< Mathayo 27 >

1 Muda wa asubuhi ulipofika, wakuu wote wa makuhani na wazee wa watu walikula njama dhidi ya Yesu wapate kumuua.
夜明けになりて、凡ての祭司長・民の長老ら、イエスを殺さんと相 議り、
2 Walimfunga, walimwongoza, na kumfikisha kwa Liwali Pilato.
遂に之を縛り、曳きゆきて總督ピラトに付せり。
3 Kisha wakati Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti, aliona kwamba Yesu amekwisha kuhukumiwa, alijuta na kurudisha vipande thelathini vya fedha kwa mkuu wa makuhani na wazee,
ここにイエスを賣りしユダ、その死に定められ給ひしを見て悔い、祭司長・長老らに、かの三十の銀をかへして言ふ、
4 na akasema, “Nimefanya dhambi kwa kuisaliti damu isiyo na hatia.” Lakini wakajibu, “Inatuhusu nini sisi? Yaangalie hayo mwenyewe.”
『われ罪なきの血を賣りて罪を犯したり』彼らいふ『われら何ぞ干らん、汝みづから當るべし』
5 Kisha alivirusha chini vile vipande vya fedha katika hekalu, na kuondoka zake na kujinyonga mwenyewe.
彼その銀を聖所に投げすてて去り、ゆきて自ら縊れたり。
6 Mkuu wa makuhani alivichukua vile vipande vya fedha na kusema, “Si halali kuiweka fedha hii katika hazina, kwa sababu ni gharama ya damu.”
祭司長らその銀をとりて言ふ『これは血の價なれば、宮の庫に納むるは可からず』
7 Walijadiliana kwa pamoja na fedha ikatumika kununulia shamba la mfinyazi la kuzika wageni.
かくて相 議り、その銀をもて陶工の畑を買ひ、旅人らの墓地とせり。
8 Kwa sababu hii shamba hilo limekuwa likiitwa, “Shamba la damu” hadi leo hii.
之によりて其の畑は、今に至るまで血の畑と稱へらる。
9 Kisha lile neno lililokuwa limenenwa na nabii Yeremia lilitimia, kusema, “Walitwaa vipande thelathini vya fedha, gharama iliyopangwa na watu wa Israel kwa ajili yake,
ここに預言者エレミヤによりて云はれたる言は成就したり。曰く『かくて彼ら値積られしもの、即ちイスラエルの子らが値積りし者の價の銀 三十をとりて、
10 na waliitumia kwa shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyokuwa amenielekeza.”
陶工の畑の代に之を與へたり。主の我に命じ給ひし如し』
11 Sasa Yesu alisimama mbele ya liwali, na liwali akamwuliza, “Je! Wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu alimjibu, “Wewe wasema hivyo.”
さてイエス、總督の前に立ち給ひしに、總督 問ひて言ふ『なんぢはユダヤ人の王なるか』イエス言ひ給ふ『なんぢの言ふが如し』
12 Lakini wakati aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu chochote.
祭司長・長老ら訴ふれども、何をも答へ給はず。
13 Kisha Pilato alimwambia, “Hujayasikia mashitaka yote dhidi yako?”
ここにピラト彼に言ふ『聞かぬか、彼らが汝に對して如何におほくの證據を立つるを』
14 Lakini hakumjibu hata neno moja, hivyo liwali alijawa na mshangao.
されど總督の甚く怪しむまで、一言をも答へ給はず。
15 Sasa katika sikukuu ilikuwa desturi ya liwali kumfungua mfungwa mmoja anayechaguliwa na umati.
祭の時には、總督 群衆の望にまかせて、囚人 一人を之に赦す例あり。
16 Wakati huo walikuwa na mfungwa sugu jina lake Baraba.
ここにバラバといふ隱れなき囚人あり。
17 Hivyo wakati walipokuwa wamekusanyika pamoja, Pilato aliwauliza, “Ni nani mnataka tumfungue kwa ajili yenu?” Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?”
されば人々の集れる時、ピラト言ふ『なんぢら我が誰を赦さんことを願ふか。バラバなるか、キリストと稱ふるイエスなるか』
18 Kwa sababu alijua kwamba wamekwisha kumkamata kwa sababu ya chuki.
これピラト彼らのイエスを付ししは嫉に因ると知る故なり。
19 Wakati alipokuwa akiketi kwenye kiti chake cha hukumu, mke wake alimtumia neno na kusema, “Usitende jambo lolote kwa mtu huyo asiye na hatia. Kwani nimeteswa mno hata leo katika ndoto kwa sababu yake.”
彼なほ審判の座にをる時、その妻、人を遣して言はしむ『かの義人に係ることを爲な、我けふ夢の中にて彼の故にさまざま苦しめり』
20 Ndipo wakuu wa makuhani na wazee waliwashawishi makutano wamwombe Baraba, na Yesu auawe.
祭司長・長老ら、群衆にバラバの赦されん事を請はしめ、イエスを亡さんことを勸む。
21 Liwali aliwauliza, “Ni yupi kati ya wawili mnataka mimi nimwachie kwenu?” Walisema, “Baraba.”
總督こたへて彼らに言ふ『二人の中いづれを我が赦さん事を願ふか』彼らいふ『バラバなり』
22 Pilato akawaambia, “Nimtendee nini Yesu anayeitwa Kristo?” Wote wakajibu, “Msulibishe”
ピラト言ふ『さらばキリストと稱ふるイエスを我いかにすべきか』皆いふ『十字架につくべし』
23 Naye akasema, “Kwa nini, ni kosa gani ametenda?” Lakini walizidi kupaza sauti hata juu mno, “Msulibishe.”
ピラト言ふ『かれ何の惡事をなしたるか』彼ら烈しく叫びていふ『十字架につくべし』
24 Hivyo wakati Pilato alipoona hawezi kufanya lolote, lakini badala yake vurugu zilikuwa zimeanza, alitwaa maji akanawa mikono yake mbele ya umati, na kusema, “Mimi sina hatia juu ya damu ya mtu huyu asiye na hatia. Yaangalieni haya wenyewe.”
ピラトは何の效なく反つて亂にならんとするを見て、水をとり群衆のまへに手を洗ひて言ふ『この人の血につきて我は罪なし、汝 等みづから當れ』
25 Watu wote wakasema, “Damu yake iwe juu yetu na watoto wetu.”
民みな答へて言ふ『其の血は、我らと我らの子孫とに歸すべし』
26 Kisha akamfungulia Baraba kwao, lakini alimpiga mijeredi Yesu na kumkabidhi kwao kwenda kusulibiwa.
ここにピラト、バラバを彼らに赦し、イエスを鞭うちて、十字架につくる爲に付せり。
27 Kisha askari wa liwali wakamchukua Yesu mpaka Praitorio na kundi kubwa la maaskari wote wakamkusanyika.
ここに總督の兵卒ども、イエスを官邸につれゆき、全 隊を御許に集め、
28 Wakamvua nguo zake na kumvika kanzu ya rangi nyekundu.
その衣をはぎて、緋色の上衣をきせ、
29 Kisha wakatengeneza taji ya miiba na kuiweka juu ya kichwa chake, na walimwekea mwanzi katika mkono wake wa kuume. Walipiga magoti mbele yake na kumkejeri, wakisema, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi?”
茨の冠冕を編みて、その首に冠らせ、葦を右の手にもたせ、且その前に跪づき、嘲弄して言ふ『ユダヤ人の王、安かれ』
30 Na walimtemea mate, na walitwaa mwanzi na kumpiga kichwani.
また之に唾し、かの葦をとりて其の首を叩く。
31 Wakati walipokuwa wakimkejeri, walimvua ile kanzu na kumvika nguo zake, na kumwongoza kwenda kumsulibisha.
かく嘲弄してのち、上衣を剥ぎて、故の衣をきせ、十字架につけんとて曳きゆく。
32 Walipotoka nje, walimwona mtu kutoka Krene jina lake Simeoni, ambaye walimlazimisha kwenda nao ili apate kuubeba msalaba wake.
その出づる時、シモンといふクレネ人にあひしかば、強ひて之にイエスの十字架をおはしむ。
33 Walipofika mahali paitwapo Galigotha, maana yake, “Eneo la fuvu la Kichwa.”
かくてゴルゴタといふ處、即ち髑髏の地にいたり、
34 Walimpa siki iliyochanganywa na nyongo anywe. Lakini alipoionja, hakuweza kuinywa.
苦味を混ぜたる葡萄酒を飮ませんとしたるに、嘗めて、飮まんとし給はず。
35 Wakati walipokuwa wamemsulibisha, waligawana mavazi yake kwa kupiga kura.
彼らイエスを十字架につけてのち、籤をひきて其の衣をわかち、
36 Na waliketi na kumwangalia.
且そこに坐して、イエスを守る。
37 Juu ya kichwa chake waliweka mashitaka dhidi yake yakisomeka, “Huyu ni Yesu, mfalme wa Wayahudi.”
その首の上に『これはユダヤ人の王イエスなり』と記したる罪標を置きたり。
38 Wanyang'anyi wawili walisulibiwa pamoja naye, mmoja upande wa kulia wake na mwingine wa kushoto.
ここにイエスとともに二人の強盜、十字架につけられ、一人はその右に、一人はその左におかる。
39 Wale waliokuwa wakipita walimdhihaki, wakitikisa vichwa vyao
往來の者どもイエスを譏り、首を振りていふ、
40 na kusema, “Wewe uliyekuwa unataka kuliharibu hekalu na kulijenga katika siku tatu, jiokoe mwenyewe! Kama ni Mwana wa Mungu, shuka chini utoke msalabani!”
『宮を毀ちて三日のうちに建つる者よ、もし神の子ならば己を救へ、十字架より下りよ』
41 Katika hali ile ile wakuu wa makuhani walikuwa wakimkashifu, pamoja na waandishi na wazee, na kusema,
祭司長らもまた同じく、學者・長老らとともに嘲弄して言ふ、
42 “Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi. Na ashuke chini toka msalabani, ndipo tutakapomwamini.
『人を救ひて己を救ふこと能はず。彼はイスラエルの王なり、いま十字架より下りよかし、さらば我ら彼を信ぜん。
43 Alimtumaini Mungu. Acha Mungu amwokoe sasa kama anataka, kwa sababu alisema, 'Mimi ni Mwana wa Mungu.'”
彼は神に依り頼めり、神かれを愛しまば今すくひ給ふべし「我は神の子なり」と云へり』
44 Na wale wanyang'anyi waliokuwa wamesulibiwa pamoja naye pia walisema maneno ya kumdhihaki.
ともに十字架につけられたる強盜どもも、同じ事をもてイエスを罵れり。
45 Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa.
晝の十二 時より地の上あまねく暗くなりて、三時に及ぶ。
46 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama thabakithan?” akimaanisha, “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”
三時ごろイエス大聲に叫びて『エリ、エリ、レマ、サバクタニ』と言ひ給ふ。わが神、わが神、なんぞ我を見 棄て給ひしとの意なり。
47 Wakati huo baadhi yao waliokuwa wamesimama pale walisikia, wakasema, “Anamwita Eliya.”
そこに立つ者のうち或 人々これを聞きて『彼はエリヤを呼ぶなり』と言ふ。
48 Mara moja mmoja wao alikimbia kuchukua sifongo na kuijaza kinywaji kichungu, akaiweka juu ya mti na kumpa apate kunywa.
直ちにその中の一人はしりゆきて海綿をとり、酸き葡萄酒を含ませ、葦につけてイエスに飮ましむ。
49 Nao waliosalia wakasema, “Mwacheni peke yake, acheni tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.”
その他の者ども言ふ『まて、エリヤ來りて彼を救ふや否や、我ら之を見ん』
50 Kisha Yesu akalia tena kwa sauti kuu na akaitoa roho yake.
イエス再び大聲に呼はりて息 絶えたまふ。
51 Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande.
視よ、聖所の幕、上より下まで裂けて二つとなり、また地震ひ、磐さけ、
52 Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa.
墓ひらけて、眠りたる聖徒の屍體おほく活きかへり、
53 Walitoka kwenye makaburi baada ya ufufuo wake, waliingia mji mtakatifu, na wakaonekana na wengi.
イエスの復活ののち墓をいで、聖なる都に入りて、多くの人に現れたり。
54 Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, “Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”
百卒長および之と共にイエスを守りゐたる者ども、地震とその有りし事とを見て甚く懼れ『實に彼は神の子なりき』と言へり。
55 Wanawake wengi waliokuwa wakimfuata Yesu kutoka Galilaya ili kumhudumia walikuwa pale wakitazama kutoka kwa mbali.
その處にて遙に望みゐたる多くの女あり、イエスに事へてガリラヤより從ひ來りし者どもなり。
56 Miongini mwao walikuwa Mariamu Magdarena, Mariamu mama yake Yakobo na Joseph, na mama wa watoto wa Zebedayo
その中には、マグダラのマリヤ、ヤコブとヨセフとの母マリヤ、及びゼベダイの子らの母などもゐたり。
57 Ilipofika jioni, alikuja mtu tajiri kutoka Arimathayo, aliyeitwa Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.
日 暮れて、ヨセフと云ふアリマタヤの富める人きたる。彼もイエスの弟子なるが、
58 Alimwendea Pilato na kuuomba mwili wa Yesu. Kisha Pilato aliagiza apate kupewa.
ピラトに往きてイエスの屍體を請ふ。ここにピラト之を付すことを命ず。
59 Yusufu aliuchukua mwili akaufunga na nguo ya sufi safi,
ヨセフ屍體をとりて淨き亞麻 布につつみ、
60 na akaulaza katika kaburi jipya lake alilokuwa amelichonga mwambani. Kisha akavingirisha jiwe kubwa likafunika mlango wa kaburi na akaenda zake.
岩にほりたる己が新しき墓に納め、墓の入口に大なる石を轉しおきて去りぬ。
61 Mariamu Magdalena na Mariamu mwingine walikuwa pale, wamekaa kuelekea kaburi.
其處にはマグダラのマリヤと他のマリヤと墓に向ひて坐しゐたり。
62 Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku baada ya maandalio, wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikusanyika pamoja kwa Pilato.
あくる日、即ち準備 日の翌日、祭司長らとパリサイ人らとピラトの許に集りて言ふ、
63 Wakamwambia, “Bwana, tunakumbuka kuwa wakati yule mdanganyifu alipokuwa hai, alisema, 'Baada ya siku tatu atafufuka tena.'
『主よ、かの惑すもの生き居りし時「われ三日の後に甦へらん」と言ひしを、我ら思ひいだせり。
64 Kwahiyo, agiza kwamba kaburi lilindwe salama mpaka siku ya tatu. Vinginevyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kumwiba na kusema kwa watu, 'Amefufuka kutoka wafu.' Na udanganyifu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”
されば命じて三日に至るまで墓を固めしめ給へ、恐らくはその弟子ら來りて之を盜み、「彼は死人の中より甦へれり」と民に言はん。然らば後の惑は前のよりも甚だしからん』
65 Pilato akawaambia, “Chukueni walinzi. Nendeni mkafanye hali ya usalama kama muwezavyo.”
ピラト言ふ『なんぢらに番兵あり、往きて力 限り固めよ』
66 Hivyo walikwenda na kufanya kaburi kuwa salama, jiwe liligongwa mhuri na kuweka walinzi.
乃ち彼らゆきて石に封印し、番兵を置きて墓を固めたり。

< Mathayo 27 >