< Luka 3 >
1 Sasa, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberia, wakati Pontio Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi, Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo ndugu yake alikuwa mkuu wa mkoa wa Iturea na Trakoniti, na Lisania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
2 na wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria, jangwani.
3 Alisafiri katika mkoa wote kuzunguka Mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi
4 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya Isaya nabii, “sauti ya mtu aliaye nyikani, “Itengenezeni tayari njia ya Bwana, yatengenezeni mapito yake yaliyoonyoka.
5 Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa, barabara zilizopinda zitanyoshwa, na njia zilizoparaza zitalainishwa.
6 Watu wote watauona wokovu wa Mungu.”
7 Hivyo, Yohana akawaambia makutano makubwa ya watu waliomjia wapate kubatizwa na yeye, “Ninyi uzao wa nyoka wenye sumu, nani aliwaonya kuikimbia gadhabu inayokuja?
8 Zaeni matunda yanayoedana na toba, na msianze kusema ndani yenu, “Tunaye Ibarahimu ambaye ni baba yetu; kwa sababu nawaambia ya kwamba, Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.
9 Tayari shoka limeshawekwa kwenye mzizi wa miti. Hivyo, kila mti usiozaa matunda mema, hukatwa na kutupwa motoni.
10 Kisha watu katika makutano walimuuliza wakisema, “Sasa tunatakiwa tufanyeje?”
11 Alijibu na kuwaambia, “kama mtu ana kanzu mbili anatakiwa atoe kanzu moja kwa mwingine ambaye hana kabisa, na ambaye ana chakula na afanye vivyo hivyo.”
12 Kisha baadhi ya watoza ushuru walikuja pia kubatizwa, na wakamwambia, “Mwalimu, tunatakiwa kufanya nini?
13 Akawaambia, “Msikusanye fedha zaidi kuliko mnachotakiwa kukusanya.”
14 Baadhi ya maaskari pia wakamuuliza wakisema, “Na sisi je? Tunatakiwa tufanye nini?” Akawambia, “Msichukue fedha kwa mtu yeyote kwa nguvu, na msimtuhumu mtu yeyote kwa uongo. Ridhikeni na mishahara yenu.”
15 Sasa, kwa kuwa watu walikuwa na shauku ya kumngojea Kristo atakaye kuja, kila mmoja alikuwa anawaza moyoni mwake kuhusu Yohana kama yeye ndiye Kristo.
16 Yohana akajibu kwa kuwaambia wote, “Mimi nawabatiza ninyi kwa maji, lakini kuna mmoja ajaye ambaye ana nguvu kuliko mimi, na sisitahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17 Pepeto lake liko mkononi mwake ili kusafisha vizuri uwanda wake wa kupepetea ngano na kuikusanya ngano ghalani mwake. Lakini, atayateketeza makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.
18 Kwa maonyo mengine mengi pia, alihubiri habari njema kwa watu.
19 Yohana alimkemea pia Herode mkuu wa mkoa kwa kumuoa Herodia, mke wa ndugu yake na kwa maovu mengine mengi ambayo Herode alikuwa ameyatenda.
20 Lakini baadaye Herode alifanya uovu mwingine mbaya sana. Alimfunga Yohana gerezani.
21 Kisha ilitokea kwamba, wakati watu wote walipokuwa wakibatizwa na Yohana, naye Yesu alibatizwa pia. Wakati alipokuwa akiomba, mbingu zikafunguka.
22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama njiwa, wakati huo huo sauti ikaja kutoka mbinguni ikisema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe.”
23 Sasa Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri upatao miaka thelathini. Alikuwa ni mwana (kama ilivyotadhaniwa) wa Yusufu, mwana wa Eli,
24 mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yana, mwana wa Yusufu,
25 mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Esli, mwana wa Nagai,
26 mwana wa Maati, mwana wa Matathia, mwana wa Semeini, mwana wa Yusufu, mwana wa Yuda,
27 mwana wa Yoanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri,
28 mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,
29 mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa Matathi, mwana wa Lawi,
30 mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yusufu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliyakimu,
31 mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,
32 mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
33 mwana wa Abinadabu, mwana wa Aramu, mwana wa Hesroni, mwana wa Peresi, mwana wa Yuda,
34 mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Ibrahimu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,
35 mwana wa Seruig, mwana wa Ragau, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala,
36 mwana wa Kenani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Nuhu, mwana wa Lameki,
37 mwana wa Methusela, mwana wa Henoko, mwana wa Yaredi, mwana Mahalalei, mwana wa Kenani,
38 mwana wa Enoshi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, mwana wa Mungu.