< Hesabu 2 >

1 BWANA akasema na Musa na Haruni tena. Akamwambia,
וידבר יהוה אל משה ואל אהרן לאמר
2 Kila mtu atapanga kulingana na mahali pake, pamoja na mabango ya baba zao. Watapanga kuzunguka hema ya kukutania kila upande.
איש על דגלו באתת לבית אבתם יחנו בני ישראל מנגד סביב לאהל מועד יחנו
3 Wale watakaopanga mashariki mwa hema ya kukutania, mahali ambapo juu huonekana wakati wa jua kuchomoza, ni makambi ya Yuda nao watakuwa katika kundi lao. Nashoni mwana wa Aminadabu ni kiongozi wa watu wa Yuda.
והחנים קדמה מזרחה דגל מחנה יהודה לצבאתם ונשיא לבני יהודה נחשון בן עמינדב
4 Idadi ya watu wa Yuda ni 74, 600.
וצבאו ופקדיהם--ארבעה ושבעים אלף ושש מאות
5 Kabila la Isakari litapanga mbele ya Yuda. Nethaneli mwana wa Zuari ataliongoza jeshi la Isakari.
והחנים עליו מטה יששכר ונשיא לבני יששכר נתנאל בן צוער
6 Idadi ya kikosi chake ni wanaume 54, 000.
וצבאו ופקדיו--ארבעה וחמשים אלף וארבע מאות
7 Kabila la Zabuloni litapanga mbele ya Isakari. Eliabu mwana wa Heloni ndiye atakayeliongoza jeshi la Zabuloni.
מטה זבולן ונשיא לבני זבולן אליאב בן חלן
8 Idadi ya kikosi chake ni 57, 400.
וצבאו ופקדיו--שבעה וחמשים אלף וארבע מאות
9 Idadi yote ya kambi y a Yuda ni 186, 400. Watakuwa wa kwanza kuondoka.
כל הפקדים למחנה יהודה מאת אלף ושמנים אלף וששת אלפים וארבע מאות--לצבאתם ראשנה יסעו
10 Upande wa kusini kutakuwa na kambi ya Reubeni katika kundi lao. Kiongozi wa kundi la Reubeni ni Elizuri mwana wa Shedeuri.
דגל מחנה ראובן תימנה לצבאתם ונשיא לבני ראובן אליצור בן שדיאור
11 Idadi ya kikosi chake ni 46, 500.
וצבאו ופקדיו--ששה וארבעים אלף וחמש מאות
12 Simeoni atapanga mbele ya Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Zurishadai.
והחונם עליו מטה שמעון ונשיא לבני שמעון שלמיאל בן צורישדי
13 Waliohesabiwa kwenye kikosi chake ni 59, 300.
וצבאו ופקדיהם--תשעה וחמשים אלף ושלש מאות
14 Kabila la Gadi litafuatia. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deuli.
ומטה גד ונשיא לבני גד אליסף בן רעואל
15 Idadi ya kikosi chake ni 45, 650.
וצבאו ופקדיהם--חמשה וארבעים אלף ושש מאות וחמשים
16 Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Reubeni, kulingana na kikosi chake, ni 151, 450. Watakuwa wa pili kuondoka.
כל הפקדים למחנה ראובן מאת אלף ואחד וחמשים אלף וארבע מאות וחמשים--לצבאתם ושנים יסעו
17 Kifuatacho, ni hema la kukutania kuondoka kambini pamoja na Walawi likiwa katikati ya kambi zote. Lazima waondoke hapo kambini kwa mpangilio huo kama walivyoingia kwenye kambi. Kila mwanamume lazima awe mahali pake kwa kufuata bango lake.
ונסע אהל מועד מחנה הלוים בתוך המחנת כאשר יחנו כן יסעו איש על ידו לדגליהם
18 Migawanyiko ya kambi y Efraimu kufuata mahali pake. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.
דגל מחנה אפרים לצבאתם ימה ונשיא לבני אפרים אלישמע בן עמיהוד
19 Hesabu ya kikosi hiki ni 40, 500.
וצבאו ופקדיהם--ארבעים אלף וחמש מאות
20 Baada ya hao lilifuata kabila la Manase. Kiongozi wa Manase ni Gamaliel mwana wa Pedazuri.
ועליו מטה מנשה ונשיא לבני מנשה גמליאל בן פדהצור
21 Hesabu ya kikosi hiki ni 32, 200.
וצבאו ופקדיהם--שנים ושלשים אלף ומאתים
22 Kabila litakalofuata ni la Benjamini. Kiongozi wa Benjamini n Abidani mwana wa Gidioni.
ומטה בנימן ונשיא לבני בנימן אבידן בן גדעני
23 Hesabu ya kikosi hiki ni 35, 000
וצבאו ופקדיהם--חמשה ושלשים אלף וארבע מאות
24 Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu ni 108, 100. Watakuwa wa tatu kuondoka.
כל הפקדים למחנה אפרים מאת אלף ושמנת אלפים ומאה--לצבאתם ושלשים יסעו
25 Upande wa kaskazini kutakuwa na kambi ya kikosi cha Dani. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.
דגל מחנה דן צפנה לצבאתם ונשיא לבני דן אחיעזר בן עמישדי
26 Hesabu ya kikosi hiki ni 62, 700.
וצבאו ופקדיהם--שנים וששים אלף ושבע מאות
27 Watu wa kabila ya Asheri watapanga mbele ya Dani. Kiongozi wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okirani.
והחנים עליו מטה אשר ונשיא לבני אשר פגעיאל בן עכרן
28 Hesabu ya Kikosi hiki ni 41, 500.
וצבאו ופקדיהם--אחד וארבעים אלף וחמש מאות
29 Kabila la Naftali ndilo litakalofuatia. Kiongozi wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.
ומטה נפתלי ונשיא לבני נפתלי אחירע בן עינן
30 Hesabu ya kikosi hiki ni 53, 400.
וצבאו ופקדיהם--שלשה וחמשים אלף וארבע מאות
31 Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Dani ni 157, 600. Hawa watakuwa wa mwisho kuondoka kambini, wakifuata bango lao.
כל הפקדים למחנה דן--מאת אלף ושבעה וחמשים אלף ושש מאות לאחרנה יסעו לדגליהם
32 Hawa ndio Waisraeli, waliohesabiwa kufuata familia zao. Wote waliohesabiwa kwenye kambi zao, kwa kufuata vikosi vyao ni 603, 550.
אלה פקודי בני ישראל לבית אבתם כל פקודי המחנת לצבאתם--שש מאות אלף ושלשת אלפים וחמש מאות וחמשים
33 Lakini Musa na Haruni hawakujumuisha Walawi kwenye Hesabu ya Waisrael. Ilikuwa kama BWANA alivyokuwa amemwagiza Musa.
והלוים--לא התפקדו בתוך בני ישראל כאשר צוה יהוה את משה
34 Watu wa Israel walifanya yote ambayo BWANA alimwagiza Musa. Walipanga kwa kufuata mabango yao. Walisafiri kutoka kambini kwa kufuata jamaa zao, kwa mpangilio wa familia za koo zao.
ויעשו בני ישראל ככל אשר צוה יהוה את משה כן חנו לדגליהם וכן נסעו--איש למשפחתיו על בית אבתיו

< Hesabu 2 >