa Wajahaleeli.
27 Hizi ndizo zilikuwa koo za Zabuloni, idadi y ao ilikuwa wanaume 60, 500.
28 Koo za uzao wa Ysufu zilikuwa Manase na Efraimu.
29 Huu ndio uliokuwa uzao wa Manase: Kwa Machiri, ukoo wa Wamachiri (Machiri ndiye aliyekuwa baba wa Giliedi), kwa Giliedi, ukoo wa Wagiliedi.
30 Wazo wa Giliedi walikuwa hawa wfuatao: Kwa Lezeri, ukoo wa Walezeri, kwa Helweki, ukoo wa Waheleki, kwa Asrieli,
31 ukoo wa Asrieli wa Waasrieli, kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu,
32 kwa Shemida, ukoo wa Washemida, kwa Hefa, ukoo wa Wahefa.
33 Zelofehadi mwana wa Hefa hakuwa na watoto wa kiume bali alikuwa na mabinti. Majina ya binti zake yalikuwa Mahilahi, Noha, Hoglaha, Milika, na Tiriza.
34 Hizi ndizo koo za Manase, idadi yao ilikuwa wanaume 52, 700.
35 Koo za wana wa uzao wa Efraimu zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuthelaha, ukoo wa Washutheleha, kwa Becheri, ukoo wa Wabecheri, kwa Tahana, ukoo wa Watahana.
36 Uzao wa Shuthelaha walikuwa, kwa Erani, ukoo wa Waerani.
37 Hizi ndizo koo za uzao wa Efraimu, idadi yao ilikuwa wanaume 32, 500. Huu ndio uzao wa Yusufu, uliohesabiwa toka kila koo zao.
38 Koo za uzao wa Benjamini zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Bela ukoo wa Wabela, kwa Ashibeli, ukoo wa Washibeli, kwa Ahiramu, ukoo wa Wahiramu,
39 kwa Shefufamu, ukoo wa Washefumamu, kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.
40 Wana wa Bela walikuwa ni Ardi na Naamani. Kutoka kwa Ardi ulijitokeza ukoo wa Waardi, na kutoka kwa Naamani ukajaitokeza ukoo wa Wanaamani.
41 Hizi ndizo koo za uzao wa Benjamini. Idadai yao ilikuwa wanaume 45, 600.
42 Kooo za uzao wa Dani zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo koo za uzao wa Dani.
43 Idadi ya koo zote za Washuhamu ilikuwa wanaume 64, 400.
44 Koo za uzao wa Asheri zilikuwa zifuatazo: Kwa Imna, ukoo wa Waimna, kwa Ishvi, ukoo wa Waishivi, kwa Beria, ukoo wa Waberia.
45 Uzao wa Beria walikuwa hawa: Kwa Heberi, ukoo wa Waheberi, kwa Malikieli, ukoo wa Wamalikieli.
46 Jina la binti wa Asheri lilikuwa Sera.
47 Hizi ndizo koo za uzao wa Asheri, idadi yao ilikuwa wanaume 53, 400.
48 Koo za uzao wa Naftali zilikuwa zifuatazo: Kwa Jahazeeli, ukoo wa Wajahazeel, kwa Guni, ukoo wa Waguni,
49 kwa Jezeri, ukoo wa Wajezeri, kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.
50 Hizi ndizo zilizokuwa koo za uzao wa Naftali, idadi yao walikuwa wanaume 45, 000.
51 Hii ndiyo iliyokuwa jumla kuu ya wanaume wa Israeli: 601, 730.
52 BWANA akanena na Musa akamwambia,
53 Ile ardhi itagawanywa kati ya wanaume hawa kama urithi wao kwa kufuata idadi ya majina yao.
54 Kwa zile koo kubwa utawagawia urithi mkubwa, na kwa koo ndogo ndogo utawagawia urithi kidogo. Kwa kila familia utawapa urithi kufuata idadi ya wanaume waliohesabiwa.
55 Lakini ardhi itagawiwa kwa kupigiwa kura. Watairithi nchi kama itakavyogawiwa kwa kufuata koo za mababu.
56 Urithi huu utagiwiwa kufuata koo kubwa na ndogo, watagawiwa kwa kufuata kura zitakavyokuwa.
57 Koo za Walawi, zilizohesabiwa kwa kufuata ukoo kwa ukoo, walikuwa hivi: Kwa Gerishoni, ukoo wa Wagerishoni, kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi, kwa Merari, ukoo wa Wamerari.
58 Koo za walawi zilikuwa hzi: ukoo wa Walibni, Ukoo wa Wahebroni, ukoo wa Wamahali, ukoo wa Wamushi, na ukoo wa Wakora. Kohathi alikuwa wa uzao wa Amramu.
59 Jina la mke wa Amramu lilikuwa Jokibed, wa ukoo wa Lawi, aliyekuwa amezaliwa kwa Walawi kule Misri. Alimzalia Amramu watoto wao, ambao walikuwa ni Haruni, Musa, na Miriamu dada yao.
60 Kwa Haruni alizaliwa Nadabu na Abihu, Eliazari na Ithamari.
61 Nadabu na Abihu walikufa walipotoa sadaka kwa BWANA sadaka ya moto isiyokubalika.
62 Waume walioheabaiwa miionigoni mwao walikuwa elfu ishirini na tatu, hawa nia wale wa umri wa mwezi mmoja na zaidi. Lakini hawakuhesabiwa kati ya wazawa wa Israeli kwa sababu hawakupewa urithi miongoni mwa wana wa Israeli.
63 Hawa nadio wale walihesabiwa na Musa na Eliazari kuhani. Waliwahesabu watu wa Israeli katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko.
64 Lakini miongoni mwa hawa hapakuwa na mwanamume aliyehasabiwa na Musa na Haruni kuhani wakati wana wa uzao wa Israeli walipohesabiwa katika jangwa la Sinai.
65 Kwa BWANA alikuwa amesema kuwa kwa hakika watu hao wote wangefia jangwani. Hapakuwa na mtu aliyebaki miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Joshua mwana wa Nuni.