< Marko 2 >

1 Aliporudi Kaperinaumu baada ya siku chache, ilisikika kwamba alikuwa nyumbani.
And again he entered Capernaum, after some days; and they heard that he was in the house.
2 Watu wengi sana walikuwa wamekusanyika pale na haikuwepo nafasi tena, hata ile ya pale mlangoni, na Yesu alisema neno kwao.
And immediately many came together, so that the house could contain them no longer, nor could the space about the door. And he preached the word to them.
3 Kisha baadhi ya watu walikuja kwake waliomleta mtu aliyekuwa amepooza; watu wanne walikuwa wamembeba.
And they came to him, bringing a paralytic, who was carried by four men.
4 Wakati waliposhindwa kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu, waliondoa paa juu ya mahali pale alipokuwa. Na walipokuwa wamekwishatoboa tundu, walishusha kitanda ambacho mtu aliyepooza alikuwa amelala.
And not being able to come near him, on account of the multitude, they took off the roof where he was, and having broken through, they let down the bed on which the paralytic lay.
5 Alipoiona imani yao, Yesu alimwambia mtu aliyepooza, “mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.”
And Jesus, seeing their faith, said to the paralytic: Son, your sins are forgiven you.
6 Lakini baadhi ya waandishi wale waliokuwa wamekaa pale walijihoji mioyoni mwao,
But some of the scribes were sitting there, and reasoning in their hearts:
7 “Anawezaje mtu huyu kusema hivi? Anakufuru! Nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”
Why does this man thus speak impiously? Who can forgive sins but God only?
8 Mara Yesu alijua rohoni mwake walichokuwa wakifikiri miongoni mwao wenyewe. Aliwaambia, “Kwa nini mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
And Jesus, immediately perceiving in his spirit that they thus reasoned within themselves, said to them: Why are you reasoning thus in your hearts?
9 Lipi ni jepesi zaidi kusema kwa mtu aliyepooza, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema 'Simama, chukua kitanda chako, na utembee?'
Which is easier, to say to the paralytic, Your sins are forgiven; or to say, Arise, take up your bed and walk?
10 Lakini ili wapate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi katika dunia, alimwambia yule aliyepooza,
But that you may know that the Son of man on earth has authority to forgive sins, (he said to the paralytic, )
11 “Nakuambia wewe, inuka, chukua mkeka wako, na uende nyumbani kwako.”
I say to you, Arise, take up your bed and go to your house.
12 Alisimama na mara moja akachukua mkeka wake, na alikwenda nje ya nyumba mbele ya kila mtu, hivyo wote walishangaa na walimpa Mungu utukufu, na wakasema “Kamwe, hatujawahi kuona jambo kama hili.”
And he arose forthwith, and took up his bed, and went out before them all; so that they were all amazed, and glorified God, saying: We have never seen it thus.
13 Alienda tena kando ya ziwa, na umati wote wa watu walikuja kwake, na akawafundisha.
And he went out again by the sea: and all the multitude came to him, and he taught them.
14 Alipokuwa akipita alimwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi kwenye sehemu ya kukusanyia kodi na akamwambia, “Nifuate.” Alisimama na kumfuata.
And as he passed by, he saw Levi the son of Alphæus sitting at the custom-house; and he said to him: Follow me. And he arose and followed him.
15 Na wakati Yesu alipokuwa akipata chakula katika nyumba ya Lawi, wakusanya kodi wengi na watu wenye dhambi walikuwa wakila na Yesu na wanafunzi wake, kwa kuwa walikuwa wengi nao walimfuata.
And it came to pass, as Jesus reclined at table in his house, that many publicans and sinners reclined with him and his disciples; for there were many, and they followed him.
16 Wakati waandishi, ambao walikuwa Mafarisayo, walipoona kwamba Yesu alikuwa akila na watu wenye dhambi na wakusanya kodi, waliwaambia wanafunzi wake, “Kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?”
And when the scribes and Pharisees saw him eating with publicans and sinners, they said to his disciples: Why is it that he eats and drinks with publicans and sinners?
17 Wakati Yesu aliposikia hivi aliwaambia, “Watu walio na afya katika mwili hawamhitaji tabibu; ni watu wagonjwa pekee ndio wanamhitaji. Sikuja kuwaita watu wenye haki, lakini watu wenye dhambi.”
And when Jesus heard it, he said to them: Those who are well have no need of a physician, but those who are sick. I have not come to call righteous men, but sinners.
18 Wanafunzi wa Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Na baadhi ya watu walikuja kwake na kumwambia, “Kwa nini wanafunzi wa Yohana na mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
And the disciples of John and of the Pharisees were in the habit of fasting; and they came, and said to him: Why do the disciples of John and of the Pharisees fast, but your disciples fast not?
19 Yesu aliwaambia, “Je waliohudhuria harusini wanaweza kufunga wakati bwana harusi bado akiwa pamoja nao? Kwa vyovyote bwana harusi akiwa bado yuko pamoja nao hawawezi kufunga.”
And Jesus said to them: Can the sons of the bride-chamber fast, while the bridegroom is with them? As long as they have the bridegroom with them, they can not fast.
20 Lakini siku zitakuja wakati bwana harusi atakapoondolewa kwao, na katika siku hizo wao watafunga.
But the days will come when the bridegroom shall be taken from them, and then they will fast in those days.
21 Hakuna mtu ashonaye kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu, vinginevyo kiraka kitabanduka kutoka katika hilo, kipya kubanduka kutoka katika kikuukuu, na kutakuwepo mpasuko mbaya.
No one sews a patch of new cloth on an old garment; if so, the new piece which fills it up, takes from the old, and a worse rent is made.
22 Hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu, vinginevyo divai itavipasua viriba na vyote viwili divai na viriba vitapotea. Badala yake, weka divai mpya katika viriba vipya.”
And no one puts new wine into old bottles; if so, the new wine bursts the bottles, and the wine is spilled, and the bottles are destroyed. But new wine must be put into new bottles.
23 Katika siku ya Sabato Yesu alipita kwenye baadhi ya mashamba, na wanafunzi wake walianza kuchukua baadhi ya masuke ya ngano.
And it came to pass, that he was going on the sabbath-day through the fields of grain: and his disciples began, as they went, to pull the ears of grain.
24 Na Mafarisayo walimwambia, “Tazama, kwa nini wanafanya kitu ambacho ni kinyume cha sheria katika siku ya Sabato?”
And the Pharisees said to him: See, why are they doing on the sabbath-day what is not lawful?
25 Aliwaambia, “Hamkusoma kile alichofanya Daudi alipokuwa katika uhitaji na njaa—yeye pamoja na watu waliokuwa pamoja naye?
And he said to them: Did you never read what David did, when he had need and was hungry, he and those who were with him?
26 Jinsi alivyoenda katika nyumba ya Mungu wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu na akala mkate uliowekwa mbele—ambao ilikuwa kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kula isipokuwa makuhani—na aliwapa hata baadhi ya wale waliokuwa pamoja naye?”
How he entered the house of God in the days of Abiathar the chief priest, and ate the loaves of the presence, which, it is not lawful, except for the priests, to eat, and gave to those also who were with him?
27 Yesu alisema, “Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, siyo mwanadamu kwa ajili ya Sabato.
And he said to them: The sabbath was made for man, not man for the sabbath.
28 Kwa hiyo, Mwana wa Adamu ni Bwana, hata kwa Sabato.”
Therefore, the Son of man is Lord also of the sabbath.

< Marko 2 >