< Mathayo 21 >
1 Yesu na wanafunzi wake wakafika karibu na Jerusalemu na wakaenda mpaka Bethfage, katika mlima mizeituni, kisha Yesu akawatuma wanafunzi wawili,
們臨近耶路撒冷,來到靠近橄欖山的貝特法革時,耶穌就打發兩個門徒,
2 akiwaambia, “Nendeni katika kijiji kinachofuata, na mara moja mtamkuta punda amefungwa pale, na mwanapunda pamoja naye. wafungueni na kuwaleta kwangu.
對他們說:「你們往對面的村莊裏去,立時會看見一匹栓的母驢,和跟牠在一起的驢駒。解開,給我牽來,
3 Ikiwa mtu yeyote akiwaambia chochote kuhusu hilo, mtasema, `Bwana anawahitaji, ` na mtu huyo mara moja atawaruhusu mje pamoja nao”
如果有人對你們說什麼,你們就說:主要用牠們。他們就會立刻放牠們來」
4 Jambo hili lilitokea ni lile lililosemwa kupitia kwa nabii lazima litimizwe. Akawaambia,
這事發生,是為應驗先知所說的:
5 Waambie binti Sayuni, tazama, mfalme wako anakuja kwenu, mnyenyekevu na akiwa amempanda punda, na mwana punda mme, mwana punda mchanga.
「你們應向熙雍女子說:看,你的君王來到你這裏,溫和地騎在一匹驢上,一匹母驢的小驢駒上。」
6 Kisha wanafunzi waliondoka na kufanya kama Yesu alivyowaagiza.
門徒就去,焄耶穌吩咐他們的做了。
7 Wakamleta punda na mwanapunda, na kuweka nguo zao juu yao, naye Yesu akakaa pale.
他們牽了母驢和驢來,把外衣搭在牠們的身上,扶耶穌坐在上面。
8 Wengi katika mkusanyiko walitandaza nguo zao njiani, na wengine walikata matawi kutoka kwenye miti na kutandaza barabarani.
很多群眾,自己的外衣舖在地上,還有些人從樹上砍下樹枝來,撒在路上。
9 Umati uliomtangulia Yesu na wale waliomfuata walipaza sauti, wakisema,”Hosana kwa mwana wa Daudi! Ni mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. Hosana juu zaidi!”
前行後隨的群眾喊說:「賀三納於達味之子!因上主之名而來的,當受讚頌!賀三納於至上之天。」
10 Yesu alipofika Yerusalemu, mji mzima ulishtuka na kusema, “Huyu ni nani?
當耶穌進入耶路撒冷的時候,全城哄動,說:「這人是誰? 」
11 “Umati ulijibu, “Huyu ni Yesu Nabii, kutoka Nazareti ya Galilaya.”
群眾說:「這是加利肋亞納匝肋的先知耶穌。」
12 Kisha Yesu akaingia katika hekalu la Mungu. akawafukuza nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wauza njiwa.
耶穌進了聖殿,把一切在聖殿內的商人顧客趕出去,把錢莊的桌子和賣鴿子的凳子推翻
13 Akawaambia, “Imeandikwa, `'Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi, `lakini ninyi mmeifanya pango la wanyang`anyi.”
向他們說:「經上記載:『我的殿宇,因稱為祈禱之所。』你們竟把它做成了賊窩。」
14 kisha vipofu na vilema wakamjia hekaluni, naye akawaponya.
在聖殿仕的瞎子和瘸子來到衪跟前,衪都治好了他們。
15 Lakini wakati wakuu wa makuhani na waandishi walipoona maajabu aliyoyatenda, na waliposikia watoto wakipiga kelele hekaluni na kusema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi,” walishikwa na hasira.
司祭長及經師見了衪所行的奇事,又聽見了孩子們在聖殿內喊說:「賀三納於達味之子!」就大發忿怒,
16 Wakamwambia, “Umesikia kile kinachosemwa na hawa watu?” Yesu akawaambia, “Ndiyo! Lakini hamjawahi kusoma, 'Kutoka kwa midomo ya watoto na watoto wachanga wanyonyao mna sifa kamili?''
對耶穌說:「你聽見他們所說的嗎!」耶穌對他們說:「是的,你們從未讀過:『你由嬰兒和吃奶者的口中,備受讚美』這句話嗎? 」
17 Kisha Yesu akawaacha na kwenda nje ya mji katika Bethania na kulala huko.
於是便離開他們走出城外,到伯達尼去,在那裏過夜。
18 Asubuhi alipokuwa anarudi mjini, alikuwa na njaa.
早晨,衪回城時,餓了,
19 Aliona mtini kandokando ya barabara. Akauendea, lakini hakupata kitu juu yake isipokuwa majani. Aliuambia, “Kusiwe na matunda kwako daima tena.” Na mara hiyo mtini ule ukanyauka. (aiōn )
見路旁有棵無花樹,就走到跟前,但在樹上除了葉子外,什麼也沒找到,就對它說:「你永遠不再結果子了!」那無花果樹立即枯乾了。 (aiōn )
20 Wanafunzi walipoona, wakastaajabu na kusema, “Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?”
門徒一見就驚異說:「怎麼這無花果樹立即枯乾了?」
21 Yesu akajibu na kuwaambia, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ` uchukuliwe na ukatupwe baharini, `na itafanyika.
耶穌回答他們說:「我實在告訴你們:你們如果有信德,不疑惑,不但能對無花果樹做這件事,既使你們對這座山說:起來,投到海中!也必要實現。
22 Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea.”
不論你們在祈禱時懇求什麼,只要信,就必獲得。」
23 Yesu alipofika hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamjia wakati alipokuwa akifundisha na kumwuliza, “Ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?”
衪進了聖殿,正教訓人時,司祭長和民間的長老來到衪跟前說:「你憑什麼權柄作這些事? 誰給了你這種權柄? 」
24 Yesu akajibu na kuwaambia, “Nami tena nitawauliza swali moja. kama mkiniambia, nami vilevile nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
耶穌回答說:「我也問你們一句話:你們若答覆我,我就告訴你們:我憑什麼權作這些事。
25 Ubatizo wa Yohana- ulitoka wapi, mbinguni au kwa wanadamu?” Wakahojiana wenyewe, wakisema, tukisema, ulitoka mbinguni, `atatuambia, kwa nini hamkumwamini? `
若翰的洗禮,是從哪裏來的?是從天上來的? 還是從人間來的? 」他們心中思量說:「如果我們說,是從天上來的,衪必對我們說:你們為什麼不信他?
26 Lakini tukisema, `ulitoka kwa wanadamu, `tunawaogopa makutano, kwa sababu wote wanamwona Yohana kama nabii.”
如果我們說:是從人來的,我們害怕民眾,因為眾人都以若翰為一位先知。
27 Kisha wakamjibu Yesu na kusema, “Hatujui” Akawaambia pia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nafanya mambo haya.
他們便耶穌說:「我們不知道。」耶穌也對們們說:「我也不告訴你們:我憑什麼權柄做道些事。
28 Lakini mnafikiri nini? Mtu mwenye wana wawili. Akaenda kwa moja na kumwambia, `Mwanangu, nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu
你們以為怎樣? 從前有一個人,有兩個兒子,他對第一個說:孩子! 你今天到葡萄園裏去工作吧!
29 leo. `Mwana akajibu na kusema, `sitakwenda, ' Lakini baadaye akabadilisha mawazo yake na akaenda.
他回答說:我去。但他卻沒有去。
30 Na Mtu yule akaenda kwa mwana wa pili na kusema kitu kilekile. Mwana huyu akajibu na kusema, `nitakwenda, bwana', lakini hakwenda.
他對第二個也說了同樣的話,第二個卻回答說:我不願意。但後來悔悟過來,而又去了。
31 Yupi kati ya wana wawili aliyefanya matakwa ya baba yake? Wakasema, “Mwana wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla yenu kuingia.
兩人中哪一個履行了夬父親的意願? 」他們說:「後一個。」耶穌對他們說:「我實告訴你們:稅吏和娼妓要在你們以先進入天國,
32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia iliyo nyoofu, lakini hamkumwamini, wakati wakusanya ushuru na makahaba walimwamini. Na ninyi, mlipoona hilo likitendeka, hamkuweza kutubu ili baadaye mumwamini.
因為若翰來到你們道裏履行了正義,你們仍不相信他。稅吏和娼妓倒相信了;至於你們,見了後,仍不悔悟去相信他。」
33 Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu, mtu mwenye eneo kubwa la ardh. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamlia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine.
你們再聽一個比喻吧!從前有一個家主,培植了一個葡萄園,周圍圍上籬笆,園內掘了一個榨酒池,築了一個守望台,把它租給園戶,就離開了本國。
34 Wakati wa mavuno ya mizabibu ulipokaribia, aliwatuma baadhi ya watumishi kwa wakulima wa mizabibu kuchukua mizabibu yake.
快到收果子的時節,他打發僕人到園戶那裏去收果子。
35 Lakini wakulima wa zabibu wakawachukua watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua mwingine, na wakampiga mmoja kwa mawe.
園戶拿住了僕人,將一個鞭打了,將一個殺了,將另一個用石頭砸死了。
36 Kwa mara nyingine, Mmiliki aliwatuma watumishi wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakulima wa mizabibu waliwatendea vilevile.
他再打發一些僕人去,人數比以前還多;園戶也一樣對待了他們,
37 Baada ya hapo bwana yule akamtuma kwao mwana wake, akisema, `'Watamheshimu mwanangu.'`
最後他打發他的兒子到他們那去,說:他們會尊敬我的兒子。
38 Lakini wakulima wa mizabibu walipomwona kijana yule, wakaambizana, `'Huyu ni mrithi, Njooni, tumuue na tumiliki urithi.'
但園戶一看見是兒子,就此說:這是繼承人;來,我們殺掉他,我們就能得到他的產業。
39 `Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumwua.
於是他們拿住他,把他推到園外殺了。
40 Je mmliki wa shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanya nini wakulima wa mizabibu?”
那麼當葡萄園的主人來時,他要怎樣處置那此些園戶呢?」
41 Wakamwambia, “Atawaharibu hao watu waovu katika njia ya ukali zaidi, na kisha atalikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine wa mizabibu, watu ambao watalipa kwa ajili ya mizabibu itakapoiva.”
他們回答說:「要兇惡地消滅那些兇惡的人,把葡萄園另租給按時給他繳納出產的園戶。」
42 Yesu akawaambia, “Hamkusoma katika maandiko, 'Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa Bwana, na inashangaza machoni petu?'
耶穌對他們說:「匠人棄而不用的石頭,反而成了屋角的基石;那是上主的所行所為,在我們眼中,神妙莫測』的這句經文,你們沒有讀過嗎?
43 Hivyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwenu na kupewa taifa linalojali matunda yake.
為此我對你們說:天主的國,必由你們中奪去,而交給果子的外邦人。
44 Yeyote atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjwa vipandevipande. Lakini kwa yeyote litakayemwangukia, litamsaga.”
跌在這石頭上的,必被撞碎;這石頭落在誰身上,必要把他壓踤」
45 Wakuu wa makuhani na mafarisayo waliposikia mifano yake, wakaona kuwa anawazungumzia wao.
司祭長和法利賽人聽了衪的這些比喻,覺出衪是指著他們說的,
46 Lakini kila walipotaka kunyosha mikono juu yake, waliogopa makutano, kwa sababu watu walimtazama kama nabii.
就想逮住衪;但害怕民眾,因為他們以耶穌為一位先知。