< Mathayo 22 >

1 Yesu alisema nao tena katika mifano, akisema,
And Jesus resuming his discourse spake unto them again in parables,
2 “Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme aliyeandaa sherehe ya harusi ya mwanawe.
saying, The kingdom of heaven is like a certain king, who made a wedding-feast for his son;
3 Akawatuma watumishi wake kuwakaribisha waliokuwa wamealikwa kuja katika sherehe ya harusi, lakini hawakufika.
and sent his servants to call those that were invited to the wedding: and they would not come.
4 Mfalme aliwatuma tena watumishi wengine, akisema. “Waambieni wote walioalikwa, Angalieni, nimeandaa chakula. Fahali na ndama wangu wanono wamechinjwa, na mambo yote yako tayari, Njoni katika sherehe ya harusi.”
Then he sent other servants, saying, Tell them that are invited, I have prepared my dinner, my oxen and my fatlings are killed, and all things are ready; come to the wedding.
5 Lakini watu hao hawakuzingatia kwa dhati mwaliko wake. Baadhi walirejea katika mashamba yao, na wengine walirudi katika sehemu zao za biashara.
But they slighted him, and went away, one to his field and another to his merchandize:
6 Wengine waliwainukia watumishi wa mfalme na kuwadharirisha na kuwaua.
and others seized his servants, and shamefully abused them, and slew them.
7 Lakini mfalme alikasirika. Alituma jeshi lake, akawaua wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.
And when the king heard of it, he was highly provoked, and sent his troops, and destroyed those murderers, and burnt their city.
8 Kisha aliwaambia watumishi wake, “Harusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakustahili.
Then saith he to his servants, The feast is ready, but they that were invited were not worthy of it:
9 Kwa hiyo nendeni kwenye makutano ya njia kuu, waalikeni watu wengi kadri iwezekanavyo waje kwenye sherehe ya harusi.”
go therefore into the public streets, and as many as ye meet with invite to the wedding.
10 Watumishi walienda njia kuu na kuwakaribisha watu wowote waliowaona, wema na wabaya. Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa wageni.
And those servants went out into the high-ways, and brought in all they met with, both bad and good: and the wedding was filled with guests.
11 Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi!
But when the king came in to look at the guests, he saw there a man that had not put on a wedding-garment, and saith to him,
12 Mfalme alimwuliza, 'Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?' Na mtu huyo hakujibu chochote.
Friend, how camest thou in here without a wedding-garment? and he was struck speechless.
13 Ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake, “Mfungeni mtu huyu mikono na miguu na mtupeni nje katika giza, huko ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
Then said the king to his attendants, Bind him hand and foot, and take him up, and throw him out into the darkness; there shall be weeping and gnashing of the teeth:
14 Kwa kuwa watu wengi wanaitwa, lakini wateule ni wachache.”
for there are many called, but few approved.
15 Ndipo Mafarisayo waliondoka na kupanga jinsi ya kumkamata Yesu katika maneno yake mwenyewe.
Then the pharisees went and consulted how they might insnare Him in his discourse.
16 Ndipo walipowatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode. Na walimwambia Yesu, “Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mtu wa kweli, na kwamba unafundisha matakwa ya Mungu katika ukweli. Haujali maoni ya mtu mwingine na hauoneshi upendeleo kwa watu.
And they send to Him their disciples along with the Herodians, saying, Master, we know that thou art a man of truth, and teachest the way of God in truth, neither carest for any man; for thou regardest not the person of men: Tell us therefore what thou thinkest,
17 Kwa hiyo tuambie, unafikiri nini? Je, ni sahihi kisheria kulipa kodi kwa Kaisari au hapana?”
Is it lawful to give tribute to Cesar, or not?
18 Yesu alifahamu uovu wao na akasema, “Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki?
But Jesus knew their malice, and said, Why do ye tempt me, ye hypocrites?
19 Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi.” Ndipo wakamletea dinari.
Shew me the tribute-money. And they brought Him a Roman Penny.
20 Yesu akawauliza, “Sura na jina hili ni vya nani?”
And He saith unto them, Whose image and inscription is this?
21 Wakamjibu, “Vya Kaisari.” Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu.”
They answered, Cesar's. Then saith He unto them, Render therefore to Cesar the things that are Cesar's; and to God the things that are God's.
22 Waliposikia hivyo walishangaa. Kisha walimwacha na kwenda zao.
And when they heard this, they marvelled, and left Him and went away.
23 Siku hiyo baadhi ya Masadukayo walikuja kwa Yesu, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu. Wakamwuliza,
On the same day came the sadducees to Him, who say there is no resurrection,
24 wakisema, “Mwalimu, Musa alisema, Ikiwa mtu amefariki bila kuzaa watoto, ndugu yake na amrithi huyo mwanamke na ampatie mtoto kwa ajili ya ndugu yake.
and asked Him, saying, Master, Moses said, If any man die, having no children, his brother shall marry his wife and raise up seed unto his brother.
25 Walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa na kisha akafariki bila kuzaa watoto. Akamwachia mke nduguye.
Now there were with us seven brothers, and the first married and died, and having no issue left his wife to his brother;
26 Kisha ndugu yake wa pili naye akafanya vivyo hivyo, kisha yule wa tatu, ikawa hivyo hadi kwa yule wa saba.
likewise the second also, and the third, even to seven;
27 Baada ya kufanya hivyo wote, yule mwanamke naye alifariki.
and last of all the woman died also;
28 Sasa katika ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani katika ndugu hao saba? Kwa sababu wote walimuoa.”
therefore in the resurrection whose wife shall she be of the seven? for they all had her.
29 Lakina Yesu aliwajibu na kuwaambia, “Mnakosea, kwa sababu hamjui Maandiko wala nguvu za Mungu.
But Jesus answered them, Ye are mistaken, not knowing the scriptures nor the power of God:
30 Kwa kuwa katika ufufuo, watu hawaoi wala kuolewa. Badala yake watu huwa kama malaika huko mbinguni.
for in the resurrection they neither marry nor are given in marriage; but are as the angels of God in heaven.
31 Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjawahi kusoma kile ambacho Mungu alikisema kwenu, akisema,
But concerning the resurrection of the dead, have ye not read what is spoken to you by God,
32 Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.”
saying, I am the God of Abraham, and the God of Isaac, and the God of Jacob? God is not the God of the dead, but of the living.
33 Wakati kusanyiko waliposikia hili, waliyashangaa mafundisho yake.
And when the people heard this, they were astonished at his doctrine.
34 Lakini Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewanyamazisha Masadukayo, walijikusanya wao wenyewe kwa pamoja.
But when the pharisees heard that He had silenced the sadducees,
35 Mmoja wao, akiwa mwana sheria, alimwuliza swali kwa kumjaribu.
they gathered together again, and one of them, an interpreter of the law, propounded a question, to try Him,
36 “Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote katika sheria?”
and said, Master, which is the greatest commandment in the law?
37 Yesu akamjibu, “Lazima umpende Bwana kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
And Jesus said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind: this is the first and great command.
38 Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza.
And the second is like it,
39 Na ya pili inafanana na hiyo- Ni lazima kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
Thou shalt love thy neighbour as thyself.
40 Sheria zote na Manabii hutegemea amri hizi mbili.”
On these two precepts depend all the law and the prophets.
41 Na Mafarisayo walipokuwa bado wamejikusanya pamoja, Yesu aliwauliza swali.
Now while the pharisees were thus gathered together, Jesus asked them,
42 Akisema, “J! e, Mwafikiri nini juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?” Nao wakamjibu, “Ni mwana wa Daudi.”
saying, What think ye of the Messiah? whose son is He? They say unto Him, David's.
43 Yesu akawajibu, “Ni kwa namna gani Daudi katika Roho anamwita Bwana, akisema,
He saith unto them, How then does David by inspiration call Him Lord,
44 'Bwana alimwambia Bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya maadui zako wawekwe chini ya miguu yako.”'?”
saying, The Lord said unto my Lord, "Sit thou on my right hand, till I make thine enemies thy footstool?"
45 Kama Daudi anamwita Kristo “Bwana,” jinsi gani atakuwa mtoto wake?”
therefore if David call Him Lord, how is He his son?
46 Hakuna aliyeweza kumjibu neno tena, na hakuna aliyethubutu tena kumwuliza maswali zaidi tangu siku hiyo na kuendelea.
And no one was able to answer Him a word, nor did any dare, from that day, to ask Him any more such questions.

< Mathayo 22 >