< Hesabu 20 >
1 Kwa hiyo wana wa Israeli, na jamii yote ya watu, wakaenda katika jangwa la Sini katika mwezi wa kwanza; wakaa Kadeshi. Hapo ndipo Miriamu alipofia na kuzikwa.
2 Huko hapakuwa na maji kwa ajili ya watu, kwa hiyo wakakusanyika kinyume na Musa na Haruni huko.
3 Watu wakamlalamikia Musa. Wakasema, “Ilikuwa ni bora kama tungelikufa wakati Waisraeli wenzetu walipokufa mbele za BWANA.
4 Kwa nini umewaleta watu wa BWANA kufia katika jangwa hili, sisi na wanyama wetu?
5 Kwa nini ulitutoa Misri na kutuleta katika eneo hili baya? Hapa hakuna nafaka, wala mitini, wala mizabibu, wala makomamanga. Na hakuna maji ya kunywa.”
6 Basi Musa na Haruni wakatoweka mbele ya mkutano huo. Wakaenda kwenye hema ya kukutania wakalala kifudifudi. Ndipo pale utukufu wa Busara wa BWANA ukaonekana kwao.
7 BWANA akanena na Musa, akamwambia,
8 “Chukua fimbo yako na uwakusanye watu, wewe na Haruni ndugu yako. Uumbie huu mwamba mbele ya macho yao, na uumuru utoe maji. Nawe utawapa maji kutoka kwenye huu mwamba, nawe utawapa maji ya kunywa hao watu na wanyama wao.”
9 Musa akachukua hiyo fimbo mbele ya BWANA, kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.
10 Kisha Musa na Haruni wakawakusanya watu pamoja mbele ya ule mwamba. Ndipo Musa akawaambia, “Sasa sikilizeni, enyi wapinzani. Lazima tuwape maji kutoka kwenye huu mwamba?”
11 Ndipo Musa akanyosha mkono wake na kuupiga ule mwamba mara mbili kwa fimbo yake, na maji mengi yakatoka. Wale watu wakanywa pamoja na wanyama wao.
12 Kisha BWANA akamwambia Musa na Haruni, “Kwa kuwa hamkuniheshimu mimi na kuniamini mbele ya watu wa Israeli, hamtawaingiza hawa watu katika nchi niliyowaahidi.
13 Mahali hapa paliitwa maji ya Meriba kwa sababu wana wa Israeli walitofautiana na BWANA pale, na akajionyesha kwao kuwa mtakatifu.
14 Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi kwa mfalme wa Edom: Ndugu yako Israeli anasema hivi: “Wewe unajua magumu yote ambayo yametupata.
15 Na unajua kuwa babu zetu walienda Misri na waliishi Misri kwa muda mrefu. Wamisri walitutendea vibaya pamoja na babu zetu.
16 Tulipomlilia BWANA, akatusikia na kututumia malaika ambaye alitutoa toka Misri. Tazama, sasa tuko Kadeshi, mji unaopakana na nchi yako.
17 Tunakuomba uturuhusu kupita katika nchi yako. Hatutapita mashambani wala kwenye mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita kwenye njia kuu ya mfalme. Hatutageuka upande wa kulia wala upande wa kushoto mpaka tutakapopita mpaka wako.”
18 Lakini mfalme wa Edomu akamjibu, “Msipite hapa. Kama mtafanya hivyo, Nitakuja na upanga kukuvamia.”
19 Ndipo wana wa Israeli wakamwambia,”tutapitia njia kuu. Kama sisi au wanyama wetu watakunywa maji yako, basi tutalipa. Tunaomba uturuhusu tupite tukitembea kwa miguu yetu, bila kufanya jambo lolote lile.”
20 Lakini mfalme wa Edomu akajibu, “Usipite hapa.” Kwa hiyo nfalme wa Edomu akawa kinyume cha Israeli kwa mkono wenye nguvu pamoja na jeshi kubwa sana.
21 Mfame wa Edomu akawazuia wana wa Israeli kupita kwenye mipaka yake. Kwa sababu ya hili, Israeli akageuka kuiacha nchi ya Edomu.
22 Kwa hiyo watu wakasafiri kutoka Kadeshi. Wana wa Israeli, watu wote, wakafika Mlima Hori.
23 BWANA akanena na Musa na Haruni hapo kwenye Mlima Hori, kwenye mpaka wa Edomu. Akasema,
24 “Sasa ni wakati wa Haruni kukusanyika na watu wake, hataingia katika nchi ile niliyowaahidi wana wa Israeli. Hii ni kwa sababu ninyi wawili hamkuitii sauti yangu pale kwenye maji ya Meriba.
25 Mchukue Haruni na Eliazari mwanaye, na uwalete juu ya Mlima Hori.
26 Umvulishi HarunI yale mavazi ya kikuhani na umvalishe Eliazari mwanaye. Haruni atakufa na kulazwa pamoja na watu wake.”
27 Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru. Wakaenda juu y a Mlima Hori na watu wote wakiona.
28 Musa akamvulisha Haruni yale mavazi ya kikuhani na kumvalisha Mwanaye Eliazari. Haruni akafa pale juu ya Mlima Hori. Kisha Musa na Eliazari wakashuka.
29 Watu walipoona kuwa Haruni amekufa, taifa lote wakamlilia Haruni kwa siku arobaini.