< Hesabu 13 >
1 Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, “tuma watu waende kuipeleleza nchi ya Kanani, ambayo nimewapa wana wa Israeli.
2 Tuma mwanamume mmoja kutoka kila jamaa ya kabila. Kila mwanamume awe kiongozi katika kabila lake.”
3 Musa akawatuma kutoka jangwa la Parani, ili watii amri ya BWANA. Watu wote hao walikuwa viongozi wa watu wa Israeli.
4 Majina yao yalikuwa haya yafuatayo: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;
5 Kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
6 Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
7 Kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yusufu,
8 Kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
9 Kutoka kabila la Benjamini, Paliti mwana wa Rafu;
10 kutoka kabila ya Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi;
11 kutoka kabila la Yusufu (hiyo inamaanisha kutoka kabila la Manase), Gadi mwana wa Susi;
12 kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemalili;
13 kutoka kabila Asheri, Setu mwana wa Mikaili;
14 kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofisi;
15 kutoka kabila la Gadi, Geuli mwana wa Machi.
16 Haya ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuipelelza ile nchi. Musa akamwita Hoshea mwana wa Nuni kwa jina la Joshua.
17 Musa akawatuma kwenda kuipeleleza ile nchi ya Kanani. Naye akawaambia, “Mkaanzie Negebu hadi mahali pa milima.
18 Kaipelelezeni nchi kujua ni nchi ya namna gani. Wachunguzeni watu wake, kama ni watu wenye nguvu au dhaifu, kama ni wachache au ni wengi.
19 Chunguzeni nchi hiyo wanayoishi ni nchi ya namna gani. Ni nzuri au mbaya? Miji yao ikoje? Je iko kama kambi au ni miji yenye ngome?
20 Chunguzeni ni nchi ya namna gani, kama ni njema kwa mazao au la kama kuna miti au hapana. Mwe hodari mkalete sampuli za mazao ya nchi,” Sasa ni muda wa msimu wa malimbuko ya mizabibu.
21 Kwa hiyo wale wanaume wakaenda kuipeleleza ile nchi kutoka jangwa la Sini mpaka Rehobi, karibu na Lebo Hamati.
22 Walienda kutoka Negebu nao wakafika Hebroni. Ahimani, Sheshai, na Talmai, Uzao wa Anaki nao walikuweko, Sasa Hebroni ilikuwa imejengwa miaka saba iliyokuwa imepita kabla ya Zoani wa Misri.
23 Nao walipofika katika bonde la Eshikoli, walikata matawi ya mizabibu lenye kishada cha zabibu. Na makundi mawili ya wapelelezi wakakibeba kwenye mti. Pia wakaleta makomamanga na mtini.
24 Mahali pale paliitwa Eshikoli, kwa sababu ya kishada cha mizabibu ambacho wana wa Israeli walikata kule.
25 Baada ya siku arobaini, wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
26 Wakaja kwa Musa, Haruni na kwa watu wote wa Israeli katka jangwa la Parani, kule Kadeshi. Wakaleta taarifa kwao na kwa Waisraeli wote, na kuwaonyesha matunda ya nchi ile.
27 Wakamwambia Musa, “Tulifika katika ile nchi uliyotutuma. Kwa hakika ni nchi ya kutiririka maziwa na asali. Na baadhi ya matunda yake ni haya hapa.
28 Hata hivyo, watu wanaoishi huko ni wenye nguvu. Miji yao ni mikubwa tena ina maboma. Pia tuliwaona wana wa Anaki huko.
29 Waamaleki wanaishi Negebu. Wahiti, Wayebusi, na Waamori nao wanaishi katika milima ya hiyo nchi. Wakanaani wanaishi kando ya bahari na mto Yorodani.”
30 Kisha Kalebu akawatuliza watu waliokuwa mbele ya Musa, akasema, “Twendeni tukaiteke nyara hiyo nchi, kwa kuwa tuna uhakika wa kuikamata.”
31 Lakini wale watu waliokuwa wameenda naye walisema, “Hatutaweza kuwashinda hao watu kwa kuwa wao ni hodari kuliko sisi.”
32 Kwa hiyo wakasambaza taarifa za kukatisha tamaa kwa Wana wa Israeli juu ya nchi ile waliyoipeleleza. Walisema, “Ile nchi tuliyoiona ni nchi inayowala watu wake. Watu wote tuliowaona ni watu warefu.
33 Kule tuliiona majitu, wana wa uzao wa Anaki, ambao nii uzao wa majitu. Sisi tulionekana kama panzi machoni mwao tulipojilingsnisha nao, hivyo ndivyo tulivyoonekana machoni mwao pia.”