< Malaki 3 >
1 Tazama, namtuma mjumbe wangu, atakayeandaa njia mbele yangu. Na Bwana, ambaye mnamtafuta, atakuja ghafla katika hekalu lake; na mjumbe wa agano, ambaye katika yeye mnafurahi, tazama anakuja.” asema Bwana wa Majeshi.
Ecce ego mitto angelum meum, et præparabit viam ante faciem meam. Et statim veniet ad templum suum Dominator, quem vos quæritis, et angelus testamenti, quem vos vultis. Ecce venit, dicit Dominus exercituum:
2 Na ni nani atakeyevumilia siku ya kuja kwake? na nani atasimama akishatokea? Yeye ni kama mtu asafishaye kwa moto na kama sabuni ya kufulia.
et quis poterit cogitare diem adventus eius, et quis stabit ad videndum eum? Ipse enim quasi ignis conflans, et quasi herba fullonum:
3 Atakaa na kutawala kama msafishaji wa fedha, na atawasafisha wana wa Lawi. na atawafanya wawe safi kama dhahabu na fedha, na wataleta sadaka za haki kwa Bwana.
et sedebit conflans, et emundans argentum, et purgabit filios Levi, et colabit eos quasi aurum, et quasi argentum, et erunt Domino offerentes sacrificia in iustitia.
4 Na sadaka ya Yuda na Yerusalem itampendeza Bwana, kama siku za kale, na miaka ya zamani.
Et placebit Domino sacrificium Iuda, et Ierusalem sicut dies sæculi, et sicut anni antiqui.
5 Kisha nitapita karibu na ninyi kuwahukumu. na nitakuwa shahidi mwepesi dhidi ya wachawi, wazinzi, mahsahidi wa uongo, na kinyume cha wale wanaoonea wafanyakazi katika mizigo yake, wanaoonea wajane na yatima, na anayemfukuza mgeni kutoka kwenye haki yake, na kwa wale wasionitii mimi,”asema Bwana wa majeshi.
Et accedam ad vos in iudicio, et ero testis velox maleficis, et adulteris, et periuris, et qui calumniantur mercedem mercenarii, viduas, et pupillos, et opprimunt peregrinum, nec timuerunt me, dicit Dominus exercituum.
6 Mimi Bwana, sibadiliki; pia ninyi, watu wa Yakobo, hamkutumia.
Ego enim Dominus, et non mutor: et vos filii Iacob non estis consumpti.
7 Toka siku za baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu na hamkuzitunza. Nigeukieni, nami nitawarudia ninyi,” asema Bwana wa majeshi. Lakini mwasema, tutakurudiaje?
A diebus enim patrum vestrorum recessistis a legitimis meis, et non custodistis. Revertimini ad me, et revertar ad vos, dicit Dominus exercituum. Et dixistis: In quo revertemur?
8 Mwanadamu anaweza kumwibia Mungu? Mnaniibia mimi, lakini mwasema, 'Tumekuibiaje?' kwa zaka na sadaka.
Si affliget homo Deum, quia vos configitis me? Et dixistis: In quo configimus te? In decimis, et in primitiis.
9 Mmelaani kwa laana, kwa kuniibia mimi, taifa lote hili.
Et in penuria vos maledicti estis, et me vos configitis gens tota.
10 Leteni zaka kamili katika ghalani, ili kwamba kiwemo chakula katika nyumba yangu. Na mnijaribu kwa hili,” asema Bwana wa Majeshi. “kama sitawafungulia madilisha ya mbinguni na kuwamwagia baraka juu yenu, ili kwamba hakutakuwa na sehemu ya kutosha kuzipokea.
Inferte omnem decimam in horreum, et sit cibus in domo mea, et probate me super hoc, dicit Dominus: si non aperuero vobis cataractas cæli, et effudero vobis benedictionem usque ad abundantiam,
11 Nitamkemea mharibifu kwako, kwamba asiharibu mavuno yenu ya nchi yenu; mizazibu yenu katika shamba haitapukutisha kabla ya wakati wake,” asema Bwana wa Majeshi.
et increpabo pro vobis devorantem, et non corrumpet fructum terræ vestræ: nec erit sterilis vinea in agro, dicit Dominus exercituum.
12 Mataifa yote watakuita mbarikiwa; kwa ajili yako itakuwa ni nchi ya furaha,” asema Bwana wa Majeshi.
Et beatos vos dicent omnes Gentes: eritis enim vos terra desiderabilis, dicit Dominus exercituum.
13 Maneo yenu yamekuwa magumu kinyume changu,” asema Bwana. lakini mwasema, “Tumesema nini kinyume chako?'
Invaluerunt super me verba vestra, dicit Dominus.
14 mmesema, 'Hakuna maana kumtumikia Mungu. Kuna faida ya namna gani kutunza maagizo yake au kutembea huku mkiomboleza mbele za Bwana wa Majeshi?
Et dixistis: Quid locuti sumus contra te? Dixistis: Vanus est, qui servit Deo: et quod emolumentum quia custodivimus præcepta eius, et quia ambulavimus tristes coram Domino exercituum?
15 Na sasa tunamwita mwenye kiburi mbarikiwa. Waharifu si kufanikiwa tu, bali kumjaribu Mungu na kumwepuka.”
Ergo nunc beatos dicimus arrogantes: siquidem ædificati sunt facientes impietatem, et tentaverunt Deum, et salvi facti sunt.
16 Kisha wale wanaomweshimu Bwana walisemezana mmoja baada ya mwingine; Bwana yuko makini kutusikiliza, na kitabu cha kumbukumbu kiliandikwa mbele zake kwa ajili ya wale wanamwogopa Bwana na kuliheshimu jina lake.
Tunc locuti sunt timentes Dominum, unusquisque cum proximo suo: Et attendit Dominus, et audivit: et scriptus est liber monumenti coram eo timentibus Dominum, et cogitantibus nomen eius.
17 “Watakuwa wangu,” asema Bwana wa majeshi,” hazina zangu, katika siku nitakayotenda; nitawapenda, kama mtu anavyompenda mwanawe anayemhudumia.
Et erunt mihi, ait Dominus exercituum, in die, qua ego facio, in peculium: et parcam eis, sicut parcit vir filio suo servienti sibi.
18 Kisha zaidi sana nitatofautisha kati ya haki wenye haki na waovu, kati ya anayemwabudu Mungu na asiyemwabudu yeye.
Et convertemini, et videbitis quid sit inter iustum, et impium: et inter servientem Deo, et non servientem ei.