< Nehemia 13 >
1 Siku hiyo walisoma Kitabu cha Musa katika masikio ya watu. Ilionekana imeandikwa ndani yake kwamba hakuna Mwamoni au Mmoabu anapaswa kuja katika kusanyiko la Mungu, milele.
2 Hii ilikuwa kwa sababu hawakuja kwa watu wa Israeli na mkate na maji, bali walikuwa wamemwajiri Balaamu kulaani Israeli. Hata hivyo, Mungu wetu aligeuza laana kuwa baraka.
3 Mara tu waliposikia sheria, waliwatenga Israeli toka kwa kila mgeni.
4 Sasa kabla ya hapo Eliashibu kuhani akawekwa juu ya vyumba vya nyumba ya Mungu wetu. Alikuwa na uhusiano na Tobia.
5 Eliashibu alimuandalia Tobia chumba kikubwa, ambako hapo awali waliweka sadaka ya nafaka, uvumba, makala, na sehemu ya kumi ya nafaka, divai, na mafuta, ambazo ziliwekwa kwa ajili ya Walawi, waimbaji, walinzi wa mlango, na michango kwa makuhani.
6 Lakini wakati huu wote sikuwepo Yerusalemu. Kwa mwaka wa thelathini na mbili wa Artashasta mfalme wa Babeli, nilikwenda kwa mfalme. Baada ya muda nikamwomba mfalme ruhusa ya kuondoka,
7 na nikarudi Yerusalemu. Nikafahamu mabaya ambayo Eliashibu alikuwa amefanya kwa kumpa Tobia chumba cha kuhifadhi katika mahakama ya nyumba ya Mungu.
8 Nilikuwa na hasira sana na nikatupa vitabu vya nyumba ya Tobia nje ya chumba cha kuhifadhi.
9 Niliamuru kwamba watakase vituo vya kuhifadhi, nami nikarudisha ndani yao makala ya nyumba ya Mungu, sadaka ya nafaka, na uvumba.
10 Niligundua kwamba sehemu zilizotolewa kwa ajili ya kuwapa Walawi hazikutolewa kwao, ili waweze kuondoka haraka hekaluni, kila mmoja kwenda shambani kwake, kama waimbaji waliofanya walivyoondoka.
11 Kwa hiyo nikawasiliana na maafisa na kusema, 'Kwa nini nyumba ya Mungu imeachwa?' Niliwakusanya pamoja na kuwaweka kwenye nafasi zao.
12 Kisha Yuda wote wakaleta zaka ya nafaka, divai mpya, na mafuta kwenye vituo vya kuhifadhi.
13 Nikawaweka kama watunza hazina juu ya hazina, Shelemia kuhani, na Sadoki mwandishi, na Walawi, Pedaya. Hanani, mwana wa Zakuri, mwana wa Matania, alikuwa na wafuasi wao, kwa sababu walihesabiwa kuwa waaminifu. Kazi yao ilikuwa kusambaza vifaa kwa washirika wao.
14 Nikumbuke, Ee Mungu wangu, juu ya hili, wala usiondoe matendo mema niliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu na huduma zake.
15 Siku hizo nikaona watu wa Yuda waliokanyaga mvinyo siku ya Sabato, na kuleta makundi ya nafaka, na kuwapakia punda, na divai, na zabibu, na tini, na kila aina ya mizigo nzito, waliyoleta Yerusalemu siku ya Sabato. Nikashuhudia kuwa walikuwa wakiuza chakula siku hiyo.
16 Watu kutoka Tiro waliokaa Yerusalemu walileta samaki na kila aina ya bidhaa, na wakawauza siku ya Sabato kwa watu wa Yuda na katika mji!
17 Kisha nikawaambia viongozi wa Yuda, “Je! ni ubaya gani huu mnafanya, kuinajisi siku ya Sabato?
18 Je! Baba zenu hawakufanya hivyo? Je, Mungu wetu hakuleta mabaya haya juu yetu na juu ya mji huu? Sasa unaleta ghadhabu zaidi juu ya Israeli kwa kudharau Sabato.”
19 Mara ilipokuwa giza kwenye milango ya Yerusalemu kabla ya Sabato, niliamuru milango ifungwe na kwamba haifai kufunguliwa hadi baada ya Sabato. Niliwaweka baadhi ya watumishi wangu kwenye malango ili mzigo wowote usiweze kuletwa siku ya Sabato.
20 Wafanyabiashara na wauzaji wa kila aina ya bidhaa walikimbia nje ya Yerusalemu mara moja au mbili.
21 Lakini niliwaonya, “Mbona mnakaa nje ya ukuta? Ikiwa mtafanya hivyo tena, nitakuweka mikononi!” Kutoka wakati huo hawakuja siku ya sabato.
22 Nikawaamuru Walawi kujitakasa, na kuja kulinda milango, ili kutakasa siku ya Sabato. Nikumbuke kwa hili pia, Mungu wangu, na kunipatia huruma kwa sababu ya uaminifu wa agano ulilonalo kwangu.
23 Katika siku hizo niliona Wayahudi waliokuwa wameoa wanawake wa Ashdodi, Amoni na Moabu.
24 Nusu ya watoto wao walizungumza lugha ya Ashdodi, lakini hawakuweza kuzungumza lugha ya Yuda, lakini lugha ya mmoja wa watu wengine.
25 Nami nikawasiliana nao, na mimi niliwaadhibu, na nikawapiga baadhi yao na kuvuta nywele zao. Naliwaapisha kwa Mungu, nikisema, Msiwape wana wao binti zenu, wala msiwachukue binti zao kwa ajili ya wana wenu, wala ninyi wenyewe.
26 Je, Sulemani mfalme wa Israeli hakufanya dhambi kwa sababu ya wanawake hawa? Miongoni mwa mataifa mengi hapakuwa na mfalme kama yeye, na alipendwa na Mungu wake. Mungu akamfanya awe mfalme juu ya Israeli wote. Hata hivyo, wake zake wa kigeni walimfanya atende dhambi.
27 Je, tunapaswa kukusikiliza na kufanya uovu huu hata kumhalifu Mungu wetu na kuwaoa wanawake wageni?
28 Mmoja wa wana wa Yoyada, mwana wa Eliashibu, kuhani mkuu, alikuwa mkwewe na Sanbalati Mhoroni. Kwa hiyo nilimondoa kutoka mbele yangu.
29 Wakukumbushe, Mungu wangu, kwa sababu wameunajisi ukuhani, na agano la ukuhani na Walawi.
30 Kwa hiyo nimewatakasa kutoka kila kitu kigeni, na kuimarisha kazi za makuhani na Walawi, kila mmoja kwa kazi yake mwenyewe.
31 Nilitoa sadaka za kuni wakati uliowekwa na matunda ya kwanza. Nikumbuke, Mungu wangu, kwa mema.