< Hesabu 23 >

1 Balaamu akamwabia Balaki, “Jenga madhabahu saba kwa ajili yangu na uandae mafahari saba na kondoo dume saba.”
Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, mnitayarishie mafahali saba na kondoo dume saba.”
2 Kwa hiyo Balaki akafanya kama Balaamu alivyoomba. Kisha Balaki na Balaamu wakatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume mmoja kwa kila madhabahu.
Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema; hao wawili kila mmoja wao akatoa fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
3 Ndipo Balaamu alipomwamiba Balaki, “Simama kwenye sadaka yako ya kuteketezwa na mimi nitaenda. Labda BWANA atakuja kukutana na mimi. Chochote atakachoniambia nitakuambia.” Kwa hiyo akaenda juu ya mlima usiokuwa na miti.
Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninakwenda kando. Huenda Bwana atakuja kukutana nami. Lolote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka.
4 Wakati bado akiwa juu ya mlima. Mungu akakutana naye, na Balaamu akamwambia, “Nimejenga madhabahu saba, na nimetoa sadaka ya fahari na kondoo dume kwa kila madhabahu.”
Mungu akakutana naye, kisha Balaamu akasema, “Nimekwisha kutengeneza madhabahu saba, na juu ya kila madhabahu nimetoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.”
5 BWANA akaweka ujumbe kwenye kinywa cha Baalamu akasema, “Rudi kwa Balaki ukamwambie.”
Bwana akaweka ujumbe katika kinywa cha Balaamu na kusema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.”
6 Kwa hiyo Balaamu akarudi kwa Balaki aliyekuwa amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na viongozi wote wa Moabu walikuwa pamoja naye.
Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake akiwa na wakuu wote wa Moabu.
7 Ndipo Balaamu alipoanza kunena unabii wake akisema, “Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka katika milima ya mashariki, 'Njoo, nilaanie Yakobo kwa ajili yangu,' alisema, 'Njoo umtie unajisi Israeli,'
Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake: “Balaki amenileta kutoka Aramu, mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki. Akasema, ‘Njoo, unilaanie Yakobo; njoo unishutumie Israeli.’
8 Nawezaje kuwalaani wale ambao Mungu hajawalaani? Nawezaje kuwapinga wale ambao Mungu hawapingi?
Nitawezaje kuwalaani, hao ambao Mungu hajawalaani? Nitawezaje kuwashutumu hao ambao Bwana hakuwashutumu?
9 Kwa kuwa kutoka juu ya miamba Ninamwona; kutoka kwenye milima ninamtazama. Kuna watu wanaoishi pekee yao na hawajioni wenyewe kama ni taifa la kawaida.
Kutoka vilele vya miamba ninawaona, kutoka mahali palipoinuka ninawatazama. Ninaliona taifa ambalo wanaishi peke yao, nao hawahesabiwi kama mojawapo ya mataifa.
10 Nani awezaye kuyahesabu mavumbi ya Yakobo au kuhesabu hata robo ya Israeli? Naomba nife kifo cha mtu mwenye haki, na mwisho wa maisha yangu uwe kama wake!”
Ni nani awezaye kuhesabu mavumbi ya Yakobo, au kuhesabu robo ya Israeli? Mimi na nife kifo cha mtu mwenye haki, na mwisho wangu na uwe kama wao!”
11 Balaki akamwambia Balaamu, “Umenifanyia nini? Nilikuleta ili uwalaani maadui wangu, lakini ona, umewabariki,”
Balaki akamwambia Balaamu, “Ni nini ulichonitendea? Nimekuleta ulaani adui zangu, lakini wewe badala yake umewabariki!”
12 Balaamu akajibu akasema, “Kwa nini nisiwe mwangalifu kusema kile ambacho BWANA anaweka kinywani mwangu?”
Balaamu akajibu, “Je, hainipasi kusema kile Bwana anachoweka katika kinywa changu?”
13 Basi Balaki akamwambia, “Hebu uje nami kwenye eneo jingine ili uwaone. Utakaowaona ni wale wa karibu tu, huwezi kuwaona wote. Huko sasa unaweza kunilaania hawa watu.”
Ndipo Balaki akamwambia, “Twende pamoja mahali pengine ambapo unaweza kuwaona; utawaona baadhi tu wala si wote. Nawe kutoka huko, unilaanie hao.”
14 Kwa hiyo akampeleka Balaamu kwenye shamba la Zofimu, lililo juu ya Mlima Pisiga, na kule akajenga madhabau zingine saba. Akatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume kwa kila madhabahu.
Basi akampeleka kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Pale akajenga madhabahu saba na kutoa sadaka ya fahali na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.
15 Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Simama hapa karibu na sadaka zako, wakati mimi naenda kukutana na BWANA kule.”
Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati ninapokwenda kuonana na Mungu kule.”
16 Kwa hiyo BWANA akakutana na Balaamu na kumwekea ujumbe kinywani mwake. Alimwambia, “Rudi kwa Balaki ukamwambie huu ujumbe toka kwangu.”
Bwana akakutana na Balaamu, akaweka ujumbe katika kinywa chake akasema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.”
17 Balaamu akamrudia, na tazama, alikuwa amesimama karibu na sadaka zake za kuteketezwa, na vionigozi wa Moabu walikuwa pamoja naye. Balaki akamwuliza, “BWANA amekwambiaje?”
Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake, akiwa na wakuu wa Moabu. Balaki akamuuliza, “Je, Bwana amesema nini?”
18 Balaamu akaanza kutoa unabii. Akasema, “Inuka, Balaki na usikilize. Nisikilize mimi wewe mwana wa Zippori.
Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake: “Balaki, inuka na usikilize, nisikie mimi, wewe mwana wa Sipori.
19 Mungu siyo mtu, kwamba umdanganye, au mwanadamu awezaye kubadili mawazo. Je, alishawahi kuahidi kitu pasipo kukitekeleza? Je, alishawahi kusema kuwa atafanya kitu bila kufanya kama alivyosema?
Mungu si mtu, hata aseme uongo, wala yeye si mwanadamu, hata ajute. Je, anasema, kisha asitende? Je, anaahidi, asitimize?
20 Tazama, Mimi nimeamriwa kuwabariki. Mungu ametoa baraka, nami siwezi kuibadilisha.
Nimepokea agizo kubariki; amebariki, nami siwezi kubadilisha.
21 Hajawahi kuona magumu katika Yakobo au tabu katika Israeli. BWANA Mungu wao yuko pamoja nao, na kelele za wafalme wao ziko pamoja nao.
“Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo, wala taabu katika Israeli. Bwana, Mungu wao yu pamoja nao, nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao.
22 Mungu aliwatoa Misri kwa nguvu kama za nyati.
Mungu aliwatoa kutoka Misri; wao wana nguvu za nyati.
23 Hakuna uganga utakaofanikiwa dhidi ya Yakobo, na hakuna uchawi utakaomwumiza Israeli. Badala yake, itasemwa juu ya Yakobo na Israeli, 'Tazama kile ambacho Mungu amefanya!'
Hakuna uchawi dhidi ya Yakobo, wala hakuna uaguzi dhidi ya Israeli. Sasa itasemwa kuhusu Yakobo na Israeli, ‘Tazama yale Mungu aliyotenda!’
24 Tazama, watu wanainuka kama simba jike, kama vile simba ainukavyo na kuvamia. Halali chini mpaka ale windo lake na kunywa damu ya windo lake,”
Taifa lainuka kama simba jike; linajiinua kama simba ambaye hatulii mpaka amalize kurarua mawindo yake na kunywa damu ya mawindo yake.”
25 Kisha Balaki akamwambia Balaamu, “Kamwe usiwalaani wala kuwabariki.”
Kisha Balaki akamwambia Balaamu, “Usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa!”
26 Lakini Balaamu akamjibu Balaki, “Sijakuambia kuwa nitasema yote ambayo BWANA ananiambia kusema?
Balaamu akajibu, “Je, sikukuambia ni lazima nifanye lolote analosema Bwana?”
27 Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo sasa, Nami nitakupeleka mahali pengine. Labda kule itampendeza Mungu kunilaania hawa hawa watu.”
Basi Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo, nikupeleke mahali pengine. Huenda itampendeza Mungu kukuruhusu unilaanie hao watu kutoka mahali hapo.”
28 Kwa hiyo Balaki akampeleka Balaamu juu ya Mlima Peori, ambao unalitazama chini lile jangwa,
Balaki akamchukua Balaamu juu ya Mlima Peori, unaotazamana na nyika.
29 Balaamu akamwambia Balaki, “Nijengee madhabahu saba hapa na uniandalie mafahari saba na kondoo duume saba.
Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, uandae mafahali saba na kondoo dume saba kwa ajili yangu.”
30 “Kwa hiyo Balaki akafanya kama alivyoambiwa; akatoa sadaka ya fahari na kondoo mume kwenye kila madhabahu.
Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema, kisha akatoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

< Hesabu 23 >