< Nehemia 9 >

1 Siku ya ishirini na nne ya mwezi huo huo watu wa Israeli walikusanyika, nao walikuwa wamefunga, nao walikuwa wamevaa magunia, nao wakaweka vumbi juu ya vichwa vyao.
这月二十四日,以色列人聚集禁食,身穿麻衣,头蒙灰尘。
2 Wazao wa Israeli walijitenga na wageni wote. Walisimama na kukiri dhambi zao wenyewe na matendo maovu ya baba zao.
以色列人就与一切外邦人离绝,站着承认自己的罪恶和列祖的罪孽。
3 Walisimama mahali pao, na robo ya siku walisoma kutoka Kitabu cha Sheria ya Bwana Mungu wao. Na robo nyingine ya siku walikiri na kuinama mbele ya Bwana Mungu wao.
那日的四分之一站在自己的地方念耶和华—他们 神的律法书,又四分之一认罪,敬拜耶和华—他们的 神。
4 Walawi, Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebaniya, Buni, Sherebia, Bani na Kenani, walisimama juu ya ngazi, wakamwita Bwana, Mungu wao kwa sauti kubwa.
耶书亚、巴尼、甲篾、示巴尼、布尼、示利比、巴尼、基拿尼站在利未人的台上,大声哀求耶和华—他们的 神。
5 Ndipo Walawi, na Yeshua, na Kadmieli, na Bani, na Hashabneya, na Sherebia, na Hodia, na Shebania, na Pethalia, wakasema, “Simameni, mkamsifu Bwana, Mungu wenu, milele na milele.” “Libarikiwe jina lako tukufu, lililotukuka kuliko baraka zote na sifa zote.
利未人耶书亚、甲篾、巴尼、哈沙尼、示利比、荷第雅、示巴尼、毗他希雅说:“你们要站起来称颂耶和华—你们的 神,永世无尽。耶和华啊,你荣耀之名是应当称颂的!超乎一切称颂和赞美。”
6 Wewe ni Bwana. Wewe peke yako. Wewe umefanya mbinguni, mbingu za juu, na malaika wote wa vita vita, na dunia na kila kitu kilicho juu yake, na bahari na vyote vilivyomo. Unawapa wote uzima, na majeshi ya malaika wanakusujudia.
“你,惟独你是耶和华!你造了天和天上的天,并天上的万象,地和地上的万物,海和海中所有的;这一切都是你所保存的。天军也都敬拜你。
7 Wewe ndiwe Bwana, Mungu aliyemchagua Abramu, akamtoa kutoka Uri wa Wakaldayo, akamwita Ibrahimu.
你是耶和华 神,曾拣选亚伯兰,领他出迦勒底的吾珥,给他改名叫亚伯拉罕。
8 Uliona moyo wake ulikuwa mkamilifu mbele yako, nawe ukafanya pamoja naye agano la kuwapa wazao wake nchi ya Wakanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Perizi, na Myebusi, na Wagirgashi. Umeweka ahadi yako kwa sababu wewe ni mwenye haki.
你见他在你面前心里诚实,就与他立约,应许把迦南人、赫人、亚摩利人、比利洗人、耶布斯人、革迦撒人之地赐给他的后裔,且应验了你的话,因为你是公义的。
9 Uliona shida ya baba zetu Misri na ukasikia kilio chao kando ya bahari ya shamu.
“你曾看见我们列祖在埃及所受的困苦,垂听他们在红海边的哀求,
10 Wewe ulifanya ishara na maajabu juu ya Farao, na watumishi wake wote, na watu wote wa nchi yake, kwa maana ulijua kwamba Wamisri walifanya kwa kujivunia. Lakini ulijifanyia jina ambalo linasimama hadi siku leo.
就施行神迹奇事在法老和他一切臣仆,并他国中的众民身上。你也得了名声,正如今日一样,因为你知道他们向我们列祖行事狂傲。
11 Ukagawanya bahari mbele yao, wakavuka katikati ya bahari juu ya nchi kavu; na ukawatupa wale waliowa ndani ya kina, kama jiwe ndani ya maji ya kina.
你又在我们列祖面前把海分开,使他们在海中行走干地,将追赶他们的人抛在深海,如石头抛在大水中;
12 Wewe uliwaongoza kwa nguzo ya wingu wakati wa mchana, na kwa nguzo ya moto wakati wa usiku, ili kuwamulikia njiani waweze kutembea katika nuru yake.
并且白昼用云柱引导他们,黑夜用火柱照亮他们当行的路。
13 Ulishuka juu ya Mlima Sinai ukazungumza nao kutoka mbinguni ukawapa amri za haki na sheria za kweli, amri nzuri na maagizo.
你也降临在西奈山,从天上与他们说话,赐给他们正直的典章、真实的律法、美好的条例与诫命,
14 Uliwajulisha sabato yako takatifu, ukawapa amri, maagizo, na sheria kupitia Musa mtumishi wako.
又使他们知道你的安息圣日,并借你仆人摩西传给他们诫命、条例、律法。
15 Uliwapa chakula kutoka mbinguni kwa ajili ya njaa yao, na maji kutoka mwamba kwa kiu yao, ukawaambia waende kuimiliki nchi uliyowaapa kwa kiapo kuwapa.
从天上赐下粮食充他们的饥,从磐石使水流出解他们的渴,又吩咐他们进去得你起誓应许赐给他们的地。
16 Lakini wao na baba zetu walifanya uasi, nao walikuwa wakaidi, wala hawakuzitii amri zako.
“但我们的列祖行事狂傲,硬着颈项不听从你的诫命;
17 Walikataa kusikiliza, na hawakufikiri juu ya maajabu uliyofanya kati yao, lakini wakawa wakaidi, na katika uasi wao waliweka kiongozi ili wairudie hali ya utumwa. Lakini wewe ni Mungu ambaye amejaa msamaha, mwenye rehema na huruma, si mwepesi wa hasira, na wingi katika upendo thabiti. Wewe haukuwaacha.
不肯顺从,也不记念你在他们中间所行的奇事,竟硬着颈项,居心背逆,自立首领,要回他们为奴之地。但你是乐意饶恕人,有恩典,有怜悯,不轻易发怒,有丰盛慈爱的 神,并不丢弃他们。
18 Wala hukuwaacha hata walipokwisha kutoa ndama katika chuma kilichochomwa na kusema, “Huyu ndio Mungu wenu aliyekuleta kutoka Misri,” wakati walipopotoka sana.
他们虽然铸了一只牛犊,彼此说‘这是领你出埃及的神’,因而大大惹动你的怒气;
19 Wewe, kwa huruma yako, hukuwaacha katika jangwa. Nguzo ya wingu iliyowangoza njiani haikuwaacha wakati wa mchana, wala nguzo ya moto usiku iliwaangazia barabara ambayo walipaswa kutembea.
你还是大施怜悯,在旷野不丢弃他们。白昼,云柱不离开他们,仍引导他们行路;黑夜,火柱也不离开他们,仍照亮他们当行的路。
20 Uliwapa Roho wako mzuri kuwafundisha, na mana yako haukuwanyima kinywani mwao, na ukawapa maji kwa kiu yao.
你也赐下你良善的灵教训他们;未尝不赐吗哪使他们糊口,并赐水解他们的渴。
21 Kwa miaka arobaini uliwaruzuku jangwani, na hawakukosa chochote. Nguo zao hazikuchakaa na miguu yao haikuvimba.
在旷野四十年,你养育他们,他们就一无所缺:衣服没有穿破,脚也没有肿。
22 Uliwapa falme na watu, na ukawapa ardhi katika kila kona ya mbali. Basi wakaimiliki nchi ya Sihoni mfalme wa Heshboni, na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani.
并且你将列国之地照分赐给他们,他们就得了西宏之地、希实本王之地,和巴珊王噩之地。
23 Uliwafanya watoto wao kuwa wengi kama nyota za mbinguni, na ukawaingiza katika nchi. Uliwaambia baba zao waingie na kumiliki.
你也使他们的子孙多如天上的星,带他们到你所应许他们列祖进入得为业之地。
24 Basi watu wakaingia, wakaimiliki nchi, ukawashinda wenyeji wa nchi hiyo, Wakanaani. Ukawatia mikononi mwao, pamoja na wafalme wao na watu wa nchi, ili Israeli afanye nao kama walivyotaka.
这样,他们进去得了那地,你在他们面前制伏那地的居民,就是迦南人;将迦南人和其君王,并那地的居民,都交在他们手里,让他们任意而待。
25 Wao waliteka miji yenye nguvu na nchi yenye ustawi, nao wakachukua nyumba zenye vitu vyote vyema, birika zilizochimbwa, mizabibu na miti ya mizeituni, na miti ya matunda mengi. Kwa hiyo walikula na wakashiba na wakatosheka, na wakafurahi kwa wema wako.
他们得了坚固的城邑、肥美的地土、充满各样美物的房屋、凿成的水井、葡萄园、橄榄园,并许多果木树。他们就吃而得饱,身体肥胖,因你的大恩,心中快乐。
26 Basi hawakukutii na wakawaasi. Walitupa sheria yako nyuma ya migongo yao. Waliwaua manabii wako waliowaonya wakurudie wewe, nao wakafanya ukatili mkubwa.
“然而,他们不顺从,竟背叛你,将你的律法丢在背后,杀害那劝他们归向你的众先知,大大惹动你的怒气。
27 Kwa hiyo ukawatia mikononi mwa adui zao, aliyewatesa. Na wakati wa mateso yao, walikulilia na wewe uliwasikia kutoka mbinguni na mara nyingi ukawaokoa katika mikono ya adui zao, kwa sababu ya huruma zako nyingi.
所以你将他们交在敌人的手中,磨难他们。他们遭难的时候哀求你,你就从天上垂听,照你的大怜悯赐给他们拯救者,救他们脱离敌人的手。
28 Lakini baada ya kupumzika, wakafanya mabaya tena mbele yako, nawe ukawaacha mikononi mwa adui zao, kwa hiyo adui zao wakatawala juu yao. Hata walipokurudia na kukulilia, ukasikia kutoka mbinguni, mara nyingi ukawaokoa kwa sababu ya huruma yako.
但他们得平安之后,又在你面前行恶,所以你丢弃他们在仇敌的手中,使仇敌辖制他们。然而他们转回哀求你,你仍从天上垂听,屡次照你的怜悯拯救他们,
29 Uliwaonya ili wapate kurudi kwenye sheria yako. Hata hivyo walifanya kiburi na hawakusikiliza amri zako. Walifanya dhambi dhidi ya amri zako ambazo humpa uzima mtu yeyote anayezitii. Hawakuzitii, hawakuzitenda na walikataa kuzisikiliza.
又警戒他们,要使他们归服你的律法。他们却行事狂傲,不听从你的诫命,干犯你的典章(人若遵行就必因此活着),扭转肩头,硬着颈项,不肯听从。
30 Kwa miaka mingi ukachukiliana nao na kuwaonya kwa Roho wako kwa njia ya manabii wako. Hata hivyo hawakusikiliza. Kwa hiyo ukawatia mikononi mwa watu wa jirani.
但你多年宽容他们,又用你的灵借众先知劝戒他们,他们仍不听从,所以你将他们交在列国之民的手中。
31 Lakini kwa huruma zako kubwa hukuwakomesha kabisa, au kuwaacha, kwa maana wewe ni Mungu mwenye rehema na mwenye huruma.
然而你大发怜悯,不全然灭绝他们,也不丢弃他们;因为你是有恩典、有怜悯的 神。
32 Basi, Mungu wetu, Mungu wetu mkuu, mwenye nguvu na mwenye kutisha, unayeweka agano lako na upendo wako, shida zote zilizotupata sisi, wafalme wetu, wakuu wetu, na makuhani wetu, na manabii wetu, na baba zetu, na watu wako wote tangu siku za wafalme wa Ashuru mpaka leo usizihesabu kuwa ni kidogo.
“我们的 神啊,你是至大、至能、至可畏、守约施慈爱的 神。我们的君王、首领、祭司、先知、列祖,和你的众民,从亚述列王的时候直到今日所遭遇的苦难,现在求你不要以为小。
33 Wewe ni mwenye haki katika yote yaliyotupata, kwa kuwa umetenda kwa uaminifu, na tumefanya uovu.
在一切临到我们的事上,你却是公义的;因你所行的是诚实,我们所做的是邪恶。
34 Wafalme wetu, wakuu wetu, makuhani wetu, na baba zetu hawakuishika sheria yako, wala hawakuzingatia amri zako au shuhuda zako ulizowashuhudia.
我们的君王、首领、祭司、列祖都不遵守你的律法,不听从你的诫命和你警戒他们的话。
35 Hata katika ufalme wao wenyewe, wakati walifurahia wema wako kwao, katika nchi kubwa na yenye mazao uliyoweka mbele yao, hawakukutumikia au kuacha njia zao mbaya.
他们在本国里沾你大恩的时候,在你所赐给他们这广大肥美之地上不事奉你,也不转离他们的恶行。
36 Sasa sisi ni watumwa katika nchi uliyowapa baba zetu kufurahia matunda yake na zawadi zake nzuri, na tazama, sisi ni watumwa!
我们现今作了奴仆;至于你所赐给我们列祖享受其上的土产,并美物之地,看哪,我们在这地上作了奴仆!
37 Mavuno mazuri kutoka nchi yetu huenda kwa wafalme uliowaweka juu yetu kwa sababu ya dhambi zetu. Watawala juu ya miili yetu na juu ya mifugo kama wanavyopenda. Tuna shida kubwa.
这地许多出产归了列王,就是你因我们的罪所派辖制我们的。他们任意辖制我们的身体和牲畜,我们遭了大难。”
38 Kwa sababu ya yote haya, tunafanya agano thabiti kwa kuandika. Kwenye hati iliyofungwa ni majina ya wakuu wetu, Walawi, na makuhani.”
因这一切的事,我们立确实的约,写在册上。我们的首领、利未人,和祭司都签了名。

< Nehemia 9 >