< Mathayo 1 >

1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
亞巴郎之子,達味之子耶穌基督的祖譜:
2 Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka, na Isaka baba wa Yakobo, na Yakobo baba wa Yuda na ndugu zake.
亞巴郎生依撒各,依撒各生雅各伯,雅各伯生猶大和他的兄弟們;
3 Yuda alikuwa baba wa Peresi na Sera kwa Tamari, Peresi baba wa Hezeroni, na Hezeroni baba wa Ramu.
猶由塔瑪爾生培勒茲和則辣黑,培勒茲生赫茲龍,赫茲龍生阿蘭,
4 Ramu alikuwa baba wa Aminadabu, Aminadabu baba wa Nashoni, na Nashoni baba wa Salimoni.
阿蘭生阿米納達布,阿米納達布生納赫雄,納赫雄生撒爾孟,
5 Salimoni alikuwa baba wa Boazi kwa Rahabu, Boazi baba wa Obedi kwa Ruth, Obedi baba wa Yese,
撒爾孟由辣哈布生波阿次,波阿次由盧德生敖貝得,敖貝得生葉瑟,
6 Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi. Daudi alikuwa baba wa Sulemani kwa mke wa Uria.
葉瑟生達味王。達味由烏黎雅的妻子生撒羅滿,
7 Sulemani alikuwa baba wa Rehoboamu, Rehoboamu baba wa Abiya, Abiya baba wa Asa.
撒羅滿生勒哈貝罕,勒哈貝罕生阿彼雅,阿彼雅生阿撒,
8 Asa alikuwa baba wa Yehoshafati, Yehoshafati baba wa Yoramu, na Yoramu baba wa Uzia.
阿撒生約沙法特,約沙法特生約蘭,約蘭生烏齊雅,
9 Uzia alikuwa baba wa Yothamu, Yothamu baba wa Ahazi, Ahazi baba wa Hezekia.
烏齊雅生約當,約當生阿哈次,阿哈次生希則克雅,
10 Hezekia alikuwa baba wa Manase, Manase baba wa Amoni na Amoni baba wa Yosia.
希則克雅生默納舍,默納舍生阿孟,阿孟生約史雅,
11 Yosia alikuwa baba wa Yekonia na kaka zake wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli.
約史雅在巴比倫流徙期間生耶苛尼雅和他的兄弟們,
12 Na baada ya kuchukuliwa kwenda Babeli, Yekonia alikuwa baba wa Shatieli, Shatieli alikuwa babu yake na Zerubabeli.
流徙巴比倫以後,耶苛尼雅生沙耳提耳,沙耳提耳生則魯巴比耳,
13 Zerubabeli alikuwa baba wa Abiudi, Abiudi baba wa Eliakimu, na Eliakimu baba wa Azori.
則魯巴比耳生阿彼鳥得,阿彼鳥得生厄里雅金,厄里雅金生阿左耳。
14 Azori alikuwa baba wa Zadoki, Zadoki baba wa Akimu, na Akimu baba wa Eliudi.
阿左耳生匝多克,匝多克生阿歆,阿歆生厄里烏得,
15 Eliudi alikuwa baba wa Elieza, Elieza baba wa Matani na Matani baba wa Yakobo.
厄里烏得生厄肋阿匝爾,厄肋阿匝爾生瑪堂,瑪堂生雅各伯,
16 Yakobo alikuwa baba wa Yusufu mume wa Mariamu, ambaye kwa yeye Yesu alizaliwa, aitwaye Kristo.
雅各伯生若瑟、瑪利亞的丈夫,瑪利亞生耶穌,衪稱為基督。
17 Vizazi vyote tangu Ibrahimu hadi Daudi vilikuwa vizazi kumi na vinne, kutoka Daudi hadi kuchukuliwa kwenda Babeli vizazi kumi na vinne, na kutoka kuchukuliwa kwenda Babeli hadi Kristo vizazi kumi na vinne.
所以從亞巴郎到達味共十四代,從達味到流徙巴比倫共十四代,從流徙巴比倫到基督共十四代。
18 Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
耶穌基督的誕生是這樣的:衪的母親許配於若瑟後,在同居前,她因聖神有孕的事已顯示出來。
19 Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri.
她的丈夫若瑟,因是義人,不願公開羞她,有意暗暗地休退她。
20 Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,'' Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
當他在思慮這事時,看,在夢人上主的天使顯現給他說:「達味之子若瑟,不要怕娶你的妻子瑪利亞,因為那在她內受生的,是出於聖神。
21 Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.''
她要生一個兒子,妳要給衪起名叫耶穌,因為衪要把自己的民族,由他們的罪惡中拯救出來。」
22 Yote haya yalitokea kutimizwa kile kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema,
這一切事的發生,是為應驗上主藉先知所說的話:
23 “Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, na watamwita jina lake Imanueli”— maana yake, “Mungu pamoja nasi.”
「看,一位貞女,將懷孕生子,人將稱衪的名字為厄瑪奴耳,意思是:天主與我們同在。
24 Yusufu aliamka kutoka usingizini na kufanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru na alimchukua kama mkewe.
若瑟從睡夢中醒來,就照上主的天使所囑咐的辦了,娶了他的妻子;
25 Hata hivyo, hakulala naye mpaka alipojifungua mtoto wa kiume na alimwita jina lake Yesu.
若瑟雖然沒認識她,她就生了一個兒子,給衪起名叫耶穌。

< Mathayo 1 >