< Hesabu 22 >
1 Watu wa Israeli wakasafiri mpaka wakaweka kambi kwenye uwanda wa Moabu karibu na Yeriko, kwenye upande mwingine wa mto Yorodani kutoka mji ule.
以色列人起行,在摩押平原、约旦河东,对着耶利哥安营。
2 Balaki mwana wa Zippori aliona yote ambayo Israeli aliwafanyia Waamori. Moabu aliogopa sana hao watu kwa sababu walikuwa wengi sana,
以色列人向亚摩利人所行的一切事,西拨的儿子巴勒都看见了。
3 na Moabu alIwahofia wana wa Israeli.
摩押人因以色列民甚多,就大大惧怕,心内忧急,
4 Mfalme wa Moabu akawaambia wazee wa Midiani, “Huu umati utakula kila kitu tulicho nacho na maksai hula nyasi za kondeni.” Sasa Balaki mwana wa Zippori alikuwa mfalme wa Moabu.
对米甸的长老说:“现在这众人要把我们四围所有的一概舔尽,就如牛舔尽田间的草一般。”那时西拨的儿子巴勒作摩押王。
5 Akatuma wajumbe kwenda kwa Balamu mwana wa Beori, kule Petho ambayo iko karibu na mto Frati, katika nchi ya taifa lake na watu wake. Akamwita na kumwambia, “Tazama, Kuna taifa ambalo wamekuja hapa tokea Misiri. Wanafunika uso wa dunia na sasa wananifuatia mimi.
他差遣使者往大河边的毗夺去,到比珥的儿子巴兰本乡那里,召巴兰来,说:“有一宗民从埃及出来,遮满地面,与我对居。
6 Tafadhali naomba uje unilaanie hili taifa, kwa sababu wana nguvu kuliko mimi. Labda nitaweza kuwavamia na kuwafukuza watoke katika nchi yangu. Najua kuwa yeyote unayembariki hubarikiwa na yeyote unayemlaani atalaaniwa.”
这民比我强盛,现在求你来为我咒诅他们,或者我能得胜,攻打他们,赶出此地。因为我知道,你为谁祝福,谁就得福;你咒诅谁,谁就受咒诅。”
7 Kwa hiyo wazee wa Moabu na wale wa Midiani wakaondoka, pamoja nao wakachukua malipo ya uganga. Wakafika kwa Balaamu wakamwambia maneno ya Balaki.
摩押的长老和米甸的长老手里拿着卦金,到了巴兰那里,将巴勒的话都告诉了他。
8 Balaamu akawaambia, “Bakini hapa usiku wa leo. Kesho nitawaletea atakachoniambia BWANA.” Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakabaki na Balaamu kwa usiku huo.
巴兰说:“你们今夜在这里住宿,我必照耶和华所晓谕我的回报你们。”摩押的使臣就在巴兰那里住下了。
9 Mungu akaja kwa Balaamu na kumwambia, “Ni akina nani hawa waliokuja kwako?”
神临到巴兰那里,说:“在你这里的人都是谁?”
10 Balaamu akamjibu Mungu, “Balaki mwana wa Zippori, Mfalme wa Moabu amewatuma kwangu. Alisema,
巴兰回答说:“是摩押王西拨的儿子巴勒打发人到我这里来,说:
11 'Tazama hawa watu waliotoka Misri wanafunika uso wa nchi yangu. Sasa naomba uje unilaanie hawa watu. Labada nitaweza kuwa kuwashinda na kuwafukuza.'”
‘从埃及出来的民遮满地面,你来为我咒诅他们,或者我能与他们争战,把他们赶出去。’”
12 Mungu akamjiu Balaam, “Usiambatane na hao wanaume. Na usiwalaani hawa wana wa Israeli kwa sababu wamebarikiwa.”
神对巴兰说:“你不可同他们去,也不可咒诅那民,因为那民是蒙福的。”
13 Balaamu akaamka asubuhi na kuwaambia wale viongozi wa Balaki, “Rudini nchini kwenu kwa sababu BWANA amenikataza kuambatana nanyi.”
巴兰早晨起来,对巴勒的使臣说:“你们回本地去吧,因为耶和华不容我和你们同去。”
14 Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakaondoka na kurudi kwa Balaki. Wakamwambia, “Balaamu amekataa kuambatana nasi.”
摩押的使臣就起来,回巴勒那里去,说:“巴兰不肯和我们同来。”
15 Balaki akatuma viongozi wengine waliokuwa wanaheshimiwa zaidi kuliko kundi lile la awali.
巴勒又差遣使臣,比先前的又多又尊贵。
16 Wakaja kwa Balaamu na kumwambia, “Balaki mwana wa Zippori anasema hivi, 'Tafadhali hebu kitu chochote kisikuzuie kuja kwangu,
他们到了巴兰那里,对他说:“西拨的儿子巴勒这样说:‘求你不容什么事拦阻你不到我这里来,
17 kwa sababu nitakulipa malipo mazuri sana na kukupa heshima kubwa, nami nitakufanyia chochote utakachoniambia. Tafadhali sana uje unilaanie hawa watu.'”
因为我必使你得极大的尊荣。你向我要什么,我就给你什么;只求你来为我咒诅这民。’”
18 Balaamu akawajibu watu wa Balaki akawaambia, “Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitaweza kufanya dhidi ya maneno ya BWANA, Mungu wangu na kufanya pungufu au zaidi ya kile anachoniambia.
巴兰回答巴勒的臣仆说:“巴勒就是将他满屋的金银给我,我行大事小事也不得越过耶和华—我 神的命。
19 Sasa basi, tafadhali subirini hapa usiku wa leo pia, ili kwamba nipate kujifunza kitu zaidi ambacho BWANA ananiambia.”
现在我请你们今夜在这里住宿,等我得知耶和华还要对我说什么。”
20 BWANA akaja kwa Balaamu usiku ule na kumwambia, “kwa kuwa hawa watu wamekuja kukuita, inuka uende nao. Lakini utafanya tu kile nitakachokuambia kufanya.”
当夜, 神临到巴兰那里,说:“这些人若来召你,你就起来同他们去,你只要遵行我对你所说的话。”
21 Balaamu akainuka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na viongozi wa Moabu.
巴兰早晨起来,备上驴,和摩押的使臣一同去了。
22 Lakini kwa sababu alienda, hasira za Mungu zikawaka. Malaika wa BWANA akasimama barabarani kama adui wa Balaamu, aliyekuwa akimpanda yule punda. Watumishi wawili wa Balaamu walikuwa pamoja naye.
神因他去就发了怒;耶和华的使者站在路上敌挡他。他骑着驴,有两个仆人跟随他。
23 Yule punda alimwona yule malaika wa BWANA akiwa amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Yule punda akageuka na kwenda shambani. Balaamu akampiga yule punda ili arudi barabarani.
驴看见耶和华的使者站在路上,手里有拔出来的刀,就从路上跨进田间,巴兰便打驴,要叫它回转上路。
24 Sasa malaika wa BWANA akasimama kwenye njia nyembamba katikati ya mashamba ya mizabibu, na kushoto kwake kulikuwa na ukuta.
耶和华的使者就站在葡萄园的窄路上;这边有墙,那边也有墙。
25 Yule punda akamwona yule malaika wa BWANA tena. Akasogea zaidi ukutani na kuubana mguu wa Balaamu ukutani. Balaamu akampiga tena yule punda.
驴看见耶和华的使者,就贴靠墙,将巴兰的脚挤伤了;巴兰又打驴。
26 Yule malaika wa BWANA akasogea mbele zaidi kwenye eneo jingine jembamba zaidi ambalo haikuwezekana kugeuka upande mwingine.
耶和华的使者又往前去,站在狭窄之处,左右都没有转折的地方。
27 Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini ya Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake.
驴看见耶和华的使者,就卧在巴兰底下,巴兰发怒,用杖打驴。
28 Kisha BWANA akafungua kinywa cha punda na akaongea. Akamwambia Balaamu, “Nimekukosea nini kiasi kwamba umenipiga mara tatu?”
耶和华叫驴开口,对巴兰说:“我向你行了什么,你竟打我这三次呢?”
29 Balaamu akamjibu yule punda, “Ni kwa sababu umenitendea kwa ujinga. Natamani kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, kama ningekuwa nao, sasa hivi ningekuwa nimekuua.”
巴兰对驴说:“因为你戏弄我,我恨不能手中有刀,把你杀了。”
30 Yule punda akamwambia Balaamu, “Je, mimi si punda wako ambaye umenipanda maishani mwako mwote mpaka hivi sasa? Je, nimewahi kuwa na tabia ya kukufanyia hivi hapo awali?” Balaamu akasema “hapana.”
驴对巴兰说:“我不是你从小时直到今日所骑的驴吗?我素常向你这样行过吗?”巴兰说:“没有。”
31 Basi BWANA akafungua macho ya Balaamu, na akamwona malaika wa BWANA amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Balaamu akainamisha kichwa chake chini.
当时,耶和华使巴兰的眼目明亮,他就看见耶和华的使者站在路上,手里有拔出来的刀,巴兰便低头俯伏在地。
32 Yule malaika wa BWANA akamwambia, “Kwa nini umempiga punda wako mara tatu? Tazama, Nimekuja kama adui yako kwa sababu matendo yako kwangu yamekuwa maovu.
耶和华的使者对他说:“你为何这三次打你的驴呢?我出来敌挡你,因你所行的,在我面前偏僻。
33 Yule punda aliniona na akageuka kutoka kwangu mara tatu. Kama asingekuwa amegeuka kutoka kwangu, hakika ningekuwa nimekua na yeye kumwacha hai.
驴看见我就三次从我面前偏过去;驴若没有偏过去,我早把你杀了,留它存活。”
34 Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, nimetenda dhambi. Sikujua kuwa ulisimama kinyume na mimi barabarani. Kwa hiyo sasa, kama haikupendezi, Nitageuka.”
巴兰对耶和华的使者说:“我有罪了。我不知道你站在路上阻挡我;你若不喜欢我去,我就转回。”
35 Lakini yule malaika wa BWANA akamwambia Balaamu, “endelea na wale watu. Lakini utasema maneno nitakayokwambia tu.”Kwa hiyo Balaamu akaendelea na wale vioingozi wa Balaki.
耶和华的使者对巴兰说:“你同这些人去吧!你只要说我对你说的话。”于是巴兰同着巴勒的使臣去了。
36 Balaki aliposikia kuwa Balaamu alikuwa amekuja, alienda kukutana naye kule mjini Moabu pale Amoni, ambao uko mpakani.
巴勒听见巴兰来了,就往摩押京城去迎接他;这城是在边界上,在亚嫩河旁。
37 Balaki akamwambia Balaamu, “Je, mimi sikutuma watu kukuita? Basi kwa nini hukuja kwangu? Je, mimi sina uwezo wa kukufanya uheshimike?”
巴勒对巴兰说:“我不是急急地打发人到你那里去召你吗?你为何不到我这里来呢?我岂不能使你得尊荣吗?”
38 Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Tazama, mimi nimekuja kwako. Je mimi sina mamlaka ya kusema chochote? Mimi ninaweza kusema maneno ambayo Mungu ameweka kinywani mwangu.”
巴兰说:“我已经到你这里来了!现在我岂能擅自说什么呢? 神将什么话传给我,我就说什么。”
39 Balaamu akaenda na Balaki, na Wakafika Kiriathi Huzothi.
巴兰和巴勒同行,来到基列·胡琐。
40 Kisha Balaki akatoa sadaka ya maksai na kondoo na kumpatia Balaamu baadhi ya hiyo nyama na wale viongozi waliokuwa pamoja naye.
巴勒宰了牛羊,送给巴兰和陪伴的使臣。
41 Kesho yake asubuhi, Balaki akampeleka Balaamu mpaka juu mahali pa Baali. Kule juu Balaamu aliweza kuona sehemu tu ya kambi za Waisraeli.
到了早晨,巴勒领巴兰到巴力的高处;巴兰从那里观看以色列营的边界。