< Luka 7 >
1 Baada ya Yesu kumaliza kila kitu alichokuwa anasema kwa watu waliomsikiliza, akaingia Kapernaumu.
Hanchu, Jisua'n mingei kôma chong a ril zoiin chu Capernaum'a khuoa a sea.
2 Mtumwa fulani wa akida, aliyekuwa wa thamani sana kwake, alikuwa mgonjwa sana na alikuwa karibu ya kufa.
Rom râlmi ruoipu tîrlâm midit tak dam maka, a thi vavânga.
3 Lakini akiwa amesikia kuhusu Yesu, yule Akida alimtuma kiongozi wa kiyahudi, kumwomba aje kumwokoa mtumwa wake ili asife.
Hanchu, Jisua'n thurchi a rieta anin chu a juonga a tîrlâm mindam ranga ngên rangin Juda Upangei a tîra.
4 Walipofika karibu na Yesu, walimsihi kwa bidii na kusema, “anastahili kwamba unapaswa kufanya hivi kwa ajili yake,
Jisua kôma an honga, “Hi mi hih na san thei ruo ani.
5 kwa sababu analipenda taifa letu, na ndiye aliyejenga sinagogi kwa ajili yetu”.
Kin mingei lung a min khama, kin synagog khom mi sin pe ani” tiin an ngên rîta.
6 Yesu akaendelea na safari yake pamoja nao. lakini kabla hajaenda mbali na nyumba, afisa mmoja aliwatuma marafiki zake kuzungumza naye. “Bwana, usijichoshe mwenyewe kwa sababu mimi sistahili wewe kuingia kwenye dari yangu.
Hanchu Jisua'n, anni ngei hah a jûi zoia. In a tung rangtôn chu, râlmi ruoipu'n a malngei a tîra, “O pu, intak takin hong no roh, ki ina mini pan rangin inhoi mu-ung.
7 Kwa sababu hii sikufikiria hata mimi mwenyewe kuwa ninafaa kuja kwako, lakini sema neno tu na mtumishi wangu atapona.
Mapêna keima ngêt no kôma hong rang khomin inhoi mu-ung. Hê vai minchôi inla ki tîrlâm chu dam a tih.
8 Kwani mimi pia ni mtu niliyewekwa kwenye mamlaka na nina askari chini yangu. Husema kwa huyu “Nenda” na huenda, na kwa mwingine, “Njoo” naye huja, na kwa mtumishi wangu 'Fanya hiki', na yeye hufanya”.
Keikhom kenêka ulien chong nuoia om ki ni. Ko chong nuoia râlmingei an oma, inkhat kôm, ‘Se roh’ ki tiin a sea, ‘Hong roh,’ ki tiin a honga, Ki tîrlâm kôm, ‘Hih sin roh’ ki tiin a sin ngâi” a tia.
9 Yesu aliposikia haya alishangaa, na kuwageukia makutano waliokuwa wanamfuata na kusema.”Nawaambia, hata katika Israeli, sijawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama huyu.
Hanchu, Jisua'n a rieta anin chu kamâm aom a tia, mipui ama jûi ngei a en titira, an kôma, “Nangni ki ril, hi angtaka taksônna hi chu Isrealngei lâia luo la mu ngâi mu-ung” a tia.
10 Kisha wale waliokuwa wametumwa walirudi nyumbani na kumkuta mtumishi akiwa mzima.
Thangthei ngeiin ruoipu in an hong kîrnôk inchu tîrlâm hah a damin an hong mu zoi.
11 fulani baada ya haya, ilitokea kuwa Yesu alikuwa anasafiri kwenda mji ulioitwa Naini. wanafunzi wake wakaenda pamoja naye wakiambana na umati wa watu.
Chomolte suole chu Jisua, Nain khopuia a se zoia, a ruoisingei le mipuingeiin an jûia.
12 Alipofika karibu na Lango la jiji tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake. aliyekuwa mjane, na umati wa wawakilishi kutoka kwenye jiji walikuwa pamoja naye.
Hanchu, khopui mokot an tungin chu, mithi an hong rojôna. Ma athipa hah meithâinu nâikhât ania, male A khopuia mi tamtak ngei khom a kôma an oma.
13 Alipomwona, Bwana akamsogelea kwa huruma kubwa sana juu yake na akamwambia, “Usilie”.
Hanchu, Pumapa'n ama amûn chu inrieng amu oka, a kôm, “Chap no roh” a tipea.
14 Kisha akasogea mbele akaligusa jeneza ambalo walibebea mwili, na wale waliobeba wakasimama akasema “Kijana nasema amka”
Hanchu ava nâia, a tolâi a tôna, a rojôn ngei an inngama, Jisua'n, “Ruotharte, inthoi roh nang ki ti,” a tia.
15 Mfu akainuka na kukaa chini na akaanza kuongea. Kisha Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
Hanchu, mithi hah ânsung lita, a chonga. Hanchu, Jisua'n a nû kôm a pêk nôk zoi.
16 Kisha hofu ikawajaa wote. wakaendelea kumtukuza Mungu wakisema “Nabii mkuu ameinuliwa miongoni mwetu” na “Mungu amewaangalia watu wake”
An rêngin an chia, Pathien an minpâka, “Ei lâia dêipu roiinpui tak a juong inlanga, a mingei mi minjôk rangin Pathien a juong zoi,” an tia.
17 Hizi habari njema za Yesu zilienea Yudea yote na kwa mikoa yote ya jirani.
Hi Jisua thurchi hih Judea ram pumpuia le a kôlrevêla ânthang zit zoi.
18 Wanafunzi wa Yohana walimwamwambia mambo haya yote.
John ruoisingeiin Jisua thurchi John an rila, hanchu a ruoisingei mi inik a koia,
19 Ndipo Yohana akawaita wawili wa wanafunzi wake na kuwatuma kwa Bwana kusema “Wewe ndiye yule ajaye, au kuna mtu mwingine tumtazamie?
Pumapa kôm a tîr ngeia, “a juong rang Messiah hah mo ni ni, mo midang kin la tûng rang mo?” itia rekel rangin.
20 Walipofika karibu na Yesu hawa wakasema, “Yohana mbatizaji ametutuma kwako kusema, 'Wewe ni yule ajaye au kuna mtu mwingine tumtazamie?”
Hanchu, Jisua kôma an honga, “Baptispu John'n, a juong rangpu hah nini mo, midang kin la tûng rang mo? a ti” tiin an rekela.
21 kwa wakati huo aliowaponya watu wengi kutoka katika magonjwa na mateso, kutoka kwa roho wachafu, na kwa watu wenye upofu aliwapa kuona.
Ma lâitaka han, Jisua'n, mi tamtak damloingei, an natnangei, ramkhori sûrngei a mindam ngeia, mitchongei mit a minvâr pea.
22 Yesu akajibu na kusema kwao. “Baada ya kuwa mmekwenda mlikotoka mtamjulisha Yohana mlichokiona na kukisikia. Wenye upofu wanapokea kuona na viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na kuwa hai tena, masikini wanaambiwa habari njema.
Hanchu, John ruoisingei kôma, “Se nôk ungla, John kôma, nin mu ngei le nin riet ngei hah va ril roi, mitchongeiin an mu theia, kholrangei an lôn thei zoi, aphârngei an inthienga, kuorsetngei kuor avâra, mithingei aringin an inthoi nôka, inriengngei kôma Thurchi Sa misîr ani zoi.
23 Na mtu ambaye hataacha kuniamini mimi kwa sababu ya matendo yangu amebarikiwa”.
Iem zoiloina nei loi ngei chu satvur anni,” a tipe ngeia.
24 Baada ya wale waliotumwa na Yohana kurudi walikotoka, Yesu akaanza kusema kwa makutano juu ya Yohana, “Mlikwenda nje kuona nini, mwanzi ukiwa unatikiswa na upepo?
John ruoisingei an se zoiin chu, Jisua'n John chungroi mipuingei kôma a misîra. “A kôma ramchâra nin se lâia han imo mu rangin nin sabei? phâivuon ai sêm sûl innîk ngei mo?
25 lakini mlikwenda nje kuona nini, mtu aliyevaa vizuri? tazama watu wale wanaovaa mavazi ya kifalme na kuishi maisha ya starehe wako kwenye nafasi za wafalme.
Imo a en ranga nin se? Puon innêm insil mi mo? Ha anga insil ngâi ngei le ningnuoma lêng ngei chu rêng inah kêng an om ngâi.
26 lakini mnakwenda nje kuona nini, Nabii? Ndiyo, ninasema kwenu na zaidi sana kuliko nabii.
Ni ril ta u, imo a en ranga nin se? Dêipu na? O, ani, Dêipu nêka lien uol nin mu zoi.
27 Huyu ndiye aliyeandikiwa, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya macho yenu, atakeyeandaa njia kwa ajili yangu,
John hih Pathien lekhabua, ‘Ki tîrton no motona na lampui sin rangin tîr ki tih,’ ai ti chu ani.
28 Nasema kwenu, kati ya wale waliozaliwa na mwanamke, hakuna mkuu kama Yohana, lakini mtu asiye muhimu sana atakayeishi na Mungu mahali alipo yeye, atakuwa mkuu kuliko Yohana.”
Nangni ki ril John hih mi murdi lâia alientak chu ani. Ania, Pathien Rêngrama achîntak khom John nêkin chu a lien uol.”
29 Na watu wote waliposikia haya pamoja na watoza ushuru, walitangaza kuwa Mungu ni mwenye Haki. Walikuwepo kati yao wale waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
John chongril mipuingeiin an rangâia, aliekin sumrusuong ngâi ngeiin Pathien chong an jôma, a kôma baptisma an changa.
30 Lakini mafarisayo na wataalamu wa sheria za kiyahudi, ambao hawakubatizwa na yeye walikataa hekima za Mungu kwa ajili yao wenyewe.
Ania Balam minchupungei le phariseengeiin chu anta ranga Pathien mintuo an henga, John baptisma khom chang mak ngei.
31 Tena naweza kuwalinganisha na nini watu wa kizazi hiki? Wakoje hasai?
Jisua'n, “Atûnlâi ruolthoitharngei hih imo an ang? Ilemo ki mintêk rang ani zoi?
32 Wanafanana na watoto wanaocheza kwenye eneo la soko, wanaokaa na kuitana mmoja baada wa mwingine wakisema, 'Tumepuliza filimbi kwa ajili yenu, na hamkucheza. tumeomboleza na hamkulia.'
Nâipangngei bazar muna insunga, senkhatin inneina berlem nangni kin tum pea, lâm mak cheia, chûlna la kin tho khomin chap mak cheia, itia in hêt inlôm angha anni.
33 Yohana mbatizaji alikuja hakula mkate wala hakunywa divai, na mkasema “Ana pepo.
Baptispu John a juonga, bungêiin uain khom nêk maka, ramkhori kêng nin tia.
34 Mwana wa Mtu amekuja amekula na kunywa na mkasema, “Angali ni mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!
Miriem Nâipasal a juonga, a sâkin a nêka, rolruokpa, sumrusuongpungei le mi nunsiengei malpa nin tia.
35 Lakini hekima imetambulika kuwa ina haki kwa watoto wake wote.”
A modôm ngei rangin chu, Pathien vârna, chongdik minlangna ani” a tia.
36 Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale.
Pharisee inkhatin Jisua bu nêk rangin a siela, Jisua a sea, bu nêk rangin ânsunga.
37 Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato.
Ma khopuia han nupang inkhat nunsie a oma. Jisua Pharisee ina bu a nêk iti a rietin chu, sariek mirimhoi alabastar bilôr a hongchôia.
38 Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato.
Jisua nûktieng a ke bula ândinga, a chapa, a mitrithîn a kengei a mindûi pea. A samin a kengei a hûia, a ke a tuma, sariek mirimhoi a buoka.
39 Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.
Pharisee han a mulungrîlin, “Hi mi hih dêipu dik anîn chu, a tônnu, nupang saloi ani tie hih riet a tih” a tia.
40 Yesu akajibu na kumwambia, “Simoni nina kitu cha kukuambia. “Akasema” “Kiseme tu mwalimu!”
Jisua'n a kôma, “Simon, nang ril rang ke nei” a tia. Simon'n, “O, Minchupu ni ril roh” a tia.
41 Yesu akasema “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini.
Jisua'n a kôma, “Mi inikin lâkâi pêk ngâipu kôm sumdâr an intânga, inkhatin razaranga, inkhatin sômranga.
42 Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi?
An thuon theiloi sikin an ruonin a ngâidam ngeia, a tu han mo lungkham uol nih?” a tia.
43 Simoni akamjibu na kusema, “Nadhani aliyesamehewa zaidi.”Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.”
Simon'n a thuona, “Ki iem lamin chu a ngâidam tam uolpu hah” a tia, Jisua'n, “Ni ti mindik” a tipea.
44 Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, “Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake.
Male chu, nupangnu tieng mâi athaka, Simon kôma, “Hi nupangnu hih nu mu mo? Ni ina ko honga, ka ke rusûkna rang tui ni pêk mak chea, ama'n chu a mit rithîn ke kengei a rusûka, a samin a hûi minhula,
45 Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu.
ni tumin ni lei don mak che, ama chu ko hong renga ka kengei a tum bâng mak.
46 Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato.
Olive sariek ku lua buok mak chea, ama'n chu ka kengei sariek a pol minzo zita.
47 Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu.”
Masikin nang ki ril, lungkhamna lien a minlang han a nunsiena tamtak ngei hah ngâidam ani zoi, iti a minthâr. Masikin, tukhom ngâidamna chînin chu lungkhamna chîn a minlang” a tia.
48 Baadaye akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa”
Male, Jisua'n nupangnu kôma, “Ni sietnangei ngâidam ani zoi” a tipea.
49 Wale waliokaa mezani pamoja naye wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani mpaka anasamehe dhambi?”
A kôma insung ngeiin, Hi anga nunsie ngei tena ngâidam thei hih tumo ai ni? anin tia.
50 Na Yesu akamwambia mwanamke, “Imani yako imekuokoa. Enenda kwa amani”
Ania, Jisua'n nupangnu kôma, “Na taksônnân nang a sanminjôk zoi, rathanngam takin se ta roh” a tipea.