< Hesabu 18 >
1 BWANA akamwambia Haruni, “Wewe, wana wako, na uzao wa baba yako watawajibika kwa dhambi zote zilizotendwa mahali patakatifu. Lakini wewe na wana wako pekee mtawajibika kwa uovu uliofanywa na yeyote mahali patakatifu.
耶和华对亚伦说:“你和你的儿子,并你本族的人,要一同担当干犯圣所的罪孽。你和你的儿子也要一同担当干犯祭司职任的罪孽。
2 Na ndugu zako nao wa kabila ya Lawi, kabila la ukoo wako, utawaleta pamoja na wewe ili kwamba waweze kuungana na wewe ili wakusaidie wakati wewe na wanao mnapokuwa mnatumikia mbele ya hema ya amri ya agano.
你要带你弟兄利未人,就是你祖宗支派的人前来,使他们与你联合,服事你,只是你和你的儿子,要一同在法柜的帐幕前供职。
3 Watakutumikia wewe na hema yote. Hata hivyo, wasisogee karibu na chochote ndani ya mahali patakatifu au kitu chochote kilichounganishwa na madhabahu, vinginevyo wewe na wao mtakufa.
他们要守所吩咐你的,并守全帐幕,只是不可挨近圣所的器具和坛,免得他们和你们都死亡。
4 Wataungana na wewe na kuitunza hema ya kukutania, kwa kazi zote zinazohusiana na hema. Mtu mgeni asikusogelee.
他们要与你联合,也要看守会幕,办理帐幕一切的事,只是外人不可挨近你们。
5 Wewe utaajibika kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya madhabahu ili kwamba hasira yangu isiwajilie watu wa Israeli tena.
你们要看守圣所和坛,免得忿怒再临到以色列人。
6 Tazama, Mmi mwenyewe nimewachagua ndugu zako wa kabila ya Walawi kutoka mioingoni mwa uzao wa Israeli. Wao ni zawadi kwako. walitolewa kwangu ili waifanye kazi inayohusiana na hema ya kukutania.
我已将你们的弟兄利未人从以色列人中拣选出来归耶和华,是给你们为赏赐的,为要办理会幕的事。
7 Lakini ni wewe pekee yako na wanao ndio mnaoruhusiwa kufanya kazi ya ukuhani kuhusiana na kila kitu kilichounganishwa na madhabahu na kitu chochote ndani ya lile pazia. Wewe mwenyewe lazima ukamilishe majukumu hayo. Mimi ninakupa ukuhani kama zawadi. Mgeni yeyote anayekaribia atauawa.”
你和你的儿子要为一切属坛和幔子内的事一同守祭司的职任。你们要这样供职;我将祭司的职任给你们当作赏赐事奉我。凡挨近的外人必被治死。”
8 Kisha BWANA akamwambia Haruni, “Tazama, Nimekupa majukumu ya kusimamia sadaka za kuinuliwa kwangu, na sadaka zengine takatifu ambazo wana wa Israeli wanatoa kwangu. Nimekupa sadaka hizi wewe na wana wako kuwa haki yako milele.
耶和华晓谕亚伦说:“我已将归我的举祭,就是以色列人一切分别为圣的物,交给你经管;因你受过膏,把这些都赐给你和你的子孙,当作永得的分。
9 Hivi ni vitu vitakatifu sana, amabavyo visiteketezwe kwa moto: kutoka kwenye sadaka zao-kila sadaka ya unga, kila sadaka ya dhambi, na kila sadaka ya hatia- ni vitu vitakatifu sana kwa ajili yako na wana wako.
以色列人归给我至圣的供物,就是一切的素祭、赎罪祭、赎愆祭,其中所有存留不经火的,都为至圣之物,要归给你和你的子孙。
10 Sadaka hizi ni takatifu sana; kila mume lazima aile, kwa kuwa ni vitakatifu kwako.
你要拿这些当至圣物吃;凡男丁都可以吃。你当以此物为圣。
11 Hizi ni sadaka ambazo zitakuwa zako: Sadaka zao, sadaka zote za kuinuliwa za wana wa Israeli. Nimekupa wewe, wana wako na binti zako kuwa gawio lako la milele. Kila mmoja ambaye ni msafi katika familia yako anaweza kula sadaka zozote katika hizi.
以色列人所献的举祭并摇祭都是你的;我已赐给你和你的儿女,当作永得的分;凡在你家中的洁净人都可以吃。
12 Mafuta yote mazuri, ile divai nzuri yote mpya na unga, malimbuko ambyo watu hutoa kwangu- vitu hivi vyote nimekupa wewe.
凡油中、新酒中、五谷中至好的,就是以色列人所献给耶和华初熟之物,我都赐给你。
13 Mavuno ya kwanza yaliyoiva yaliyo katika ardhi yao ambayo wanaleta kwangu, yatakuwa yako. Kila mtu aliye msafi kwenye famila yako anaweza kula vitu hivi.
凡从他们地上所带来给耶和华初熟之物也都要归与你。你家中的洁净人都可以吃。
14 Kila kitu kilichotolewa wakfu katika Israeli kitakuwa chako.
以色列中一切永献的都必归与你。
15 Kila kitu kinachofungua tumbo, kila limbuko ambalo watu hutoa kwa BWANA, vyote vya watu na wanyama, vitakuwa vyako. Hata hivyo, watu lazima wawakomboe wazaliwa wa kwanza wa kiume, na watawakomboa wazaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi.
他们所有奉给耶和华的,连人带牲畜,凡头生的,都要归给你;只是人头生的,总要赎出来;不洁净牲畜头生的,也要赎出来。
16 Wale ambao wanahitaji kukombolewa na watu watakombolewa wakiwa na umri wa mwezi mmoja. Ndipo watu watawakomboa kwa bei ya shekeli tano, kwa kiwango cha shekeli za mahali patakatifu, ambacho ni sawa na gera ishirini.
其中在一月之外所当赎的,要照你所估定的价,按圣所的平,用银子五舍客勒赎出来(一舍客勒是二十季拉)。
17 Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwana wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi-msiwakomboe hawa wanyama, wametengwa kwa ajili yangu. Utanyunyizia damu yake madhabahuni na kuteketeza mafuta yao kama sadaka ya moto, ambayo ni harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.
只是头生的牛,或是头生的绵羊和山羊,必不可赎,都是圣的,要把它的血洒在坛上,把它的脂油焚烧,当作馨香的火祭献给耶和华。
18 Nyama yao itakuwa yako. Kama kidali cha kuinuliwa na paja la kulia, nyama yao itakuwa yako.
它的肉必归你,像被摇的胸、被举的右腿归你一样。
19 Sadaka yote takatifu ambayo watu wa Israeli wanaitoa kwa BWANA, nimekupa wewe, na wana wako na binti zako walio pamoja nawe. Kama gawio la kudumu. Hili ni agano la milele la chumvi, agano linalofunga milele, mbele za BWANA kwako wewe na uzao wako walio pamoja na wewe.”
凡以色列人所献给耶和华圣物中的举祭,我都赐给你和你的儿女,当作永得的分。这是给你和你的后裔、在耶和华面前作为永远的盐约。”
20 BWANA akasema na Haruni. “hautakuwa na urithi katika ardhi ya watu, wala hautakuwa na gawio miongoni mwa watu. Mimi ndimi gawiio lenu na urithi wenu miongoni mwa watu wa Israeli.
耶和华对亚伦说:“你在以色列人的境内不可有产业,在他们中间也不可有分。我就是你的分,是你的产业。”
21 Tazama, Nimewapatia uzao wa Lawi, zaka zote za Israeli kuwa urithi wao kwa sababu ya huduma wanayotoa katika hema ya kukutania.
“凡以色列中出产的十分之一,我已赐给利未的子孙为业;因他们所办的是会幕的事,所以赐给他们为酬他们的劳。
22 Kuanzi a sasa, watu wa Israeli wasisogee karibu na hema ya kukutania, vinginevyo wataajibika kwa dhambi hii na kufa.
从今以后,以色列人不可挨近会幕,免得他们担罪而死。
23 Walawi wafanya kazi inayohusiana na hema ya kukutania. Wataajibika kwa dhambi inyohusiana na hema. Hii itakuwa sheri ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Na miongoni mwa watu wa Israeli hawa hawatakuwa na urithi.
惟独利未人要办会幕的事,担当罪孽;这要作你们世世代代永远的定例。他们在以色列人中不可有产业;
24 Kwa kuwa zaka za wana wa Israeli, wanazotoa kama mchango kwangu -ndivyo hivyo ambavyo nimewapa Walawi kuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu ya kuwaambia, Kuwa hawatakuwa na urithi kati ya watu wa Israeli.
因为以色列人中出产的十分之一,就是献给耶和华为举祭的,我已赐给利未人为业。所以我对他们说:‘在以色列人中不可有产业。’”
25 BWANA akanena na Musa, akamwambia,
耶和华吩咐摩西说:
26 “Inakupasa ukaseme na Walawi uwaambie, 'Mnapopokea zaka toka kwa watu ambayo BWANA amewapa kutoka kwao kuwa urithi, ndipo na nyie mtakapotoa sehemu ya kumi ya zaka hizo.
“你晓谕利未人说:你们从以色列人中所取的十分之一,就是我给你们为业的,要再从那十分之一中取十分之一作为举祭献给耶和华,
27 Zaka yenu itahesabika kama moja ya mapato ya sakafu ya kupuria nafaka ya mazao yenu au mazao ya vinu vya kukamulia zabibu.
这举祭要算为你们场上的谷,又如满酒榨的酒。
28 Kwa hiyo na ninyi lazima mtoe mchango wenu kwa BWANA kutokana na zaka mnazopata kutoka kwa watu wa Israeli. Kutokana na hizo mtatoa matoleo yenu kwa Haruni yule kuhani.
这样,你们从以色列人中所得的十分之一也要作举祭献给耶和华,从这十分之一中,将所献给耶和华的举祭归给祭司亚伦。
29 Kwa kila sadaka mnayopata, mtatoa matoleo yenu kwa BWANA. Mtafanya hivi kutokana na vitu vizuri na vitakatifu sana ambavyo mmepewa.
奉给你们的一切礼物,要从其中将至好的,就是分别为圣的,献给耶和华为举祭。
30 Kwa hiyo utawaambia, 'Mnapotoa hayo matoleo mazuri, ndipo itahesabika kwa Walawi kuwa ni mazao yao kutoka kwenye sakafu za kupuria na vinu vyao vya kukamulia.
所以你要对利未人说:你们从其中将至好的举起,这就算为你们场上的粮,又如酒榨的酒。
31 Ndipo matakapokula nafaka zote zinazobaki mahali popote, ninyi na famailia zenu kwa sababu ndiyo malipo yenu ya kazi y a kwenye hema ya kukutania.
你们和你们家属随处可以吃;这原是你们的赏赐,是酬你们在会幕里办事的劳。
32 Hamtakuwa na hatia yeyote kwa kuvila na kuvinywa, kama mtatoa kwa BWANA matoleo yenu mazuri mliyopokea. Lakini msizinajisi sadaka takatifu za wana wa Israeli, vinginevyo mtakufa.,”
你们从其中将至好的举起,就不至因这物担罪。你们不可亵渎以色列人的圣物,免得死亡。”