< Marko 12 >

1 Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mifano. Akasema, “Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la kusindika mvinyo. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali.
I uze im zboriti u prispodobama: Čovjek vinograd posadi, ogradom ogradi, iskopa tijesak i kulu podiže pa ga iznajmi vinogradarima i otputova.
2 Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu.
I u svoje vrijeme posla vinogradarima slugu da od njih uzme dio uroda vinogradarskoga.
3 Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote.
A oni ga pograbiše, istukoše i otposlaše praznih ruku.
4 Akamtuma kwao mtumishi mwingine, wakamjeruhi kichwani na kumtendea mambo ya aibu.
I opet posla k njima drugog slugu: i njemu razbiše glavu i izružiše ga.
5 Bado alimtuma mwingine, na huyu mmoja walimwua. Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo, wakiwapiga na wengine kuwaua.
Trećega također posla: njega ubiše. Tako i mnoge druge: jedne istukoše, druge pobiše.”
6 Alikuwa bado na mtu mmoja zaidi wa kumtuma, mwana mpendwa. Naye alikuwa wa mwisho aliyetumwa kwao. Akisema, “Watamheshimu mwanangu”.
“Još jednoga imaše, sina ljubljenoga. Njega naposljetku posla k njima misleći: 'Poštovat će sina moga.'
7 Lakini wapangaji walisemezana wao kwa wao, “Huyu ndiye mrithi. Njoni, hebu na tumwue, na urithi utakuwa wetu.”
Ali ti vinogradari među sobom rekoše: 'Ovo je baštinik! Hajde da ga ubijemo i baština će biti naša.'
8 Walimvamia, wakamuua na kumtupa nje ya shamba la mizabibu.
I pograbe ga, ubiju i izbace iz vinograda.”
9 Kwa hiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wa mizabibu na atalikabidhi shamba la mizabibu kwa wengine.
“Što li će učiniti gospodar vinograda? Doći će i pobiti te vinogradare i dati vinograd drugima.
10 Hamjapata kusoma andiko hili? “Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe la pembeni.
Niste li čitali ovo Pismo: Kamen što ga odbaciše graditelji, postade kamen zaglavni.
11 Hili lilitoka kwa Bwana, na ni la ajabu machoni petu.”
Gospodnje je to djelo - kakvo čudo u očima našim!”
12 Walitafuta kumkamata Yesu, Lakini waliwaogopa makutano, kwani walijua kuwa alikuwa amenena mfano huo dhidi yao. Hivyo walimwacha na wakaenda zao.
I tražili su da ga uhvate, ali se pobojaše mnoštva. Razumješe da je protiv njih izrekao prispodobu pa ga ostave i odu.
13 Kisha wakawatuma baadhi ya mafarisayo na maherodia kwake ili kumtega kwa maneno.
I pošalju k njemu neke od farizeja i herodovaca da ga uhvate u riječi.
14 Walipofika, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba hujali maoni ya yeyote na huonyeshi upendeleo kati ya watu. Unafundisha njia ya Mungu katika ukweli. Je! Ni haki kulipa kodi kwa Kaisari au la? Je! Twaweza kulipa au la?
Oni dođu i kažu mu: “Učitelju, znamo da si istinit i ne mariš tko je tko jer nisi pristran, nego po istini učiš putu Božjemu. Je li dopušteno dati porez caru ili nije? Da damo ili da ne damo?”
15 Lakini Yesu alijua unafiki wao na kuwaambia, “Kwa nini mnanijaribu? Nipeni dinari niweze kuitazama.”
A on im reče prozirući njihovo licemjerje: “Što me iskušavate? Donesite mi denar da vidim!”
16 Wakaleta moja kwa Yesu, Akawaambia, “Je! ni sura ya nani na maandishi yaliyopo hapa ni ya nani? Wakasema, “Ya Kaisari.”
Oni doniješe. I reče im: “Čija je ovo slika i natpis?” A oni će mu: “Carev.”
17 Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vya Kaisari na Mungu vitu vya Mungu.” Wakamstaajabia.
A Isus im reče: “Caru podajte carevo, a Bogu Božje!” I divili su mu se.
18 Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema,
Dođu k njemu saduceji, koji vele da nema uskrsnuća, i upitaju ga:
19 “Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, 'Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.'
“Učitelju, Mojsije nam napisa: Umre li čiji brat i ostavi ženu, a ne ostavi djeteta, neka njegov brat uzme tu ženu te podigne porod bratu svomu.
20 Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto.
Sedmero braće bijaše. Prvi uze ženu i umrije ne ostavivši poroda.
21 Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika.
I drugi je uze te umrije ne ostavivši poroda. I treći jednako tako.
22 Na wa saba alikufa bila kuacha watoto. Mwishowe na mwanamke pia akafa.
I sedmorica ne ostaviše poroda. Najposlije i žena umrije.
23 Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwani wale ndugu wote saba walikuwa waume wake.”
Komu će biti žena o uskrsnuću, kad uskrsnu? Jer sedmorica su je imala za ženu.”
24 Yesu aliwaambia, “Je! Hii si sababu kuwa mmepotoshwa, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?”
Reče im Isus: “Niste li u zabludi zbog toga što ne razumijete Pisama ni sile Božje?
25 Wakati wa kufufuka toka kwa wafu, hawataoa wala kuingia katika ndoa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni.
Ta kad od mrtvih ustaju, niti se žene niti udavaju, nego su kao anđeli na nebesima.
26 Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamkusoma kutoka katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema na kumwambia, 'Mimi ni Mungu wa Abrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?'
A što se tiče mrtvih, da ustaju, niste li čitali u knjizi Mojsijevoj ono o grmu, kako Mojsiju reče Bog: Ja sam Bog Abrahamov i Bog Izakov i Bog Jakovljev?
27 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Ni dhahiri mmepotoka.”
Nije on Bog mrtvih, nego živih. Uvelike se varate.”
28 Mmoja wa waandishi alikuja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, “Je! ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi katika zote?”
Tada pristupi jedan od pismoznanaca koji je slušao njihovu raspravu. Vidjevši da im je dobro odgovorio, upita ga: “Koja je zapovijed prva od sviju?”
29 Yesu alimjibu, “Iliyo ya muhimu ni hii, “Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja.
Isus odgovori: “Prva je: Slušaj, Izraele! Gospodin Bog naš Gospodin je jedini.
30 Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako yote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.'
Zato ljubi Gospodina Boga svojega iz svega srca svojega, i iz sve duše svoje, i iz svega uma svoga, i iz sve snage svoje!”
31 Amri ya pili ni hii, 'Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.' Hakuna amri nyingine kuu zaidi ya hizi.”
“Druga je: Ljubi svoga bližnjega kao sebe samoga. Nema druge zapovijedi veće od tih.”
32 Mwandishi akasema, “Vema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake.
Nato će mu pismoznanac: “Dobro, učitelju! Po istini si kazao: On je jedini, nema drugoga osim njega.
33 Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mwenyewe, ni muhimu mno kuliko matoleo na dhabihu za kuteketeza.”
Njega ljubiti iz svega srca, iz svega razuma i iz sve snage i ljubiti bližnjega kao sebe samoga - više je nego sve paljenice i žrtve.”
34 Wakati Yesu alipoona ametoa jibu la busara, alimwambia, “Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu.” Baada ya hapo hakuna hata mmoja aliye thubutu kumwuliza Yesu maswali yoyote.
Kad Isus vidje kako je pametno odgovorio, reče mu: “Nisi daleko od kraljevstva Božjega!” I nitko se više nije usuđivao pitati ga.
35 Na Yesu alijibu, wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, akasema, “Je! waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi?
A naučavajući u Hramu, uze Isus govoriti: “Kako pismoznanci kažu da je Krist sin Davidov?
36 Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, 'Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye maadui wako kuwa chini ya miguu yako.'
A sam David reče u Duhu Svetome: Reče Gospod Gospodinu mojemu: 'Sjedni mi zdesna dok ne položim neprijatelje tvoje za podnožje nogama tvojim!'
37 Daudi mwenyewe humwita Kristo, 'Bwana' Je! ni mwana wa Daudi kwa jinsi gani?” Na kusanyiko kuu lilimsikiliza kwa furaha.
Sam ga David zove Gospodinom. Kako mu je onda sin?” Silan ga je svijet s užitkom slušao.
38 Katika mafundisho yake Yesu alisema, “Jihadharini na waandishi, wanaotamani kutembea na kanzu ndefu na kusalimiwa kwenye masoko
A on im u pouci svojoj govoraše: “Čuvajte se pismoznanaca, koji rado idu u dugim haljinama, vole pozdrave na trgovima,
39 na kuketi kwenye viti vya wakuu katika masinagogi na katika sikukuu kwa maeneo ya wakuu.
prva sjedala u sinagogama i pročelja na gozbama;
40 Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu.”
proždiru kuće udovičke, još pod izlikom dugih molitava. Stići će ih to oštrija osuda!”
41 Kisha Yesu aliketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa.
Potom sjede nasuprot riznici te promatraše kako narod baca sitniš u riznicu. Mnogi bogataši bacahu mnogo.
42 Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia vipande viwili, thamani ya senti.
Dođe i neka siromašna udovica i baci dva novčića, to jest jedan kvadrant.
43 Kisha akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, “Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka.
Tada dozove svoje učenike i reče im: “Doista, kažem vam, ova je sirota udovica ubacila više od svih koji ubacuju u riznicu.
44 Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake.”
Svi su oni zapravo ubacili od svoga suviška, a ona je od svoje sirotinje ubacila sve što je imala, sav svoj žitak.”

< Marko 12 >