< Mathayo 20 >

1 Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mmliki wa shamba, aliyeamka asubuhi na mapema ili kuajiri wafanyakazi katika shamba lake la mizabibu.
천국은 마치 품군을 얻어 포도원에 들여 보내려고 이른 아침에 나간 집 주인과 같으니
2 Baada ya kuwa amekubaliana na wafanyakazi dinari moja kwa kutwa, aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu.
저가 하루 한 데나리온씩 품군들과 약속하여 포도원에 들여 보내고
3 Alienda tena baada ya masaa matatu hivi na aliona wafanyakazi wengine wakiwa wamesimama bila kazi katika eneo la soko.
또 제 삼시에 나가 보니 장터에 놀고 섰는 사람들이 또 있는지라
4 Akawaambia, 'Ninyi pia, nendeni katika shamba la mizabibu, na chochote kilicho halali nitawapa.' Hivyo wakaenda kufanya kazi.
저희에게 이르되 너희도 포도원에 들어가라 내가 너희에게 상당하게 주리라 하니 저희가 가고
5 Akaenda tena baada ya masaa sita na tena katika saa ya tisa, na alifanya hivyo hivyo.
제 육시와 제 구시에 또 나가 그와 같이 하고
6 Mara nyingine tena mnamo saa kumi na moja, alienda na kuwakuta watu wengine wamesimama bila kazi. Aliwaambia, 'kwanini mmesimama hapa bila kazi yoyote kwa siku nzima?
제 십일 시에도 나가 보니 섰는 사람들이 또 있는지라
7 Wakamwambia, kwasababu hakuna mtu yeyote aliyetuajiri. Akawaambia, 'Nanyi ninyi pia nendeni katika shamba la mizabibu.'
가로되 너희는 어찌하여 종일토록 놀고 여기 섰느뇨 가로되 우리를 품군으로 쓰는 이가 없음이니이다 가로되 너희도 포도원에 들어가라 하니라
8 Wakati wa jioni ulipofika, mwenye shamba la mizabibu alimwambia msimamizi wake, 'Waite wafanyakazi na uwalipe mishahara, kwa kuanza na wa mwisho hadi wa kwanza.'
저물매 포도원 주인이 청지기에게 이르되 품군들을 불러 나중 온 자로부터 시작하여 먼저 온 자까지 삯을 주라 하니
9 Walipokuja wale walioajiriwa saa kumi na moja, kila mmoja wao alipokea dinari.
제 십일 시에 온 자들이 와서 한 데나리온씩을 받거늘
10 Walipokuja wafanyakazi wa kwanza, walifikiri kuwa watapokea zaidi, lakini walipokea pia kila mmoja dinari moja kila mtu.
먼저 온 자들이 와서 더 받을 줄 알았더니 저희도 한 데나리온씩 받은지라
11 Baada ya kupokea malipo yao, walimlalamikia mmiliki wa shamba.
받은 후 집 주인을 원망하여 가로되
12 Wakasema, 'Hawa wafanyakazi wa mwisho wametumia saa moja tu katika kufanya kazi, lakini umewalinganisha na sisi, sisi tumebeba mzigo kwa siku nzima na kuungua na joto.'
나중 온 이 사람들은 한 시간만 일하였거늘 저희를 종일 수고와 더위를 견딘 우리와 같게 하였나이다
13 Lakini mwenye shamba akajibu na kusema kwa mmoja wao, 'Rafiki, sikutenda jambo baya. Je! hatukukubaliana na mimi kwa dinari moja?
주인이 그 중의 한사람에게 대답하여 가로되 친구여 내가 네게 잘못한 것이 없노라 네가 나와 한 데나리온의 약속을 하지 아니 하였느냐
14 Pokea kile kilicho halali yako na uende zako. Ni furaha yangu kuwapa hawa wafanyakazi walioajiriwa mwisho sawa sawa na wewe.
네 것이나 가지고 가라 나중 온 이 사람에게 너와 같이 주는 것이 내 뜻이니라
15 Je! Si haki kwangu kufanya kile ninachotaka na mali zangu? Au jicho lako ni ovu kwa sababu mimi ni mwema?
내 것을 가지고 내 뜻대로 할 것이 아니냐 내가 선하므로 네가 악하게 보느냐
16 Hivyo wa mwisho atakuwa kwanza na wa kwanza wa mwisho''
이와 같이 나중 된 자로서 먼저 되고 먼저 된 자로서 나중 되리라
17 Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalem, aliwachukuwa wanafunzi wake kumi na mbili pembeni, na njiani akawaambia,
예수께서 예루살렘으로 올라 가려 하실 때에 열 두 제자를 따로 데리시고 길에서 이르시되
18 ''Tazama tunaelekea Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa katika mikono ya wakuu wa makuhani na waandishi. Watamhukumu kifo
보라, 우리가 예루살렘으로 올라 가노니 인자가 대제사장들과 서기관들에게 넘기우매 저희가 죽이기로 결안하고
19 na watamtoa kwa watu wa mataifa ili kumdhihaki, kumchapa na kumsulibisha. Lakini katika siku ya tatu atafufuka.''
이방인들에게 넘겨 주어 그를 능욕하며 채찍질하며 십자가에 못박게 하리니 제 삼일에 살아나리라
20 Kisha mama wa wana wa Zebedayo alikuja kwa Yesu na wana wake. Alipiga magoti mbele yake na kumwomba kitu kutoka kwake.
그 때에 세베대의 아들의 어미가 그 아들들을 데리고 예수께 와서 절하며 무엇을 구하니
21 Yesu akamwambia, “Unataka nini?” Akamwambia, ''Amuru kuwa hawa wanangu wawili wakae, mmoja mkono wako wa kulia na mmoja mkono wako wa kushoto katika ufalme wako.''
예수께서 가라사대 무엇을 원하느뇨? 가로되 `이 나의 두 아들을 주의 나라에서 하나는 주의 우편에 하나는 주의 좌편에 앉게 명하소서'
22 Lakini Yesu akajibu na kusema, “Haujui kile unachoomba. Je! Unaweza kukinywea kikombe ambacho nitakinywea?” wakamwambia, “Tunaweza.”
예수께서 대답하여 가라사대 너희 구하는 것을 너희가 알지 못하는도다 나의 마시려는 잔을 너희가 마실 수 있느냐? 저희가 말하되 `할 수 있나이다'
23 Akawaambia, “Kikombe changu hakika mtakinywea. Lakini kukaa mkono wangu wa kulia na mkono wangu wa kushoto si jukumu langu kuwapa, lakini ni kwa wale ambao wamekwisha kuandaliwa na Baba yangu.”
가라사대 너희가 과연 내 잔을 마시려니와 내 좌우편에 앉는 것은 나의 줄 것이 아니라 내 아버지께서 누구를 위하여 예비하셨든지 그들이 얻을 것이니라
24 Wanafunzi wengine kumi waliposikia hivyo, wakahuzunishwa sana na wale ndugu wawili.
열 제자가 듣고 그 두 형제에 대하여 분히 여기거늘
25 Lakini Yesu aliwaita mwenyewe na kuwaambia, “Mnafahamu ya kuwa watawala wa mataifa huwatiisha, na wakuu wao hutekeleza mamlaka juu yao.
예수께서 제자들을 불러다가 가라사대 이방인의 집권자들이 저희를 임의로 주관하고 그 대인들이 저희에게 권세를 부리는 줄을 너희가 알거니와
26 Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote atakayetaka kuwa mkubwa miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.
너희 중에는 그렇지 아니하니 너희 중에 누구든지 크고자 하는 자는 너희를 섬기는 자가 되고
27 Na atakaye kuwa wa kwanza miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.
너희 중에 누구든지 으뜸이 되고자 하는 자는 너희 종이 되어야 하리라
28 Kama vile Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa uhai wake kuwa ukombozi kwa wengi.”
인자가 온 것은 섬김을 받으려 함이 아니라 도리어 섬기려 하고 자기 목숨을 많은 사람의 대속물로 주려 함이니라
29 Wakati wakitoka Yeriko, umati mkubwa ulimfuata.
저희가 여리고에서 떠나갈 때에 큰 무리가 예수를 좇더라
30 Na waliwaona vipofu wawili wameketi kando ya barabara. Waliposikia kuwa Yesu alikuwa anapita, walipaza sauti na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.”
소경 둘이 길 가에 앉았다가 예수께서 지나가신다 함을 듣고 소리질러 가로되 `주여! 우리를 불쌍히 여기소서 다윗의 자손이여' 하니
31 Lakini umati ukawakemea, na kuwaambia nyamazeni. Hata hivyo, wao wakapaza sauti zaidi na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.”
무리가 꾸짖어 잠잠하라 하되 더욱 소리질러 가로되 `주여! 우리를 불쌍히 여기소서 다윗의 자손이여' 하는지라
32 Kisha Yesu alisimama na aliwaita na kuwauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”
예수께서 머물러 서서 저희를 불러
33 Wakamwambia, “Bwana kwamba macho yetu yafumbuliwe.”
가라사대 너희에게 무엇을 하여주기를 원하느냐? 가로되 `주여! 우리 눈뜨기를 원하나이다'
34 Basi Yesu, akiwa amevutwa na huruma, akayagusa macho yao, mara hiyo, wakapokea uwezo wa kuona na wakamfuata.
예수께서 민망히 여기사 저희 눈을 만지시니 곧 보게 되어 저희가 예수를 좇으니라

< Mathayo 20 >