< Hesabu 14 >

1 Usiku huo watu wote walilia kwa sauti.
ותשא כל העדה ויתנו את קולם ויבכו העם בלילה ההוא
2 Watu wote wa Israeli wakamlalamikia Musa na Haruni. Watu wote wakawaambia, “Ni bora kama tungelifia katika nchi ya Misri, au katika hili!
וילנו על משה ועל אהרן כל בני ישראל ויאמרו אלהם כל העדה לו מתנו בארץ מצרים או במדבר הזה לו מתנו
3 Kwa nini BWANA alituleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa watumwa wao. Je, si bora kwetu kurudi Misri?”
ולמה יהוה מביא אתנו אל הארץ הזאת לנפל בחרב--נשינו וטפנו יהיו לבז הלוא טוב לנו שוב מצרימה
4 Wakasemezana wao kwa wao, “Na tuchague kiongozi mwingine, turudi Misri.”
ויאמרו איש אל אחיו נתנה ראש ונשובה מצרימה
5 Ndipo Musa na Haruni wakalala kifudifudi mbele ya kundi lote la wana wa Israeli.
ויפל משה ואהרן על פניהם לפני כל קהל עדת בני ישראל
6 Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, ambao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa waemtumwa kwenda kuipeleleza nchi wakachana mavazi yao.
ויהושע בן נון וכלב בן יפנה מן התרים את הארץ--קרעו בגדיהם
7 Wakawaambia watu wote wa Israeli. Walisema, “Ile nchi tuliyopita katikati yake ni nchi nzuri sana.
ויאמרו אל כל עדת בני ישראל לאמר הארץ אשר עברנו בה לתור אתה--טובה הארץ מאד מאד
8 Kama BWANA amependezwa nasi, basi atatuingiza katika nchi hii na kutupatia. Ile nchi inatiririka maziwa na asali.
אם חפץ בנו יהוה--והביא אתנו אל הארץ הזאת ונתנה לנו ארץ אשר הוא זבת חלב ודבש
9 Lakini msimwasi BWANA, na msiwahofie hao wakazi wa nchi hiyo. Tutawateketeza kwa urahisi kama kula chakula. Ulinzi wao utaondolewa kutoka kwao, kwa sababu BWANA yuko pamoja nasi. Msiwahofie.”
אך ביהוה אל תמרדו ואתם אל תיראו את עם הארץ כי לחמנו הם סר צלם מעליהם ויהוה אתנו אל תיראם
10 Lakini watu wote walitishia kuwapiga kwa mawe mpaka wafe. Kisha utukufuwa BWANA ukaonekana kwenye hema ya kukutania kwa watu wote wa Israeli.
ויאמרו כל העדה לרגום אתם באבנים וכבוד יהוה נראה באהל מועד אל כל בני ישראל
11 BWANA akamwambi Musa, “watu hawa watanidharau hadi lini? Wataendelea kutoniamini mpaka lini? Nijapokuwa nimefanya ishara kwa nguvu zangu kati yao?
ויאמר יהוה אל משה עד אנה ינאצני העם הזה ועד אנה לא יאמינו בי בכל האתות אשר עשיתי בקרבו
12 Nitawapiga kwa mapigo, na kuwaondolea urithi, na kufanya taifa kubwa kutoka kwenye ukoo wako ambalo litakuwa kubwa na lenye nguvu kuliko wao.
אכנו בדבר ואורשנו ואעשה אתך לגוי גדול ועצום ממנו
13 Musa akamwambia BWANA, “Kama utafanya hivi, Na Wamisiri wakisikia habari hizi, na kwa sababu uliwaokoa kutoka kwao kwa nguvu zako.
ויאמר משה אל יהוה ושמעו מצרים כי העלית בכחך את העם הזה מקרבו
14 Basi watawaambia wakazi wa nchi hii. Wamesikia ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa, kwa sababu uso wako waonekana. Wingu lako husimama juu ya watu wetu. Wewe huwatangulia katika nguzo ya wingu wakati wa mchana na katika nguzo ya moto wakati wa usiku.
ואמרו אל יושב הארץ הזאת שמעו כי אתה יהוה בקרב העם הזה אשר עין בעין נראה אתה יהוה ועננך עמד עלהם ובעמד ענן אתה הלך לפניהם יומם ובעמוד אש לילה
15 Sasa kama utawaua hawa watu kama mtu mmoja, basi mataifa ambao wamesikia sifa zako watasema,
והמתה את העם הזה כאיש אחד ואמרו הגוים אשר שמעו את שמעך לאמר
16 “Kwa Sababu BWANA hana uwezo wa kuwapeleka watu hawa katika nchi ambayo aliwaapia kuwapa, ndiyo maana amewaua katika jangwa hili.'
מבלתי יכלת יהוה להביא את העם הזה אל הארץ אשר נשבע להם וישחטם במדבר
17 Sasa, nakusihi, utumie uweza wako. Kwa kuwa umesema kuwa,
ועתה יגדל נא כח אדני כאשר דברת לאמר
18 'BWANA si mwepesi wa hasira na ni mwingi wa uaminifu katika agano. Yeye husamehe uovu na uasi. Kwa vyovyote vile atafutilia hatia atakapoleta hukumu ya dhambi za mababu juu ya wazao wao, kwa kizazi cha tatu na cha nne.'
יהוה ארך אפים ורב חסד נשא עון ופשע ונקה לא ינקה--פקד עון אבות על בנים על שלשים ועל רבעים
19 Ninakusihi uwasameha watu hawa dhambi zao kwa sababu ya ukuu wa uaminifu wa agano lako, kama vile ambavyo umekuwa ukiwasamehe watu hawa tokea wakati wakiwa Misri mpaka sasa.”
סלח נא לעון העם הזה--כגדל חסדך וכאשר נשאתה לעם הזה ממצרים ועד הנה
20 BWANA akasema, Nimewasamehe kwa kama ulivyoomba,
ויאמר יהוה סלחתי כדברך
21 bali kama Niishivyo, na kama vile dunia yote itakavyojazwa na utukufu wangu,
ואולם חי אני וימלא כבוד יהוה את כל הארץ
22 watu wote walioona utukufu wangu na ishara za nguvu zangu nilizotenda kule Misri na kule jangwani - Lakini bado wamenijaribu mara kumi sasa na hawakuisikiliza sauti yangu.
כי כל האנשים הראים את כבדי ואת אתתי אשר עשיתי במצרים ובמדבר וינסו אתי זה עשר פעמים ולא שמעו בקולי
23 Kwa hiyo nasema kwamba hakika hawataiona nchi ile ambayo niliwaahdi kuwapa mababu zao. Hakuna hata mmoja wao ambao wamenidharau watakaoiona,
אם יראו את הארץ אשר נשבעתי לאבתם וכל מנאצי לא יראוה
24 isipokuwa mtumishi wangu Kalebu, kwa sababu alikuwa na roho nyingine. Yeye amenifuata kwa ukamilifu; Yeye nitampeleka katika nchi hiyo ambayo alienda kuipeleleza. Wazao wake wataimilki.
ועבדי כלב עקב היתה רוח אחרת עמו וימלא אחרי--והביאתיו אל הארץ אשר בא שמה וזרעו יורשנה
25 (Sasa Waamaleki na Wakanani waliishi katika bonde.) Kesho mtageuka na kwenda katika jangwa kwa njia ya bahari ya Shamu.”
והעמלקי והכנעני יושב בעמק מחר פנו וסעו לכם המדבר--דרך ים סוף
26 BWANA akanena na Musa na Haruni, akasema,
וידבר יהוה אל משה ואל אהרן לאמר
27 “Nitaivumilia jamii ya watu hawa waovu ambao wananinung'unikia mpaka lini? Nimeyasikia malalamiko ya wana wa Israeli dhidi yangu.
עד מתי לעדה הרעה הזאת אשר המה מלינים עלי את תלנות בני ישראל אשר המה מלינים עלי--שמעתי
28 Waambie, 'Kama niishivyo,' asema BWANA, 'kama vile mlivyosema katika masikio yake, nitawafanyia jambo hili:
אמר אלהם חי אני נאם יהוה אם לא כאשר דברתם באזני כן אעשה לכם
29 Maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili, Ninyi nyote mliolalamika dhidi yangu, ninyi mliohesabiwa kwenye ile sensa, idadi yote ya watu kuanzia umri wa mika ishirini na kuendelea.
במדבר הזה יפלו פגריכם וכל פקדיכם לכל מספרכם מבן עשרים שנה ומעלה אשר הלינתם עלי
30 Kwa hakika hamtaingia kwenye ile nchi ambayo niliahidi kuwapa kuwa makazi yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Joshua mwana wa Nuni.
אם אתם תבאו אל הארץ אשר נשאתי את ידי לשכן אתכם בה--כי אם כלב בן יפנה ויהושע בן נון
31 Bali watoto wenu ambao mlisema kuwa watakuwa watumwa, wao ndio nitakaowapeleka katika nchi hiyo. Wao wataifurahia nchi ambayo nInyi mmeikataa!
וטפכם--אשר אמרתם לבז יהיה והביאתי אתם--וידעו את הארץ אשר מאסתם בה
32 Lakini ninyi, maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili.
ופגריכם אתם--יפלו במדבר הזה
33 Watoto wenu watakuwa wachungaji katika jangwa hili kwa muda wa miaka arobaini. Lazima watabeba madhara ya matendo yenu ya kutokuamini mpaka mwisho wa maiti ya mwisho jangwani.
ובניכם יהיו רעים במדבר ארבעים שנה ונשאו את זנותיכם--עד תם פגריכם במדבר
34 Kama vile ilivyo hesabu ya siku ambayo mliipeleleza nchi—siku arobaini, vivyo hivyo mtabeba madhara ya dhambi zenu kwa muda wa miaka arobaini—mwaka mmoja kwa kila siku moja, na mtajua kuwa ni sawa na kuwa adui yangu.
במספר הימים אשר תרתם את הארץ ארבעים יום--יום לשנה יום לשנה תשאו את עונתיכם ארבעים שנה וידעתם את תנואתי
35 Mimi BWANA nimesema. Hakika nitafanya hivi kwa kizazi hiki chote kiovu ambacho kimekusanyika kinyume na Mimi. Wao watakatwa kabisa, na watafia hapa.'”
אני יהוה דברתי אם לא זאת אעשה לכל העדה הרעה הזאת הנועדים עלי במדבר הזה יתמו ושם ימתו
36 Kwa hiyo wale wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuingalia ile nchi wote walikufa kwa tauni mbele ya BWANA.
והאנשים אשר שלח משה לתור את הארץ וישבו וילונו (וילינו) עליו את כל העדה להוציא דבה על הארץ
37 Hawa ni wale ambao waliorudi na kutoa taarifa mbaya juu ya nchi. Hii iliwafanya watu wote wamlalamikie Musa.
וימתו האנשים מוצאי דבת הארץ רעה--במגפה לפני יהוה
38 Kati ya watu wale waliokuwa wameenda kuiangalia nchi ile, ni Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune tu ndio waliobaki hai.
ויהושע בן נון וכלב בן יפנה חיו מן האנשים ההם ההלכים לתור את הארץ
39 Musa alipowataarifu mambo haya watu wote wa Israeli waliomboleza sana.
וידבר משה את הדברים האלה אל כל בני ישראל ויתאבלו העם מאד
40 Waliamka asubuhi na mapema wakaenda juu ya mlima na kisha wakasema, “Tazama, tuko hapa, na tutaenda mahali pale ambapo BWANA ametuahidi, kwa kuwa tumetenda dhambi.”
וישכמו בבקר ויעלו אל ראש ההר לאמר הננו ועלינו אל המקום אשר אמר יהוה--כי חטאנו
41 Lakini Musa akasema, “Kwa nini sasa mnapinga amri ya BWANA? hamtafanikiwa.
ויאמר משה למה זה אתם עברים את פי יהוה והוא לא תצלח
42 Msiende, kwa sababu BWANA hayuko pamoja nanyi kuwalinda dhidi ya maadui zenu.
אל תעלו כי אין יהוה בקרבכם ולא תנגפו לפני איביכם
43 Waamaleki na Wakanaani wako kule, na mtakufa kwa upanga kwa sababu mliumtegea mgongo BWANA na hamkumfuata. Kwa hiyo hatakuwa pamoja nanyi.
כי העמלקי והכנעני שם לפניכם ונפלתם בחרב כי על כן שבתם מאחרי יהוה ולא יהיה יהוה עמכם
44 Lakini walithubutu kukwea mlimani; lakini si Musa wala Sanduku la agano la BWANA walioondoka kambini.
ויעפלו לעלות אל ראש ההר וארון ברית יהוה ומשה לא משו מקרב המחנה
45 Kisha Waamaleki walikuja chini, pia wale Wakanaani walioshi kwenye hiyo milima. Wakawavamia Waisreli wakawapiga na kuwaangusha mpaka Horima.
וירד העמלקי והכנעני הישב בהר ההוא ויכום ויכתום עד החרמה

< Hesabu 14 >