< Nahumu 2 >

1 Yule ambaye atakuharibu vipande vipande anakuja dhidi yako. Linda kuta za mji, linda barabara, jitieni nguvu ninyi wenyewe, yakusanyeni majeshi yenu.
尼尼微啊,那打碎邦國的上來攻擊你。 你要看守保障,謹防道路, 使腰強壯,大大勉力。 (
2 Maana Yehova anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli, ingawa wateka nyara waliwaharibu na kuharibu matawi ya zabibu zao.
耶和華復興雅各的榮華, 好像以色列的榮華一樣; 因為使地空虛的, 已經使雅各和以色列空虛, 將他們的葡萄枝毀壞了。)
3 Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, na watu hodari wamevaa nguo nyekundu; magari ya vita yameandaliwa yanang'ara kwenye vyuma vyake wakati wa mchana, na mikuki ya mivinje inarushwa hewani.
他勇士的盾牌是紅的, 精兵都穿朱紅衣服。 在他預備爭戰的日子, 戰車上的鋼鐵閃爍如火, 柏木把的槍也掄起來了。
4 Magari ya vita yapo kasi kwenye mitaa; yanakimbia mbele na nyuma katika mitaa. Yapo kama kurunzi, na yanakimbia kama radi.
車輛在街上急行, 在寬闊處奔來奔去, 形狀如火把, 飛跑如閃電。
5 Yule ambaye atakuvunja vipande vipande anawaita maafisa wake; wanajikwaa kila mmoja kwa mwingine katika kutembea kwao; wanaharakisha kuushambulia ukuta wa mji. Ngao kubwa imetayarishwa kujikinga na hawa washambuliaji.
尼尼微王招聚他的貴冑; 他們步行絆跌, 速上城牆,預備擋牌。
6 Malango kwenye mito yamelazishwa kufunguka, na jumba la mfalme linaanguka kwenye uharibifu.
河閘開放,宮殿沖沒。
7 Husabu amevuliwa mavazi yake na amachukuliwa; watumishi wake wa kike wanaomboleza kama njiwa, wanavipiga vifua vyao.
王后蒙羞,被人擄去; 宮女搥胸,哀鳴如鴿。 此乃命定之事。
8 Ninawi ni kama bwawa la maji linalovuja, watu wake kwa pamoja wanakimbia kama maji yanayotiririka. Wengine wanasema, “Simama, simama,” lakini hakuna anayegeuka nyuma.
尼尼微自古以來充滿人民, 如同聚水的池子; 現在居民卻都逃跑。 雖有人呼喊說:站住!站住! 卻無人回顧。
9 Chukua nyara ya fedha, kuchua nyara ya dhahabu, maana hakuna mwisho wake, kwa fahari ya vitu vyote vizuri vya Ninawi.
你們搶掠金銀吧! 因為所積蓄的無窮, 華美的寶器無數。
10 Ninawi ipo tupu na imeharibiwa. Moyo wa kila mtu unayeyuka, magoti ya kila mmoja yanagongana pamoja, na uchungu upo kwa kila mmoja; sura zao wote zimepauka.
尼尼微現在空虛荒涼, 人心消化,雙膝相碰, 腰都疼痛,臉都變色。
11 Sasa liko wapi pango la simba, sehemu ambapo simba wadogo hula chakula, sehemu ambapo simba dume na simba jike walitembea, pamoja wana-simba, ambapo hawakuogopa kitu chochote?
獅子的洞和少壯獅子餵養之處在哪裏呢? 公獅母獅小獅遊行、無人驚嚇之地在哪裏呢?
12 Simba alirarua mawindo yake vipande vipande kwa ajili ya watoto wake; aliwanyonga mawindo wake kwa ajili ya wake zake, na kulijaza pango lake mawindo, makao yake kwa mizoga iliyoraruliwa.
公獅為小獅撕碎許多食物, 為母獅掐死活物, 把撕碎的、掐死的充滿牠的洞穴。
13 “Tazama, mimi nipo kinyume na wewe- hili ni neno la Yehova wa majeshi. Nitayachoma magari yenu ya vita katika moshi, na upanga utateketeza simba wenu vijana. Nitazuia nyara zenu kutoka kwenye nchi yangu, na sauti za wajumbe wenu hazitasikika tena.”
萬軍之耶和華說:「我與你為敵,必將你的車輛焚燒成煙,刀劍也必吞滅你的少壯獅子。我必從地上除滅你所撕碎的,你使者的聲音必不再聽見。」

< Nahumu 2 >