< Nehemia 10 >
1 Wale ambao waliweka majina yao kwenye nyaraka zilizofunikwa walikuwa Nehemia mwana wa Hakalia gavana, na makuhani waliowekwa walikuwa Sedekia,
On the sealed documents were Nehemiah, the governor, son of Hakaliah and Zedekiah,
2 Seraya, Azaria, Yeremia,
Seraiah, Azariah, Jeremiah,
3 Pashuri, Amaria, Malkiya,
Pashhur, Amariah, Malchijah,
4 Hamshi, Shekania, Maluki,
Hattush, Shebaniah, Malluk,
5 Harimu, Meremothi, Obadia,
Harim, Meremoth, Obadiah,
6 Danieli, Ginethoni, Baruki,
Daniel, Ginnethon, Baruch,
7 Meshulamu, Abiya, Miyamini,
Meshullam, Abijah, Mijamin,
8 Maazia, Bilgai na Shemaya. Hawa walikuwa makuhani.
Maaziah, Bilgai, and Shemaiah. These were the priests.
9 Walawi walikuwa Yeshua mwana wa Azania, Binui wa jamaa ya Henadadi, Kadmieli,
The Levites were: Jeshua son of Azaniah, Binnui of the family of Henadad, Kadmiel,
10 na Walawi wenzake, Shebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani,
and their fellow Levites, Shebaniah, Hodiah, Kelita, Pelaiah, Hanan,
11 Mika, Rehobu, Hashabia,
Mika, Rehob, Hashabiah,
12 Zakuri, Sherebia, Shebania,
Zaccur, Sherebiah, Shebaniah,
13 Hodiya, Bani na Beninu.
Hodiah, Bani, and Beninu.
14 Viongozi wa watu walikuwa Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani,
The leaders of the people were: Parosh, Pahath-Moab, Elam, Zattu, Bani,
16 Adoniya, Bigwai, Adini,
Adonijah, Bigvai, Adin,
17 Ateri, Hezekia, Azuri,
Ater, Hezekiah, Azzur,
18 Hodia, Hashumu, Besai,
Hodiah, Hashum, Bezai,
19 Harifu, Anathothi, Nobai,
Hariph, Anathoth, Nebai,
20 Magpiashi, Meshulamu, Heziri,
Magpiash, Meshullam, Hezir,
21 Meshezabeli, Sadoki, Yadua,
Meshezabel, Zadok, Jaddua,
22 Pelatia, Hanani, AnaYA,
Pelatiah, Hanan, Anaiah,
23 Hoshea, Hanania, Hashubu,
Hoshea, Hananiah, Hasshub,
24 Haloheshi, Pilha, Shobeki,
Hallohesh, Pilha, Shobek,
25 Rehumu, Hashabna, Maaseya,
Rehum, Hashabnah, Maaseiah,
27 Maluki, Harimu na Baana.
Malluk, Harim, and Baanah.
28 Na watu wengine waliokuwa makuhani, na Walawi, na walinzi wa malango, na waimbaji, na watumishi wa hekalu, na wote waliokuwa wamejitenga wenyewe na watu wa nchi za jirani, kwa sheria ya Mungu, na wanawake zao, na wana wao, na Binti zao, wote walio na ujuzi na ufahamu,
As for the rest of the people, who were priests, Levites, gatekeepers, singers, temple servants, and all who had separated themselves from the people of the neighboring lands and pledged themselves to the law of God, including their wives, their sons and their daughters, all who have knowledge and understanding,
29 walijiunga na ndugu zao, wakuu wao, na kujifunga katika laana na kiapo cha kutembea katika sheria ya Mungu, iliyotolewa na Musa mtumishi wa Mungu, na kuzingatia na kutii amri zote za Bwana Mungu wetu na hukumu zake na sheria zake.
they joined together with their brothers, their nobles, and bound themselves with both a curse and an oath to walk in God's law, which was given by Moses the servant of God, and to observe and obey all the commandments of Yahweh our Lord and his decrees and his statutes.
30 Tuliahidi kuwa hatuwezi kuwapa binti zetu watu wa nchi au kuchukua binti zao kwa wana wetu.
We promised that we would not give our daughters to the people of the land or take their daughters for our sons.
31 Pia tuliahidi kwamba ikiwa watu wa nchi wataleta bidhaa au nafaka yoyote ya kuuza siku ya Sabato, hatuwezi kununua kutoka kwao siku ya Sabato au siku yoyote takatifu. Kila mwaka wa saba tutaacha mashamba yetu kupumzika, na tutafuta madeni yote yaliyotokana na Wayahudi wengine.
We also promised that if the people of the land bring goods or any grain to sell on the Sabbath day, we would not buy from them on the Sabbath or on any holy day. Every seventh year we will let our fields rest, and we will cancel all debts.
32 Tulikubali amri za kutoa shilingi ya shekeli kila mwaka kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu wetu,
We accepted the commands to give a third of a shekel each year for the service of the house of our God,
33 kutoa mkate wa uwepo, na sadaka ya nafaka ya kawaida, sadaka za kuteketezwa siku za Sabato, sikukuu mpya za mwezi na sikukuu za kuteketezwa, na sadaka takatifu, na sadaka za dhambi za kufanya upatanisho kwa Israeli, pamoja na kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.
to provide for the bread of the presence, and for the regular grain offering, the burnt offerings on the Sabbaths, the new moon festivals and appointed feasts, and for the holy offerings, and for the sin offerings to make atonement for Israel, as well as for all the work of the house of our God.
34 Na makuhani, Walawi, na watu wakapiga kura kwa ajili ya sadaka ya kuni. Kura ilichagua ni nani wa familia zetu ataleta kuni ndani ya nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati zilizowekwa kila mwaka. Kuni hizo zilichomwa juu ya madhabahu ya Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika sheria.
The priests, the Levites, and the people cast lots for the wood offering. The lots would select which of our families would bring wood into the house of our God at the appointed times each year, to be burned on the altar of Yahweh our God, as it is written in the law.
35 Tuliahidi kuleta nyumbani kwa Bwana matunda ya kwanza yaliyotokana na udongo wetu, na matunda ya kwanza ya mti kila mwaka.
We promised to bring to the house of Yahweh the firstfruits grown from our soil, and the firstfruits of every tree each year.
36 Na kama ilivyoandikwa katika sheria, tuliahidi kuleta nyumbani kwa Mungu na kwa makuhani watumikao hapo wazaliwa wa kwanza wa wana wetu ma wanyama wetu.
As it is written in the law, we promised to bring to the house of God and to the priests who serve there, the firstborn of our sons and of our herds and flocks.
37 Tutaleta unga wa kwanza na sadaka zetu za nafaka, na matunda ya kila mti, na divai mpya na mafuta tutaleta kwa makuhani, kwenye vyumba vya kuhifadhi vya nyumba ya Mungu wetu. Tutawaletea Walawi sehemu ya kumi kutoka kwenye udongo wetu kwa sababu Walawi hukusanya zaka katika miji yote tunayofanya kazi.
We will bring the first of our dough and our grain offerings, and the fruit of every tree, and the new wine and the oil we will bring to the priests, to the storerooms of the house of our God. We will bring to the Levites the tithes from our soil because the Levites collect the tithes in all the towns where we work.
38 Kuhani, mzao wa Haruni, lazima awe na Walawi wakati wanapopokea zaka. Walawi wanapaswa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu kwenye vyumba vya kuhifadhi hazima.
A priest, a descendant of Aaron, must be with the Levites when they receive the tithes. The Levites must bring a tenth of the tithes to the house of our God to the storerooms of the treasury.
39 Kwa maana wana wa Israeli na wana wa Lawi, wataleta sadaka za nafaka, divai mpya, na mafuta katika vyumba vya kuhifadhi ambapo vitu vya patakatifu vinasimamishwa, na mahali pa makuhani watumishi, na walinzi wa mlango, na waimbaji. Hatuwezi kuacha nyumba ya Mungu wetu.
For the people of Israel and the descendants of Levi are to bring the contributions of grain, new wine, and oil to the storerooms where the articles of the sanctuary are kept and where the priests who are serving, and the gatekeepers, and the singers stay. We will not neglect the house of our God.