< Nehemia 3 >

1 Kisha Eliashibu, kuhani mkuu, akasimama pamoja na ndugu zake makuhani, wakajenga lango la kondoo. Walitakasa na kuweka milango yake. Waliweka wakfu hadi mnara wa Hamea na hadi mnara wa Hananeli.
Eliashibu kuhani mkuu na makuhani wenzake walikwenda kufanya kazi na kulijenga upya Lango la Kondoo. Waliliweka wakfu na kuweka milango mahali pake, wakajenga hadi kufikia Mnara wa Mia, ambao waliuweka wakfu hadi Mnara wa Hananeli.
2 Baada yao watu wa Yeriko walijenga, na baada yao Zakuri mwana wa Imri alijenga.
Watu wa Yeriko wakajenga sehemu zilizopakana nao, naye Zakuri mwana wa Imri akajenga karibu nao.
3 Wana wa Senaa wakajenga lango la samaki. Wanaweka mihimili yake na kuweka milango yake na vyuma vyake na makomeo yake.
Lango la Samaki lilijengwa upya na wana wa Hasenaa. Waliweka boriti zake, na wakaweka milango yake na makomeo na nondo.
4 Meremoth aliandaa sehemu inayofuata. Yeye ni mwana wa Uria mwana wa Hakosi. Na baada yao Meshulamu akatengeneza. Yeye ni mwana wa Berekia mwana wa Meshezabeli. Karibu nao Sadoki akatengeneza. Yeye ni mwana wa Baana.
Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu iliyofuatia. Baada yake Meshulamu mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli, alifanya ukarabati na aliyemfuatia ni Sadoki mwana wa Baana.
5 Baada yao Watekoi wakatengeneza, lakini viongozi wao walikataa kufanya kazi iliyoagizwa na wakuu wao.
Sehemu iliyofuatia ilikarabatiwa na watu kutoka Tekoa, lakini wakuu wao walikataa kufanya kazi chini ya wasimamizi wao.
6 Yoyada mwana wa Pasea, na Meshulamu mwana wa Besodeya, walitengeneza lango la Kale. Wanaweka mihimili, na kuweka milango yake na vyuma vyake na makomeo yake.
Lango la Yeshana lilikarabatiwa na Yoyada mwana wa Pasea, na Meshulamu mwana wa Besodeya. Waliweka boriti zake, na wakaweka milango, makomeo na nondo.
7 Nao, Melatia Mgibeoni, na Yadoni Meronothi, watu wa Gibeoni na Mispa, walifanyia matengenezo juu ya sehemu ambapo mkuu wa mkoa wa ng'ambo ya Mto aliishi.
Karibu nao ukarabati ulifanywa na watu kutoka Gibeoni na Mispa, yaani Melati Mgibeoni, na Yadoni Mmeronothi, sehemu hizi zikiwa chini ya mamlaka ya mtawala wa Ngʼambo ya Frati.
8 Na baada yake Uzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa wafua dhahabu, akatengeneza; na baada yake Hanania, mtengenezaji wa manukato. Wakajenga tena Yerusalemu mpaka Ukuta mpana.
Uzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa masonara, alikarabati sehemu iliyofuatia, naye Hanania mmoja wa watengenezaji marashi akakarabati sehemu iliyofuatia. Walitengeneza Yerusalemu mpaka kufikia Ukuta Mpana.
9 Na baada yao Refaya mwana wa Huri akajenga. Alikuwa mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu.
Refaya mwana wa Huri, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia.
10 Na baada yao Yedaya mwana wa Harumafu akajenga karibu na nyumba yake. Na baada yake Hatushi mwana wa Hashabneya akajenga.
Kupakana na sehemu hii, Yedaya mwana wa Harumafu alikarabati sehemu iliyokuwa mkabala na nyumba yake, naye Hatushi mwana wa Hashabnea akakarabati sehemu iliyofuatia.
11 Malkiya mwana wa Harimu na Hashubu mwana wa Pahat Moabu, wajenga sehemu nyingine pamoja na mnara wa tanuu.
Malkiya mwana wa Harimu, na Hashubu mwana wa Pahath-Moabu walikarabati sehemu nyingine pamoja na Mnara wa Matanuru.
12 Baada yao Shalumu mwana wa Haloheshi, mkuu wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, akajenga, pamoja na binti zake.
Shalumu mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia akisaidiwa na binti zake.
13 Hanuni na wenyeji wa Zanoa walijenga lango la bondeni. Walijenga tena na kuweka milango yake, na vyuma vyake na makomeo yake. Walijenga dhiraa elfu hadi lango la jaa.
Lango la Bondeni lilikarabatiwa na Hanuni na wakazi wa Zanoa. Walilijenga upya, na kuweka milango yake na makomeo na nondo mahali pake. Pia walikarabati ukuta wenye urefu wa mita 450 hadi Lango la Samadi.
14 Malkiya, mwana wa Rekabu, mkuu wa wilaya ya Beth-Hakeremu, akajenga lango la jaa. Alijenga na kuweka milango yake, na vyuma vyake na makomeo yake.
Lango la Samadi lilikarabatiwa na Malkiya mwana wa Rekabu, mtawala wa wilaya ya Beth-Hakeremu. Alilijenga upya, na kuweka milango yake, na makomeo na nondo.
15 Shalumu mwana wa Kolhoze, mkuu wa wilaya ya Mispa, akajenga lango la Chemchemi. Alijenga, na kuweka kifuniko juu yake na kuweka milango yake na vyuma vyake na makomeo yake. Alijenga upya ukuta wa Pwani wa Silowamu kwa bustani ya mfalme, hadi ngazi ya kuongoza kutoka mji wa Daudi.
Lango la Chemchemi lilikarabatiwa na Shalumu mwana wa Kolhoze, mtawala wa wilaya ya Mispa. Alilijenga upya, akaliezeka na kuweka milango yake, na makomeo na nondo mahali pake. Pia alikarabati ukuta wa Bwawa la Siloamu karibu na Bustani ya Mfalme, hadi kwenye ngazi zinazoshuka kutoka Mji wa Daudi.
16 Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-suri, akajenga mahali hapo, toka maburini ya Daudi, mpaka birika lililojengwa na watu, na nyumba ya watu wenye nguvu.
Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa.
17 Baada yake, Walawi walijenga, pamoja na Rehumi mwana wa Bani na baada yake, Hashabia, mtawala wa nusu ya wilaya ya Keila, kwa wilaya yake.
Baada yake, ukarabati ulifanywa na Walawi chini ya uongozi wa Rehumu mwana wa Bani. Aliyefuatia ni Hashabia, mtawala wa nusu ya wilaya ya Keila, aliyekarabati sehemu ya wilaya yake.
18 Baada yake watu wa nchi zao walijenga, ikiwa ni pamoja na Binui mwana wa Henadadi, mkuu wa nusu ya wilaya ya Keila.
Baada yake, ukarabati ulifanywa na ndugu zao chini ya usimamizi wa Binui mwana wa Henadadi, mtawala wa nusu hiyo ingine ya wilaya ya Keila.
19 Baada yake alijenga Ezeri, mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alijenga sehemu nyingine kuelekea ghala ya silaha, kwenye kona ya ukuta.
Baada yao, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, mpaka kwenye pembe ya ukuta.
20 Baada yake Baruki, mwana wa Zakai, akajenga kwa hiari sehemu nyingine, toka kona ya ukuta mpaka mlango wa nyumba ya Eliashibu, kuhani mkuu.
Baada yake, Baruku mwana wa Zakai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe, mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliashibu kuhani mkuu.
21 Baada yake Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, akajenga sehemu nyingine, toka mlango wa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu.
Kupakana naye, Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia penye lango la nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wake.
22 Kisha baada yake makuhani, watu wa eneo hilo karibu na Yerusalemu, walijenga.
Baada yake, ukarabati ulifanywa na makuhani waliotoka eneo lililouzunguka mji.
23 Baada yao Benyamini na Hashubu walijenga kuielekea nyumba yao. Baada yao Azaria mwana wa Maaseya, mwana wa Anania, alijenga karibu na nyumba yake.
Baada yao Benyamini na Hashubu walikarabati mbele ya nyumba zao, na baada yao Azaria mwana wa Maaseya, mwana wa Anania alifanya ukarabati kando ya nyumba yake.
24 Baada yake Binui mwana wa Henadadi akajenga sehemu nyingine, kutoka nyumba ya Azaria hadi kona ya ukuta.
Baada yake, Binui mwana wa Henadadi alikarabati sehemu nyingine, kuanzia kwenye nyumba ya Azaria mpaka kwenye pembe ya ukuta.
25 Palali, mwana wa Uzai, akajenga juu ya kona ya ukuta na mnara unaoenea juu kutoka nyumba ya juu ya mfalme katika uwanda wa walinzi. Baada yake Pedaya mwana wa Paroshi akajenga.
Naye Palali, mwana wa Uzai alijenga sehemu iliyokuwa mkabala na pembe ya ukuta, mpaka kwenye mnara wa juu ambao unajitokeza kuanzia kwenye jumba la kifalme, kando ya ua wa walinzi. Baada yake, Pedaya mwana wa Paroshi,
26 Sasa watumishi wa hekalu waliokaa Ofeli walijenga mpaka upande wa Hifadhi ya Maji upande wa mashariki wa mnara unaojitokeza.
na watumishi wa Hekalu walioishi juu ya kilima cha Ofeli walikarabati hadi kufikia mkabala na Lango la Maji, kuelekea mashariki na ule mnara uliojitokeza.
27 Baada yake, Watekoi walijenga sehemu nyingine, kuelekea mnara mkubwa ulio nje, mpaka ukuta wa Ofeli.
Baada yao, watu wa Tekoa walikarabati sehemu nyingine, kuanzia mnara mkubwa utokezao hadi ukuta wa Ofeli.
28 Makuhani wakajenga juu ya lango la farasi, kila mmoja kuelekea nyumba yake.
Makuhani walifanya ukarabati juu ya Lango la Farasi, kila mmoja mbele ya nyumba yake.
29 Baada yao Sadoki, mwana wa Imeri, alijenga sehemu hiyo kuelekea nyumba yake. Na baada yake Shemaya mwana wa Shekania, mlinzi wa lango la mashariki, akajenga.
Baada yao, Sadoki mwana wa Imeri alifanya ukarabati mkabala na nyumba yake. Baada yake, Shemaya mwana wa Shekania, mlinzi wa Lango la Mashariki, alifanya ukarabati.
30 Baada yake Hanania, mwana wa Shelemia, na Hanuni, mwana wa sita wa Salafu, wakajenga sehemu nyingine. Meshulamu mwana wa Berekia akajenga kuelekea kwenye vyumba vyake.
Baada yake, Hanania mwana wa Shelemia, na Hanuni mwana wa sita wa Salafu walikarabati sehemu nyingine. Baada yao, Meshulamu mwana wa Berekia alikarabati sehemu iliyokuwa mkabala na nyumba zake za kuishi.
31 Baada yake Malkiya, mmoja wa wafua dhahabu, akajenga mpaka nyumba ya watumishi wa hekalu na wafanyabiashara waliokuwa wakielekea lango la gereza na mpaka chumba cha juu cha pembeni.
Baada yake Malkiya, mmoja wa masonara, alifanya ukarabati mpaka kwenye nyumba za watumishi wa Hekalu na wafanyabiashara, mkabala na Lango la Ukaguzi, hadi kufikia chumba kilicho juu ya pembe.
32 Wafanyabiashara wa dhahabu na wafanyabiashara walijenga kati ya chumba cha juu cha kona na Lango la Kondoo.
Masonara na wafanyabiashara walifanya ukarabati kutoka chumba kilichoko juu ya pembe hadi Lango la Kondoo.

< Nehemia 3 >